Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Jose Mourinho amefutwa kazi wadhifa wake kama meneja wa Manchester United.

Klabu hiyo imetangaza kwamba ameondoka katika klabu hiyo mara moja.

"Klabu hii ingependa kumshukuru Jose kwa kazi yake kipindi ambacho amekuwepo Manchester United na inamtakia kila la heri siku za usoni."

Meneja mpya wa muda atateuliwa kuongoza klabu hiyo hadi mwisho wa msimu, huku klabu hiyo ikiendelea na mchakato wa kumtafuta meneja mpya wa kudumu."

Mourinho, 55, amekuwa Old Trafford kwa miaka miwili unusu pekee, baada ya kuchukua mikoba kutoka kwa Mholanzi Louis van Gaal mwezi Mei mwaka 2016.

Mreno huyo alikuwa ametia saini kandarasi mpya mnamo mwezi Januari ambayo iliimarisha mafao na mahitaji yake ya kikazi mbali na kumuongezea kandarasi yake hadi mwaka 2020.

Alishinda Kombe la Ligi na Europa League akiwa Manchester United lakini kwa sasa wamo alama 19 nyuma ya viongozi wa Ligi Kuu ya England kwa sasa, ambao ni Liverpool waliowachapa 3-1 Jumapili.

Hali ya United kwa sasa, ambapo wamezoa alama 26 pekee baada ya kucheza mechi 17 za msimu Ligi ya Premia ndiyo mbaya zaidi katika historia ya klabu hiyo hatua kama ya sasa tangu msimu wa 1990-91.

Wamo alama 11 nyuma ya klabu nne za kwanza kwenye jedwali, ambazo hufuzu kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Wanakaribia zaidi eneo la kushushwa daraja kuliko kileleni.

Yamkini mwezi Desemba si wa bahati kwa Mreno huyo, alifutwa kazi tarehe 17 Desemba mwaka 2015 na klabu ya Chelsea baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.

The Blues walikuwa wameshinda Ligi ya Premia msimu uliotangulia lakini msimu huo mambo yakawaendea kinyume, na walikuwa alama moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja ligini.

Kejeli za Paul Pogba

Paul Pogba ambaye ameonekana kuzozana na Mourinho siku za karibuni na amekuwa hachezeshwi tena katika kikosi cha kuanza mechi ameandika ujumbe ulioonekana kuwa wa kejeli kwenye Twitter kisha akaufuta.

Mourinho amezozana kwa muda na Mfaransa huyo aliyenunuliwa kwa bei iliyovunja rekodi ya klabu hiyo ya £89m.

Pogba alikuwa benchi na hakuchezeshwa katika mechi hiyo ambayo walichapwa na Liverpool uwanjani Anfield Jumapili.

Baada ya kutoka sare 1-1 na Wolves wiki chache zilizopita, Pogba alisema angependa United wawe wakishambulia na kushambulia na kushambulia wakiwa nyumbani.

Hilo lilimfanya Mourinho kudai kwamba Mfaransa huyo hangekuwa nahodha msaidizi wa klabu hiyo tena.

Pogba alimjibu kwamba hahitaji kitambaa hicho cha nahodha.

Oktoba, zilitokea taarifa kwamba Mourinho huenda angefutwa kabla ya mechi yao dhidi ya Newcastle iwapo wangeshindwa.

Lakini baada yakuwa nyuma 2-0, walijikwamua na kushinda 3-2 na meneja huyo wa zamani wa Chelsea, Inter Milan na Real Madrid akapata muda zaidi.

Wakala wa Mourinho, Jorge Mendes alijaribu kutuliza wasiwasi mapema Desemba kwa kuchukua hatua isiyo ya kawaida ya kutoa taarifa rasmi kusema Mourinho ana furaha sana, na kwamba amejitolea kuendelea kuhudumu katika klabu hiyo.

Lakini hata licha ya kufuzu kwa hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambapo wamepangwa kucheza na Paris St-Germain ya Ufaransa, wameshinda mechi moja pekee ligini kati ya sita walizocheza karibuni.

Kufutwa kwa Mourinho kunaendeleza historia yake ya kutomaliza misimu mitatu mfululizo katika klabu moja.

Ni wakati mmoja tu ambapo alifanikiwa kuhudumu msimu wa nne, lakini aliondoka Chelsea 17 Desemba 2015 wakati wa kipindi chake cha pili Stamford Bridge.

Manchester United wamedokeza kwamba watamteua meneja mpya wa muda.

Lakini hatakuwa meneja msaidizi Michael Carrick au meneja wa akademi Nicky Butt.

Atakuwa ni mtu kutoka nje ya klabu hiyo, lakini hatakuwa meneja wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger.

Baadhi wanamzungumzia Zinedine Zidane aliyekuwa meneja wa Real Madrid.

