Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kama pale angeKuwa anakuja Ole peke ake ningekua na mashaka sana na maamuz ya bodi ya Man united, Ila kwa kuweka wale watu wawil nyuma ya Ole kwa maana ya Phelan na mwenzie plus Carrick Let us give him the chance to prove to us ule utamaduni wa Manchester United uliopotea toka alipoondoka Fergie,

Tusisahau Phelan was the Man behind Fergie's success so kuna vitu atakuja kuongeza pale kutokana na uzoefu wake wa team na Ligi kwa ujumla.

Kwa sasa we are United with Ole.
 
Wakuu tumeletewa kocha wa zamani wa Cardif city ambaye aliishusha daraja
Mainz 04 ya ujeruman ilitaka kushuka daraja ikiwa mikononi mwa klopp borusi dortmund ilinusurika kushuka daraja mikononi mwa klopp hadi alifukuzwa kazi kisha akaja liverpool

Zidane aliishusha daraja real madrid castilla

Luis enrique alifukuzwa roma na celta vigo kisha akabeba ndoo 5 na barcelona

Sioni point yako hapo ukikosa wachezaj makini ukikutana na timu ngumu utapigwa tu

Angalia wolves endapo mbele wangekuwa na top players ingakuwaje?

Acha baby face apige kazi na bench zima la ufundi aliifundisha morde ya norway ilikuwa timu tishio mwama wa 2015/16 hadi rosenberg akawa anapata tabu timu iliharibika baada ya injuriea na kuuza wachezaji alikuja cardif timu ambayo tayar ilishapoteza uelekeo

Sina wasiwasi na benchi la ufundi ni suala la muda.
 
Solskjaer amefundisha Molde na Cardiff ambayo aliishusha daraja sasa uzoefu mkubwa ni upi
Huwezi kumlinganisha na scholes wala michael carick solskjaer ana uzoefu mzur tu aliipeleka molde europa baada ya kumaliza wa pili nyuma ya rosenberg hii ni baada ya kutolewa kwenye mchujo wa uefa wao wanatoa timu moja kucheza champions league
 
"HATA MAJIVU YA MWILI WA BILL SHANKLY YALIKUSANYIKA TENA"

Usiku mmoja wa saa 00.30 Usiku wa tarehe 29.09.1981 kwenye hospitali ya Broadgreen iliyopo Jiji la Liverpool ilitoka taarifa Baba wa klabu ya Liverpool FC amefariki dunia.
Siyo mwingine ni Bill Shankly.. Liverpool ni Bill Shankly na Shankly ni Liverpool FC. Ndani ya miaka 15 aliyofanya kazi Kama mkufunzi mkuu wa timu ya Liverpool FC aliitengenezea misingi migumu na imara ambayo hata sasaivi bado inaishi.

Ndani ya uwanja wa Anfield hairuhusiwi mechi yeyote kuanza mpaka walevi wao watakapomaliza sala yao takatifu ya wimbo wa "U Will Never Walk Alone ",Ndani ya Anflied Kuna jukwaa maalumu linaitwa "The Kop End" ambalo linanuka marashi ya majivu ya mwili wa marehemu Bill Shankly.

Yapo mengi Achana na uwepo wa kibao cha "THIS IS ANFIELD, Achana na uwepo wa kiwanja cha MELWOOD ambacho Shankly mwenyewe alikuwa anaamini hapo ndipo mahali maalumu kwa ajili ya "Askofu" mkuu kuandalia muongozo wa ibada.

Kwanini hata majivu ya Bill Shankly yalikusanyika tena?

Jibu ni Kiwango kitakatifu kilichooneshwa na Liverpool FC siku ya jumapili ya tarehe 16.12.2018 kwenye ardhi takatifu ya Anfield.
Niliingalia jinsi timu ya Manchester united ilivyonyanyasika chini ya mikono ya mjerumani Jurgen Klopp ,nikaangalia kwenye jukwaa flani la V.I.P nikaiona sura ya Sir Alex Ferguson imekuwa nyekundu huku akitingisha kichwa kwa ishara ya kusikitika .
Nikasafiri mpaka kwenye jukwaa wanaokaa watu maalumu waliokulia Liverpool FC na kukutana na sura ya Sir King Kenny Daglish Nikaona jinsi anavyotabasamu kwa furaha baada ya mechi kuisha.

