Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

kitatokezea kitu gani kama tukiamua kumrudisha eneo la ulinzi wa kati nemanja matic halafu herrera na perreira wakawa wanabadilisha nafasi ya namba 6.
kuna baadhi ya timu si lazima uziwekee walinzi wa nne wa asili
matic amekuwa mzito sana msimu huu kwa kila kitu.
Matic anatakiwa kumpisha herrera hilo lipo wazi ujio wake ulisababisha herrera kupoteza kiwango chake si mzur ktk ulinz wakat herrera anakupa vitu viwili ulinz na kushambulia
 
Hata 10 akicheza pogba mkuu nyuma yao akae herrera
hahahahaaaaa nemanja matic mtoto wa mourinho akae benchi?
unataka jose mourinho atukanwe tena kwa kusajili useless player kwa fedha nyingi, ndio maana nikashauri jamaa arudishwe mlinzi wa kati ili kuendelea kuweka hali ya hewa sawa kwenye timu.
herrera kiupande mwengine anastahili kurudishiwa heshima yake ya miaka miwili nyuma aliyojijengea klabuni.

msimu uliopita ujio wa nemanja matic ulituaminisha tutacheza 4-3-3 kwenye mechi zetu lakini ikawa kinyume chake kwa sababu hata huyu pogba akiwa namba 10 mechi nyingi tunazocheza hali ya timu yetu inakuwa vile vile.
mimi nadhani solution ni ndogo sana tunachopaswa kufanya ni kurudisha tena makali yetu eneo la pembeni kwa kusajili winga na mabeki wenye spidi kama nyakati za fergie kwa sababu tayari tumeshaonyesha udhaifu chini ya mourinho hatuna uwezo wa kucheza soka la kasi tunapowatumia viungo watatu wa asili.
 
hahahahaaaaa nemanja matic mtoto wa mourinho akae benchi?
unataka jose mourinho atukanwe tena kwa kusajili useless player kwa fedha nyingi, ndio maana nikashauri jamaa arudishwe mlinzi wa kati ili kuendelea kuweka hali ya hewa sawa kwenye timu.
herrera kiupande mwengine anastahili kurudishiwa heshima yake ya miaka miwili nyuma aliyojijengea klabuni.

msimu uliopita ujio wa nemanja matic ulituaminisha tutacheza 4-3-3 kwenye mechi zetu lakini ikawa kinyume chake kwa sababu hata huyu pogba akiwa namba 10 mechi nyingi tunazocheza hali ya timu yetu inakuwa vile vile.
mimi nadhani solution ni ndogo sana tunachopaswa kufanya ni kurudisha tena makali yetu eneo la pembeni kwa kusajili winga na mabeki wenye spidi kama nyakati za fergie kwa sababu tayari tumeshaonyesha udhaifu chini ya mourinho hatuna uwezo wa kucheza soka la kasi tunapowatumia viungo watatu wa asili.
Kweli mkuu suala la 7 na 11 wa maana linatusumbua sana hii ni point.
 
kuna mdau mmoja ameshauri tucheze mpira wa kasi ili tuweze kuwadhibiti maadui na pia kuongeza kiwango cha utengenezaji wa magoli.
kwa uelewa wangu mdogo wa mpira nina imani ya kuwa soka la kasi msingi wake ni wachezaji wa pembeni ndipo wanafuatia viungo wa kati. Timu nyingi zinazofanya vizuri kwenye soka kwa kiasi kikubwa sana wanaringia wachezaji wao wa pembeni ndipo zinafuata sehemu nyenginezo.


  • kipindi cha nyuma tuliringia uwepo wa beckham, giggs,ronaldo, evra, park ji sung, luis nani
  • unaikumbuka bayern munich iliobeba ubingwa pale wembley kwa kuifunga dortmund , walikuwa na lahm, alaba, robben, ribery, shaqiri.
  • hata barcelona hivyo hivyo hawana masihara kwenye kutafuta wachezaji wa pembeni kuanzia dani alves, jordi alba, david villa, iniesta, coutinho, dembele,henry, messi.
  • waangalie madrid maeneo yao ya pembeni kwa miaka 3 walikuwa moto, carvajal, marcelo, bale, ronaldo, isco na hata asensio,
  • hata juventus na wao wameanza kubadilika kipindi hiki na kuamua kuwekeza eneo la pembeni, jaribu kurejea usajili wa dani alves, alex sandro, douglas costa, ronaldo, cuadrado.
  • PSG wanaringia uwezo wa dimaria, mbappe, neymar, muniri, alves,draxler.
kwetu sisi miaka 6 hii tumekuwa tofauti sana, tuna wachezaji wenye majina lakini uwezo ni mdogo wanapokuwa uwanjani.
antonio valencia, ashley young, alex sanchez, matteo darmian,lingard mpaka ulimwegu utakwisha hawawezi kukupa faida kwenye soka la kushambulia.
ule msemo wa fyekelea mbali unahitajika kwenye timu yetu.