Yupo pia meneja wa zamani wa Chelsea Mwitaliano Antonio Conte.

Yupo pia meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone na meneja wa sasa wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino.
 
Nimemdharau mkuu

Hawa ndio wale wasioelewa maana loyalty kwa timu, sio kocha ..... Kwa timu
Umejiunga Jamii forum May 2018 unaanza kudharau expert members ambao tumepitia mitikisiko mikubwa kwenye harakati zetu za kumuondoa Nduli JOSE MOURINHO.

Hatimaye tumefanikiwa unaanza kuzarau jitihada za sisi manguli ambao uwezo Wetu wa kupambana na Gaidi Mou ilitubidi tukatae nafsi zetu. Sadly hujui mijadala iliyokuwa humu mwaka Jana kuhusu mou ndio maana umerukia kuwa unatudharau. Kaa chini na wahenga upewe ABC..
 
Mimi nitamuuliza swali dogo tu

Hivi mtu akiponda kila kitu, narudia tena MTU AKIPONDA KILA KITU anachofanya Darmian uwanjani, ama Rojo je hutawatetea? Ina maana hawana mazuri?

Wanajua maana ya loyalty ??
 
Nimemdharau mkuu

Hawa ndio wale wasioelewa maana loyalty kwa timu, sio kocha ..... Kwa timu
Wao wanafikir kocha akiondoka basi utaacha kushabikia timu

Mimi ni mshabiki wa timu nzima hadi bench la ufundi tukifanya vibaya tunasema tukishinda tunasema wao timu ikishinda wapo kimyaaa iktandikwa wanaibuka kocha atoke
 
Mimi nitamuuliza swali dogo tu

Hivi mtu akiponda kila kitu, narudia tena MTU AKIPONDA KILA KITU anachofanya Darmian uwanjani, ama Rojo je hutawatetea? Ina maana hawana mazuri?

Wanajua maana ya loyalty ??
Hatar sana mkuu kuna chenga alilambwa harrera na mane goli la pili giggs akauoizwa ule ndo ujinga aliotumwa na kocha kukaba vile kizembe? Kuna vitu hutokea tu
 
Let's all take a moment and laugh at the sinking ship (Man United) and their sacked special one Moureen.

Hahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaahahahahahaha
 
Sawa wewe mmarekani
Hata kama Kocha haumkubali inatakiwa uwe professional sio baada ya kutimuliwa wewe unaenda Instagram kuonesha wewe ni zaidi
Usichokijiua wenzetu wanathamini saaaaaaana tena sana Uhuru wa maoni kama ulivyokuwa speculated na Universal Declaration Of Human Rights.

Kwahiyo mtu kuonesha hisia zake ni kosa ???? Come on young Babylon. Wenzetu wenye high level of civilisation wameshapita huko kwenye kwenye barbaric living era. Ni mwendo wa ukweli na uwazi. Ndio maana schooles tangu kuchaguliwa Mou mpaka Leo hamkubali.

Unakumbuka beef la Pogba na mou lilianzia wapi ?? Ni huko huko instagram. Halafu kama mou na yeye angekuwa proffesional asingekuwa anampiga benchi Valencia kwa sababu za kipuuzi. Najua unazijua hizo SAbabu.

Hebu acha vijana wafurahi bana. Kama Mimi niliyeko huku Nanjilinji Nina furaha ya kumuondoa huyu Mpuuzi sembuse vijana walioko kule kwa malkia?
 
Mimi ni United Fan sio shabiki wa Mou
Kiungo wetu pogba anaangaika sana na nywele kuliko uwanjani juzi kama ulimsikiliza roy Kean sky sports utanielewa
Kuangaika na nywele kwan kaanzia man utd! vitu vingine hua ni mambo binafsi hutakiwi hata kuingilia afu huyo Roy kean yale yalikua ni mawazo yake tu sio sheria ww pia unaweza ukatoa mawazo yako sio eti kwa sababu flani kasema!
 
Umejiunga Jamii forum May 2018 unaanza kudharau expert members ambao tumepitia mitikisiko mikubwa kwenye harakati zetu za kumuondoa Nduli JOSE MOURINHO.

Hatimaye tumefanikiwa unaanza kuzarau jitihada za sisi manguli ambao uwezo Wetu wa kupambana na Gaidi Mou ilitubidi tukatae nafsi zetu. Sadly hujui mijadala iliyokuwa humu mwaka Jana kuhusu mou ndio maana umerukia kuwa unatudharau. Kaa chini na wahenga upewe ABC..
Hivi huu ushamba wa kusema umejiunga juzi mnautoa wapi? Hivi mtu aliyejiunga juzi hana haki ya kuhoji, kutoa michango humu?

