Manchester United (Red Devils) | Special Thread

jamii forums Where we Dare to Talk Openly!
huyu Damushin wa leo na wa jana ni watu wawili tofauti lakini cha kushangaza wote wanatumia account moja hapa JF.
hahahahahahahahahaha (하하하아하하하아) naandika hii comment nikiwa najicheka mwenyewe kwanza na naamini na leo mutanivumilia kama jana nilipotofautiana na jose mourinho na falsafa zake.
naanza na nukuu zifuatazo zilizotolewa na watu muhimu sana ndani ya klabu yetu ambao kwa sasa wametufanya mashabiki tugawanyike pande mbili.

  • jose mourinho : msimu ujao michael carrick ataungana nami kwenye benchi la ufundi, marouanne fellaini hatma yake haijulikani hivyo basi kama wote wataondoka tunahitaji kuziba nafasi zao na pia tunahitaji kuimarisha kikosi chetu baadhi ya maeneo na tayari nimeshaweka mezani mipango yangu kwa bosi wangu (ed woodward)
  • jose mourinho baada ya kufungwa na sevilla : hivi munadhani sevilla ni timu nyepesi wakati kuna baadhi ya wachezaji wana uwezo wa kuchezea manchester united.
  • jose mourinho : josep guardiola amerithi kikosi bora manchester city kuliko mimi na bado anasajili wachezaji bora, tusipokuwa makini itakuwa ni vigumu sana kuwakamata majirani zetu wenye kelele (maneno ya mwisho nimeongeza mimi)
  • ed woodward : tuko vizuri sana kwenye eneo la kibiashara kuliko timu yoyote duniani na matokeo ya ndani ya uwanja hayaleti athari kubwa sana kwenye biashara zetu.
  • ed woodward: manchester united ndiyo timu pekee yenye uwezo wa kumsajili mchezaji yoyote kwenye soko la usajili bila ya kupata athari yoyote na kwa hilo namuahidi kocha nitayafanyia kazi mapendekezo yake
  • ed woodward : mourinho amefanya kazi ngumu sana hapa manchester united na amezidi kudhihirisha ya kwamba anastahili kupewa mkataba mpya.
upande wa pili wa shilingi tunapaswa tufahamu ya kwamba mourinho huyu ndiye
  1. yule yule aliyewapa ubingwa fc porto kwa mfumu wake pendwa wa kujilinda zaidi huku akimpa nafasi ya uhuru fundi deco souza kuwa kiungo huru.
  2. ndiye yule yule aliyekuja uingereza miaka miwili ya mwanzo na kumdhalilisha ferguson na timu yake na pia kuweka rekodi ya kuchukua ubingwa kwa point 95 na kuruhusu goli 15 msimu mzima kwa kutumia zaidi mfumo wa kujilinda na kumpa nafasi ya uhuru fundi frank lampard, Ina maana hata kocha wetu ferguson hakuwahi kuifikia rekodi yake. na bila ya kusahau msimu wake wa pili alibeba ubingwa kwa kutufunga goli 3 hku wayne rooney akiumizwa mguu na ricardo carvalho mwanadamu aliyemfanya john terry aonekane ni mlinzi bora kumbe ni kama dejan lovren wa liverpool, na kwa ushahidi wa hilo alipoondoka ricardo carvalho ndio ukawa mwisho wa john terry (naruhusu povu kwa mashabiki wa chelsea)
  3. ndiye mourinho huyu huyu aliyeifunga barcelona ya guardiola akiwa na inter milan kwa mfumo ule ule wa kujilinda zaidi na huku akimpa nafasi ya uhuru fundi wesley sneijder.
  4. ndiye mourinho huyu huyu aliyepata dawa ya kupambana na barcelona ya guardiola kwa kutumia mfumo huu huu wa kujilinda kwa kumtumia pepe na msimu wake wa pili akawapa real madrid ubingwa kwa kuweka rekodi ya kukusanya pointi nyingi kwenye historia ya laliga, na pia kutengeneza timu iliyowapa mafanikio carlo ancelotti na zinedine zidane, ina maana hata guardiola hakuifikia rekodi ya kukusanya point 100 na kushinda mechi 32 za ligi kuu kwa msimu mmoja..
maswali tunayopaswa kujiuliza sisi mashabiki, wapenzi na wapiga kelele wa manchester united
  • je wakati bodi ya klabu ya manchester united wanampa kazi jose mourinho walikuwa hawafahamu ya kwamba huyu jamaa anacheza mpira wa kujilinda zaidi?
  • wakati wanampa mkataba walikuwa hawafahamu ya kwamba huyu jamaa hana tabia ya kuwavumilia wachezaji wake pindi wanapokuwa ovyo?
  • bodi walikuwa hawafahamu ya kwamba huyu jamaa ni mtumiaji wa pesa sana kama alivyofanya chelsea na real madrid?
mnamo 28 July 2009 akiwa Inter Milan alizungumza maneno yafuatayo
"I would consider going to Manchester United but United have to consider if they want me to succeed Sir Alex Ferguson. If they do, then of course."
bila ya shaka walikuwa wanayafahamu yote na ndio maana walifikia makubaliano pande zote mbili ya kufanya kazi pamoja.na huyu special one.
sasa kwa nini manchester united wanashindwa kumtimizia mahitaji yake ya kusajili wachezaji haliyakuwa ed woodward ameshajisifu mara nyingi sana ya kwamba klabu ina uwezo wa kumsajili mchezaji yoyote anayetakiwa na mwalimu.
kwa kutumia akili zangu za GPA ya 32 kwa kauli ya ed woodward anamaanisha ya kwamba manchester united wana uwezo wa kuinunua liverpool na wafanyakazi wote na pesa ya kuisaidia bajeti ya wizara ya kilimo ya Tanzania ikabakia.