Ashley Young Reportedly Eyeing New 2-Year Contract at Manchester United.
mkuu hivi kweli menejimenti yetu ipo serious?
Ashley Young ni mchezaji Muhimu sana pale Man u kwa sasa.
1 Moja yeye ba smalling na Valencia ndiyo wanaoijua Man u kuliko mchezaji mwingine yeyote ndiyo maana umeona amepewa arm band na mechi zote ambazo amekuwa captain tumeshinda except mechi na Chelsea.

2 ndiye mchezaji pekee anayeweza kucheza zaidi ya position nne kwenyr kikosi na bado akaoffer Kitu uwanjani mfano.
Anacheza fullbacks zote, anaweza cheza wing ya kushoto na kulia, na anaweza cheza kama inside ten
Hivi unafikiri Galeth southgate alikuwa mjinga kumtumia Young world cup ?

3 anapace na anauwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi za magoli,

4 ni mpambanaji kweli kweli toka Valencia akae bench huyu jamaa anacheza kulia wakati yeye hucheza left back au wing ya kushoto

5 team bado haina mbadala wake kwa sasa ndiyo maana wanaendelea kumpa mkataba.

Ungesema kuhusu.
Valencia
Lukaku
Darmian
Phil Jones
na fellain ningekuelewa siyo kwa Ashley Young
 
Nakubaliana na wachambuzi wengi hapa kwamba mpira wa asili wa MUFC ni mpira wa kasi kwa kutumia wingers. Kipindi cha AF magoli mengi yalitokea pembeni. Umaarufu wa Van Nestory, Rooney, Cole nk ulichangiwa sana na mipira ya kutoka pembeni. David Beckam, CR, Valencia, Gigs na Nani walipata umaarufu kwa mipira ya pembeni. Evra alitisha sana kwasababu ya kupanda na kupiga cross.

Kuna umuhimu wa kupata typica wingers pia back 2 na 3 wanaoweza kupanda na kupiga cross kama ilivyo kuwa Real Madrid ya akina Roberto Carlos na Cafu.
 
heshima kwako rafiki.
nathubutu kusema comment yako japokuwa ni fupi sana ila kiupande wangu naichukulia ni miongoni mwa comment bora kwa siku ya leo ikifuatiwa na comment ya Darmian ambayo alikuwa anazungumzia performance isiyoridhisha ya Nemanja Matic msimu huu unaoendelea. navutiwa sana na mshabiki wa mpira mwenye tabia na mtazamo kama upepo unaovuma kwa kasi kuliko mshabiki wa mpira mwenye tabia na mtazamo usiobadilika, bahati mbaya sana humu ndani washabiki wengi hatuna tabia za upepo unaovuma kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

kiupande wangu nipo tofauti sana ukilinganisha na baadhi ya wachangiaji wengine wenye msimamo mmoja tu na hata ukijaribu kuzipitia comment zangu zilizopita ndani ya thread hii utagundua ya kwamba maandishi yangu yana nafsi mbili (hupendelea kuwasilisha mawazo yangu kwa kuangalia zaidi muda uliopo). Sisi wengine mpaka muda huu hatujajiingiza kwenye starehe za ulevi, kamari, ngono zembe na hata kufuatilia video za ovyo kama za amber rutty na wajinga wengineo lakini tunapoteza muda mrefu sana kwa ajili ya kufuatilia starehe ya mpira wa miguu, sote tunafahamu machungu na madhila tunayoyapata pindi starehe unayoipendelea inapokwenda kinyume na matarajio yako uliojiwekea.