Any way, kuweka kumbukumbu sawa ID ya Mc Cane ni ya hiyo tarehe lakini wanajamii forum wamekuwa wakiona michango yangu (sio ya ID ya MC Cane) tangu kitambo sana

Pia nilikuwa sijajua kama Mourinho yupo humu JF, hongera kwa kumtumbua Mou wa JF mkuu

Pia naendelea kukushauri usishabikie matusi
 
Usichokijiua wenzetu wanathamini saaaaaaana tena sana Uhuru wa maoni kama ulivyokuwa speculated na Universal Declaration Of Human Rights.

Kwahiyo mtu kuonesha hisia zake ni kosa ???? Come on young Babylon. Wenzetu wenye high level of civilisation wameshapita huko kwenye kwenye barbaric living era. Ni mwendo wa ukweli na uwazi. Ndio maana schooles tangu kuchaguliwa Mou mpaka Leo hamkubali.

Unakumbuka beef la Pogba na mou lilianzia wapi ?? Ni huko huko instagram. Halafu kama mou na yeye angekuwa proffesional asingekuwa anampiga benchi Valencia kwa sababu za kipuuzi. Najua unazijua hizo SAbabu.

Hebu acha vijana wafurahi bana. Kama Mimi niliyeko huku Nanjilinji Nina furaha ya kumuondoa huyu Mpuuzi sembuse vijana walioko kule kwa malkia?
sawa lakini huyu mtu mweusi mwenzetu hana professionalism kabisa, ilitakiwa kukausha tu sababu kama sikosei ni jose ndiyo amemsajili pogba, Pogba anatakiwa azingatie mpira na aachane na nywele mara instagram yote kwa yote timu ya Man United wapiga kazi wachache sana
 
Umejiunga Jamii forum May 2018 unaanza kudharau expert members ambao tumepitia mitikisiko mikubwa kwenye harakati zetu za kumuondoa Nduli JOSE MOURINHO.

Hatimaye tumefanikiwa unaanza kuzarau jitihada za sisi manguli ambao uwezo Wetu wa kupambana na Gaidi Mou ilitubidi tukatae nafsi zetu. Sadly hujui mijadala iliyokuwa humu mwaka Jana kuhusu mou ndio maana umerukia kuwa unatudharau. Kaa chini na wahenga upewe ABC..
Halafu kumbe umejiunga 2014

Ndio unanikosoa mimi kwamba nimejiunga juzi

You are very junior kwangu in terms of JF membership mzee
 
Kuangaika na nywele kwan kaanzia man utd! vitu vingine hua ni mambo binafsi hutakiwi hata kuingilia afu huyo Roy kean yale yalikua ni mawazo yake tu sio sheria ww pia unaweza ukatoa mawazo yako sio eti kwa sababu flani kasema!
These budah have got very cheapest logic to support their arguments to undermine Le Dance, POGBA.

Mou nilivyoona ameanza beef na Pogba nikajua hiyo ndio safari. Kwa wanaonisoma humu I said this early. Ngao ya mou kubaki man u kwa jinsi alivyokuwa na beef na wachezaji ilikuwa ni yeye ashinde mataji Tuuuuuu. Kinyume na hapo ilikuwa ni suala la muda tu.

Zaidi akaanza mibifu na watu wanaoingizia hela team akiwemo Pogba na uwanjani hakuna la maana , hapa hata masau bwile lazima akufukuze hahahaha.
 
Mimi nitamuuliza swali dogo tu

Hivi mtu akiponda kila kitu, narudia tena MTU AKIPONDA KILA KITU anachofanya Darmian uwanjani, ama Rojo je hutawatetea? Ina maana hawana mazuri?

Wanajua maana ya loyalty ??
Bad thing is wewe bado Mpya kwenye hili jukwaa. Vitu vingine zama PM tukusaidie.

Narudia tena huu Mjadala umeukutia njiani. Hayo yote uliyouliza ukirudisha page za hii thread nyuma utakuta majibu mujarabu.

Watu tulikuwa tumepoa humu kwasababu tulikuwa kwenye vita vikali vya kumuondoa huyu ibilisi.
 
Usichokijiua wenzetu wanathamini saaaaaaana tena sana Uhuru wa maoni kama ulivyokuwa speculated na Universal Declaration Of Human Rights.

Kwahiyo mtu kuonesha hisia zake ni kosa ?

Something might be legal but unethical.

Kama ni sahihi, kipi kimemfanya afute?
 
sawa lakini huyu mtu mweusi mwenzetu hana professionalism kabisa, ilitakiwa kukausha tu sababu kama sikosei ni jose ndiyo amemsajili pogba, Pogba anatakiwa azingatie mpira na aachane na nywele mara instagram yote kwa yote timu ya Man United wapiga kazi wachache sana
Is kukausha Legal or Moral Duty???

Yaani kuna vifungo vya sheria vinamtaka akaushe ??? Kama ndio basi kakosea. Ila kama kukausha ni suala la kuamua basi hajakosea. That's moral duty.
 
Back
Top Bottom