Hiyo Ndiyo Liverpool FC ambayo marehemu Bill Shankly aliijenga na kuagiza siku akifa mwili wake uchomwe moto na majivu yake kusambazwa kwenye jukwaa la The Kop End, hiyo Ndiyo Liverpool ambayo Steven Gerrard ameagiza siku akifa mwili wake usipelekwe mortuary bali ukawekwe katikati ya kiwanja cha Anfield.

Siku zote kwenye maisha yake fundi Bill Shankly alikuwa anaamini ni laana kubwa Sana Liverpool FC kuwa chini ya Manchester United au Evarton na Ndiyo maana akaja na usemi usemao "In Liverpool city there only two best teams and those teams are Liverpool FC and Liverpool Reserves "

Anachofanya saivi Jurgen Klopp ni kurudi kwenye misingi ya Bill Shankly ambapo alikuwa akiamini katika mambo makuu mawili ambayo ni umuhimu wa mchezaji kufahamu kwanini kavaa jezi ya Liverpool FC na mchezaji anatakiwa kufahamu Melwood ni uwanja wa vita wa wajerumani.

Yapo mengi ya kuwasimulia wadogo zangu ambao hawaijui Liverpool FC zaidi ya kuijua kwenye makundi ya Whatsap na kwenye Odds za kubet, lakini ninachoamini siku ya Jumapili majivu ya mwili wa Bill Shankly yalikusanyika kwa furaha kutokana na mateso waliyopitia Manchester United kwa dakika 90.

Ni Nadra Sana kwa Mtukutu Kama Jose Morinho kwenda kwenye "Post Match Press Conference " na kukiri mbele ya vyombo vya habari kuwa alipitia mateso makubwa Sana kwenye ardhi ya adui.. Ila jumapili Morinho alikiri kupitia mateso makubwa sana na kukiri kuwa ilikuwa ni mechi ya mbingu na ardhi.

Kwa heshima ya jumapili naamini Billy Shankly kabakiza deni moja kwa Jurgen Kloop ambalo ni kuwapa Kombe Liverpool FC.
Hiyo Ndiyo Liverpool FC ambayo watoto wasioijua Liverpool FC wakawa wanakesha mitandaoni wakipiga porojo kuwa Napoli anaenda kuwatoa Liverpool FC kwenye UEFA Champion League , hiyo ndiyo Liverpool ambayo Pep Gurdiola anasema anapenda kusoma vitabu lakini kila akiiwaza anaacha kusoma kitabu, hiyo ndiyo Liverpool ambayo mwaka 1997 kuliwekwa Jukwaa la Bill Shankly nje ya jukwaa la the Kop End kuwakumbusha wachezaji shujaa huyo.

Wanaoweza kujua vizuri kuwa majivu ya Bill Shankly yalikusanyika tena Anfield kwa furaha ni Marehemu Bob Paisley, Joe Fagan na Renben Bennett.

Hiyo Ndiyo Liverpool ambayo iliamua kutoa misa takatifu kwa Manchester United na Kunikumbusha Liverpool ya akina Phil Neal, Alan Hansen na Ian Rush.

Kilichotokea Jumapili ni Liverpool FC kuipa Manchester United PENZI la Ghetto ambalo Kanye West anampa Kim Kardashian.. Kama Hujui Penzi la ghetto tafuta video ya Kanye West na Kim Kardashian wakiwa Ikulu ya Uganda kwa Yoweri Kaguta Museven.

