Lampard Frank Lampard alimzidi vitu vingi sana kiufundi Jose Mourinho katika mchezo wa Manchester United 2(7)-2(8) Derby Country.
Mpira ni mchezo wa wazi sana, unapozidiwa shurti uaibike na ndicho Mwanafunzi alichomfanya Mwalimu wake wa zamani.
Jose Mourinho ana vipindi vyake, hiki ni miongoni mwa vipindi vyake, bahati mbaya tu United hawana Doctor wa Kike aidhinishe safari aliyoizoea Jose Mourinho.
Frank Lampard identity yake tactically imeonekana na niliipenda zaidi ule mguu wa Wilson machoni mwa Romero mbele ya ukuta wa faulu.
Kilichobaki kwa Jose ni kuhesabu alichokivuna na sio atakachokivuna.

hahahahahaaaaaa nilikuwa najisemea nafsini mwangu baada ya kukupa like hapo juu natamani Lyon Lee atoe mchango wake humu ndani kuhusiana na hali ngumu inayomkabili jose mourinho muda huu, ahsante sana inaonekana ombi langu umelisikia huko uliko.

tokea nianze kufuatilia mpira wa miguu ni mara yangu ya kwanza kushuhudia timu inapoteza pambano kabla haijaingia uwanjani kwa dhumuni la kupambana na adui wake wa ukweli. Hali ya hewa tuliokuwa nayo nchini Marekani tukijiandaa na maandalizi ya msimu huu ilionyesha dhahiri kitakachotukuta kwenye ligi, Inastaajabisha sana muda huu tumebaki tunapokea dhihaka na kejeli zisizokwisha kutoka kwa wapinzani wetu wenye kelele.
sioni dalili yoyote tena ya jose mourinho kuliokoa jahazi la manchester united lililozama umbali wa mita 100 kutoka usawa wa nchi kavu tena nyakati hizi za asubuhi.

Tunamuhitaji nahodha ambaye hatokuwa na visingizio vya ajabu kama vile kutokuwepo kwa jenereta litakalotoa muangaza kwa ajili ya kuendeleza zoezi la uokoaji wa miili iliyozama asubuhi hii, Ni ipi khatma ya mwanadamu huyu pindi atakapoondoka manchester united.

  1. chelsea = sidhani kama watakubali kufunga tena ndoa na mwanadamu huyu mwenye kelele nyingi
  2. real madrid = pia sidhani kama watamhitaji tena mourinho endapo kocha wao wa sasa atakapofanya vibaya.
  3. inter milan = bado wanamuona ni kama nabii kiupande wao ila sifikirii kama mourinho atarudi Italia.
jose mourinho alitumia nguvu kubwa sana kutengeneza CV yake ila cha ajabu anatumia tena nguvu kubwa kuiharibu CV yake.

ila ningependa jose mourinho aondoke pamoja na ed woodward japo kuwa ni ngumu jambo hili kutokea, ni rahisi zaidi kwa familia ya glazer kuiuza manchester united kuliko kuishi bila ya ed woodward.
1537962386362.png
Manchester United earn record revenues but still have debt of £487m
 
Kweli pengine wanaosema adui wa kwanza ni mtu wako wa karibu ,fanya kana kwamba jana mechi haijachezwa make kilichotokea ni sawa na mtoto kumkana babake ...kuna kitu nilikuwa naanza kukifatiliaa na kukiogopaa pale OT (usiulize mimi niko chama kipi ) kabla ya kutegemea hiki kinachoendelea hivi yule mwanadamu Fred asume ndo kashaadapt full then chezesha akili anapokuwa drafted alongside Matic alafu behind kuna rafiki yangu Pogba bwanabwanah ufalme wa mzee baba Pogba nilikuwa naanza kuuandikia insha sema ndo hivo mzee wao kaona cha kufia nini ufalme ujengwe kwanza kwake mengine ya uwanjan tusubirie uwepo wa mzee fagiiii kwenye kile kichumba chake pale juu...
 
Back
Top Bottom