Sababu kubwa iliyonifanya ninukuu comment ya brother hapo juu ni kuhusiana na jambo moja tu ambalo kiupande wangu naliona halipo sawa kwenye klabu yetu tunayoishabikia na kadri siku zinavyosogea jambo hilo nyeti mizizi yake inazidi kwenda chini ya ardhi bila ya kutafutiwa ufumbuzi, jambo hilo si jengine isipokuwa ni sera za kutafuta wachezaji wapya (usajili)

ukweli utatuweka huru na haijalishi ukweli huo ni mchungu, jamani klabu yetu ya Manchester united tumekuwa ovyo sana kwenye soko la kutafuta wachezaji watakaoweza kuendana na misingi ya timu yetu na ugonjwa huu ulianza tokea wakati wa utawala wa Sir Alex Ferguson.
Babu yetu fergie miaka yake 4 ya mwisho alianza kuonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye soko la usajili jambo la kushukuru zaidi soko la ushindani wa ligi kuu nyakati za fergie ilikuwa ni afadhali sana ukilinganisha na nyakati hizi. Japokuwa wachezaji hao hao wenye viwango vya kawaida walikuwa wanatupa ubingwa wa ligi kuu lakini udhaifu wao ulikuwa unaonekana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ambapo mara nyingi tulikuwa tunaishia kufungishwa virago na timu zilizo makini kwenye soko la usajili zaidi yetu. Sina nia ya kumdhihaki ferguson ambaye CV yake ni kubwa na nzito zaidi ya mlima wa kilimanjaro ila najaribu kuonyesha ni wapi udhaifu wa timu yetu ulipoanzia na bado mpaka sasa udhaifu huo unaendelea kututafuna.
nimebaki najiuliza maswali yafuatayo muda huu?​

  • je wasaka vipaji wetu wamepoteza nuru kupitia jicho lao la tatu ambalo ndio muhimu zaidi pindi unapomchunguza mchezaji unayemuhitaji?
  • je inawezekana makocha wetu wamepoteza uwezo wa kuweza kumtambua ni yupi mchezaji atakayefaa kwenye falsafa zake na hatimaye wanaamua kucheza kamari la usajili?
  • je inawezekana tatizo ni wachezaji wenyewe wanaosajiliwa wakija klabuni kwetu wanacheza kwa pressure sana jambo linalopelekea kupoteza kujiamini wakiwa uwanjani?
  • je inawezekana tumeingia kwenye mkumbo wa laana tokea nyakati za mwisho za ferguson lakini hatukuweza kuligundua mapema suala hilo la kusajili wachezaji watakaofiti kwenye timu, na kama tumeingia kwenye mkumbo wa laana ina maana hata kama tutamsajili mungu wa mpira lionel messi na malaika wake wa mpira kama mbappe, neymar watakuwa ni flop ndani ya klabu yetu?
  • je inawezekana mawakala na viongozi wa timu pinzani wanatumia udhaifu wetu wa kutaka kurudisha heshima ya klabu kwa haraka hivyo basi wanatuuzia wachezaji wenye viwango vya kawaida kwa fedha nyingi sana, rejea usajili wa lindelof, lukaku, fred,pogba, sanchez, tetesi za maguire na alderweireld kwa 60 millioni pounds.
nyakati za mwisho za utawala wa sir alex ferguson biashara pekee ya maana ilikuwa ni usajili wa chicharito ambaye hata kama leo angelikuwepo kwenye klabu yetu angelistahili kupata nafasi japo dakika 30
  1. klabu ilimuuza cristiano ronaldo ambaye ana uwezo wa kufunga magoli 40 kwa msimu cha ajabu anayerithi nafasi yake alikuwa ni antonio valencia ambaye mpaka leo hii sidhani kama amefikisha angalau magoli 40 ndani ya miaka 10 hii tokea asajiliwe manchester united. Kiwango chake kisichoridhisha kimechangia kwa kiasi kikubwa arudishwe eneo la ulinzi wa kulia, hata huku kwenye nafasi yake mpya amekuwa na kiwango kisichoridhisha na ndiye chanzo kikuu cha timu yetu kupoteza makali upande wa kulia kwa miaka hii.
  2. jaribu kuangalia usajili wa chris smalling kutoka fulham: fergie alikubali kuzidiwa kete na jose mourinho kwenye dili la varane kwa sababu ya smalling ambaye thamani yake ilikuwa ni paundi 10 millioni kama ilivyo kwa varane alipotoka lens ya ufaransa. huu ni mwaka wa saba jamaa kiwango chake hakieleweki wakati varane cv yake ni nzito. media za uingereza zilimjaza ujinga mzee wetu na kama kawaida yake akaonyesha mapenzi yake tena kwa wachezaji wa kiingereza, cha ajabu mimi niliyekuwepo huku nchi za kimasikini njaa kali niliamini ya kwamba smalling aling'arishwa zaidi na mwanadamu kutoka norway ambaye sura yake ilifanana na nemanja vidic muheshimiwa brade hangeland pale fulham.Cha ajabu smalling bado ameendelea kuwa sehemu ya tatizo hata nyakati hizi wakati huo huo tunamyemelea varane kwa dau la zaidi ya 60 millioni paundi.
  3. usajili wa Ashley young kutoka aston villa:nimeanza kumfahamu ashley tokea nipo shule ya msingi kipindi hicho anachezea watford akiwa bado na pumzi za kutosha (kinda), baadae akapiga mpira mwingi sana Aston villa chini ya mwalimu martin o'neill mpaka wakafikia hatua ya kugombania top 4 msimu ulee wa federico macheda alipotuinua kwenye viti dakika za nyongeza, miaka michache mbele ashley young alipoteza muelekeo wa kisoka na alizidiwa kiuwezo hata na steward downing na gabriel agbonlahor. hivi tukiachana na mechi ile tuliyomfunga arsenal magoli 8 ni mechi ipi nyengine ambayo young alionyesha kiwango cha maana akiwa uwanjani? Ashley young ameendelea kuwa ni sehemu ya tatizo kwenye klabu yetu ila cha kustaajabisha mourinho na bosi wake ed woodward wanafanya naye mazungumzo ya kumpa mkataba mpya.
  4. bila ya kuwasahau akina buttner, bebe, anderson, gabriel obertan.
utawala wa david moyes kutoka everton