Ashante Jurgen Kloop kwa kusababisha majivu ya Bill William Obe Shankly kukusanyika kwa Mara nyingine ndani ya ardhi tukufu ya Anfield

Montelo 10

Kapumzike Mourinho nenda Inter Milan ukamalizie ufalme wako ulioshindwa kusimama OT, najua team pinzani hazitamani kukutana na Liverpool kwa sasa duh noma sana
we nae mechi moja tu kelele kibao fala we
 
Je lilikuwa suluhisho kumtimua Jose mourinho?
Je baada ya kumtimua matatizo ya man united yatakuwa yamekwisha?
Je tatizo la man united lilikuwa mourinho au wachezaji?
Je baada ya mourinho kuondoka man united itaanza kufanya vizuri?

Ni maswali ninayojiuliza
 
Je lilikuwa suluhisho kumtimua Jose mourinho?
Je baada ya kumtimua matatizo ya man united yatakuwa yamekwisha?
Je tatizo la man united lilikuwa mourinho au wachezaji?
Je baada ya mourinho kuondoka man united itaanza kufanya vizuri?

Ni maswali ninayojiuliza
Suala la muda tu ila kuna wachezaj walikuwa washamchoka
 
Je lilikuwa suluhisho kumtimua Jose mourinho?
Je baada ya kumtimua matatizo ya man united yatakuwa yamekwisha?
Je tatizo la man united lilikuwa mourinho au wachezaji?
Je baada ya mourinho kuondoka man united itaanza kufanya vizuri?

Ni maswali ninayojiuliza
Jose' Mourihno alikuwa ameshaanza kutudharau hata sisi mashabiki..kufukuzwa kwake kuna mambo mengi na sio guarrantee kuwa tuchukua trebble siku sio nyingi..No,tunachohitaji ni timu iimarike na icheze kama timu kubwa duniani
 
Mainz 04 ya ujeruman ilishuka daraja ikiwa mikononi mwa klopp borusi dortmund ilinusurika kushuka daraja mikononi mwa klopp hadi alifukuzwa kazi kisha akaja liverpool

Zidane aliishusha daraja real madrid castilla

Luis enrique alifukuzwa roma na celta vigo kisha akabeba ndoo 5 na barcelona

Sioni point yako hapo ukikosa wachezaj makini ukikutana na timu ngumu utapigwa tu

Angalia wolves endapo mbele wangekuwa na top players ingakuwaje?

Acha baby face apige kazi na bench zima la ufundi aliifundisha morde ya norway ilikuwa timu tishio mwama wa 2015/16 hadi rosenberg akawa anapata tabu timu iliharibika baada ya injuriea na kuuza wachezaji alikuja cardif timu ambayo tayar ilishapoteza uelekeo

Sina wasiwasi na benchi la ufundi ni suala la muda.

Sawa Mkuu ngoja tusubiri tuone itakuaje
 
Sky Sports understands the Portuguese manager was also unwilling for the club to change its model and bring in a sporting director, as Arsenal did during the summer, but Neville told a The Debate special now was the time for United to step up to the plate and restructure their off-field operation.

Kumbe Mou hakutaka hili
 
Je lilikuwa suluhisho kumtimua Jose mourinho?
Je baada ya kumtimua matatizo ya man united yatakuwa yamekwisha?
Je tatizo la man united lilikuwa mourinho au wachezaji?
Je baada ya mourinho kuondoka man united itaanza kufanya vizuri?

Ni maswali ninayojiuliza
Jambo jema kuhusu haya mabadiliko yaliyoanza kufanywa jana na leo ni pamoja kutafuta Director of Football ambaye ataanza kazi kabla ya summer

Klabu kua na Director of football ndio mfumo wa kisasa unaotumiwa na vilabu vikubwa duniani. Huyu ni daraja kati kocha na wachezaji (footballing factor) na CEO na board (administrative factor na commercial factor)

Uwepo wa Director of football utafanya kocha aajiriwe kwa kuzingatia filosofia ya club na wachezaji wasajiliwe kwa mujibu wa filosofia ya club

So haya mabadiliko yaliyoanza jana yanaweza kuwa na matokeo chanya (ya haraka) na/au ya muda mrefu
 
Back
Top Bottom