Mkuu nimekuelewa sana lakini kuna maeneo inabidi tuweke sawa
Ni kweli Lindelof na Bailly walikuwa ni machaguo ya Mourinho, lakini si machaguo ya kwanza
Mou amekuwa akieleza kila msimu unapoelekea kuisha kuwa kazi yake ni kutoa list of names katika namba anayotaka kununua, kwa hiyo hapa huwa anaweka orodha hata ya wachezaji 4 au 5 kwa mpangilio wa umuhimu ili Ed anunue mmoja wapo
Kwa rekodi ya Mou ya kutaka wachezaji ambao ni already proven players, tutajidanganya tukisema Lindelof na Bailly walikuwa ni machaguo ya kwanza ya Jose. Wale walikuwa ni potential zaidi, na Ed huwa anapenda potential players sababu ya resale value yao. Kwahiyo hawa walikuwa ni machaguo ya kwanza ya Ed na Glazer family kwa kuwa ilikuwa ni convenient kwao kibiashara kuwa na mchezaji ambaye unaweza kumtumia miaka 8, na bado ukaja ukamuuza kwa £ 40 mil.
Ukirudi kwa beki za pembeni, Mou alikiwa anajitaji sana beki wa pande zote 2, wa kulia na kushoto. Kulia hakuweka mkazo sana kutokana na dhana ya kuweka kipaumbele, ambapo aliona kushoto ni tatizo zaidi. KWENYE HILI JOSE ALIKOSEA, HUWA SI PATIENT KWA WACHEZAJI VIJANA WANAOPOTOKA. Hii imejitokeza hata kwa Martial ambaye alitaka kuondoka kwa sehemu hiyo ilisababishwa na José lakini na yeye Martial alikiwa ana shida kwenye attitude yake.
Kuhusu kununua baadhi ya wachezaji na kuto click kama kocha alivyotazamia, Jose hatakuwa wa 1 wala wa mwisho. Nimetoa mfano jana kwa Guadiola wa Claudio Bravo, pia kuna Mhisipania mmoja alikuja msimu 1 tu City kisha akarejea Hispania (ukihitaji jina nitakutafutia). Fergie aliwanunua akina Djemba Djemba, Bebe, Oberten n.k ambao wakaishia kuwa ma flop
Mil. 30 ni ndogo sana kwa beki wa kati kwenye post Ronaldo, Bale, Pogba and Neymar Market, unless uwe unataka uwe timu ya mid table kwenye msimamo wa ligi ya Premier kama akina Everton