  • mpaka leo najiuliza ina maana huyu moyes alikuwa haangalii rekodi za mechi za manchester united kabla hajaanza kibarua chake na kwa nini akatumia 30 millioni paundi kwa ajili ya marouanne fellaini, alipokuja manchester david tulikuwa na washambuliaji watatu lakini bwana yule akamleta fellaini awe namba 10 wetu. Fellaini ameendelea kuwa ni sehemu ya tatizo kwenye timu yetu hadi leo hii na hakuna kiongozi yeyote anayejali uchovu wa fellaini.Kocha na mtendaji mkuu anayekwenda na wakati hawezi kumpa mkataba mpya fellaini na hutomuona mchezaji mwenye uwezo kama wa fellaini kwenye timu kubwa isipokuwa manchester united
utawala wa van gaal

  1. huyu mzee ndio kazidisha majanga miaka yake miwili ya kazi, kamleta matteo darmian kwa 15 millioni ambaye hana cha maana alichokileta kwenye klabu yetu.
  2. kamleta morgan schneiderlin kwa 26 millioni paund na yeye amefeli, kamleta blind amefeli, depay pressure kubwa amefeli, di maria pressure kubwa amefeli.
  3. luke shaw baada ya miaka minne kupita kidogo ameanza kuonyesha mwanga wa kuonyesha thamani yake.
utawala wa jose mourinho

hizi zimekuwa ni nyakati za mawakala na viongozi wa timu kujikusanyia fedha nyingi kutokana na mauzo ya wachezaji wenye viwango vya kawaida wanapokuja manchester united. Leo hii tumekuwa hatuna tofauti kubwa sana na madada poa (makahaba) ambao huuza miili yao kwa ajili ya kupata pesa ya mkate na sabuni.
  • makahaba wanawapa wateja wao huduma kwa fedha kidogo japokuwa inasemekana huduma ya amber rutty (sijawahi kuona video yake) inakuwa na dau kubwa wakati manchester united tunatoa fedha nyingi kwa ajili ya kupewa huduma ya mchezaji aisiyetabirika.hawa mawakala akiwemo mino raiola, mendez wanatufanyia uhuni sana kipindi hiki.
usajili wa Fred
Inaumiza sana pale unapo endelea kushuhudia klabu ikiendelea kufanya makosa yenye kujirudia kila panapo funguliwa dirisha la usajili, tumefanya makosa kwa sanchez, lindelof, pogba (105 million pounds), dimaria n.k

Hivi kweli Fred huyu anayezidiwa kimpira na moussa dembele ana thamani ya paundi millioni 55 ?​
United tumepoteza muelekeo kiasi ambacho tunalipa hela ndefu kwa mchezaji ambaye hana uwezo wa kuingia kikosi cha kwanza nyakati hizi, sasa kwa nini tukamsajili au uvumi wa kutaka kuwapokonya tonge manchester city una ukweli ndani yake?

kule klabuni shakhtar donetsk,mchezaji Taras stepanenko alikuwa anacheza kiungo wa chini na fred akawa anacheza nafasi ya kiunganishi cha timu(box to box) wakati huku kwetu anayecheza nafasi hiyo ni paul pogba, kivyovyote fred hawezi kumweka nje paul pogba na vile vile hawezi kumweka nje nemanja matic ili awe kiungo mkabaji.
kocha akiwapanga wote watatu kwa pamoja tunakuwa wazito sana kuwasogelea maadui, ina maana benchi la ufundi walikuwa hawayajui haya?


fedha ya usajili wa fred ilipaswa itumike kwanza kwa ajili ya kumsajili mchezaji atakayetupa faida papo kwa papo hata kama ni mlinzi na si kumsajili mchezaji wa kusubiri mchezaji fulani apate majeruhi ndio apewe nafasi. Tuwatazame manchester city wamelipa paundi millioni 50 kwa ajili ya ryad mahrez ambaye tayari ana uwezo wa kuendana na kasi ya ligi kuu ya uingereza pamoja na mechi kubwa, kiukweli klabu imefanya tena biashara ya kijinga sana na viongozi wa shakhtar wana haki ya kutukejeli kwa kuwapa hela nyingi.

mbona manchester city wamelipa pesa nyingi kwa bernard silva, gundogan, danilo, mendy, jesus na bado wanakaa nje?
ukweli mwengine tusioupenda mashabiki wa manchester united ni kuhusiana na viwango vya wachezaji wetu ukiwalinganisha na wachezaji wa manchester city.
Tumekuwa tukijidanganya na kujiaminisha ya kwamba wachezaji wetu wana viwango sawa na wachezaji na timu nyengine ila tunakosa mwalimu mzuri wa kutengeneza wachezaji wetu wachezae vizuri.
Baada ya kuangalia mechi za msimu huu napingana na wale wanaoamini ya kwamba tuna wachezaji bora kama mancheter city, chelsea,liverpool na timu nyengine kubwa barani ulaya, nusu na robo ya wachezaji wetu wana majina maarufu sana lakini wakiwa uwanjani wapo ovyo kuliko soda aliokunywa bwana harusi wa UDSM.
Wenzetu bado wanaendelea na steji ya kujenga timu ya ushindani ukilinganisha na upande wetu sisi ambao bado tumeendelea kulala usingizi huku tukiringia historia.

bernard silva, gundogan, danilo, mendy wote hao wanapopewa nafasi kikosi cha kwanza wanacheza vizuri sana ukilinganisha na wachezaji wetu tuliowasajili kwa gharama kama vile lukaku, bailly, lindelof.
kwa hali tukiofikia hatuna haki ya kujilinganisha na miamba ya soka la bara la ulaya kama juventus, barcelona, madrid, atletico madrid, man city na hata liverpool.

siku ambayo fred atacheza vizuri nitakuja kumsifia humu ndani ila naogopa kusema iyo siku iko mbali sana.
View attachment 920544
Khaaa watu mnachambua
 
Screenshot_20181104-230522.jpg
 
Teams to score 5+ goals in a league game since Man Utd last did it in May 2013.

1.Manchester City 21 times
2.Liverpool 12
3.Tottenham 9
4.Arsenal 8
5.MK Dons 8
6.Peterborough 8
7.Bournemouth 7
8. Chelsea 7
9.Brentford 6
10.Derby 6
11.Hull 6
12.Bristol City 5
13.Cambridge 5
14.Norwich 5
15.Watford 5
16.Accrington 4
 
Teams to score 5+ goals in a league game since Man Utd last did it in May 2013.

1.Manchester City 21 times
2.Liverpool 12
3.Tottenham 9
4.Arsenal 8
5.MK Dons 8
6.Peterborough 8
7.Bournemouth 7
8. Chelsea 7
9.Brentford 6
10.Derby 6
11.Hull 6
12.Bristol City 5
13.Cambridge 5
14.Norwich 5
15.Watford 5
16.Accrington 4
Can you put the number of trophy they won during that time?
 
Back
Top Bottom