  1. tukiangalia upande wa pili wa majirani zetu wenye kelele josep guardiola alirithi manchester city ikiwa imeishia nafasi ya 4 kwenye msimu wa 2015/2016 na pia kutolewa nusu final ya mashindano ya champions league na akaanza kufanya mabadiliko makubwa sana ya wachezaji ambao aliwaona hawana faida kiupande wake.
  2. Timu iliishia nusu final kwenye ligi ya mabingwa lakini bado aliwaondoa wachezaji wafuatao kwa misimu miwili hii/
joe hart, bacary sagna, gael clichy, zabaleta pablo, alexander kolarov, samir nasri, jesus navas, wilfried bony, mangala, martin demicheliss na kelechi iheanacho.
ukiangalia list ya wachezaji hawa pia kwenye timu yetu utagundua kuna wachezaji vilaza kuliko walioachwa na guardiola.
na kwa akili zangu za GPA ya 40 ukiniambia nichague kati ya ashley young + luke shaw dhidi ya alexander kolarov nitamchagua alexander kolarov mmoja kuliko hao wawili kwa pamoja
msimu wake wa kwanza akafanya usajili wa wachezaji wafuatao​
claudio bravo, ikay gundogan, john stones, nolito, leroy sane na gabriel jesus.

wakati huo huo nasisitiza tena alirithi timu yenye wachezaji kama david silva, yaya toure, kevin de bruyne, sergio aguero, vicent kompany, otamendi nicolas, fernandinho, raheem sterling na ukiangalia kwa umakini utagundua ya kwamba ni yaya toure pekee ndiye asiyekuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
sasa kwa nini mourinho aliyerithi timu yenye wachezaji kama smalling, jones, young, shaw, valencia, lingard, mata mvivu,rooney kibonge awekewe ngumu kwenye usajili?
.
msimu wake wa pili akawaongezea mafundi wafuatao​
kyle walker, ederson, bernardo silva, danilo, laporte, benjamin mendy na msimu huu kamuongezea ryad mahrez.

ukija huku kwetu utastaajabu ya mussa na farao
  1. wakati guardiola anamuondoa nolito kwa kutokuendana na falsafa yake msimu wake wa pili alionekana malaika lakini mourinho alipomuondoa mkhitaryan kwa kushindwa kuwa kwenye kiwango msimu wake wa pili alionekana ni shetani.
  2. wakati guardiola anathubutu kufanya usajili wa makipa wawili ndani ya kikosi cha kwanza kwa bei iliovunja rekodi anaonekana ni malaika lakini special one anapoweka maombi ya kuongezewa mlinzi mmoja wa kati mwenye roho ngumu kama bonucci kwa ajili ya kukaza basi lake anaonekana ni shetani.
  3. wakati guardiola anasajili walinzi wawili wa kushoto huku akimuondoa mlinzi mwengine mahiri ambaye ni kolarov anaonekana ni malaika lakini huku kwetu the special one anapoomba apewe fungu la usajili kwa ajili ya alex sandro anaonekana ni shetani asiye na uvumilivu, unabaki kujiuliza kama ni guardiola je angeliendelea kumtumia luke shaw na ashley young kama walinzi wake haliyakuwa amemuondoa alexandre kolarov na gael clichy?
  4. kama guardiola aliweza kuwandoa wachezaji kama mangala na demichelis je kama angelikuwepo manchester united angeliendelea kufanya kazi na wachezaji kama smalling na phil jones.?
bodi ya klabu wanapaswa waendelee kumpa fedha za kutosha jose mourinho bila ya kuhoji matumizi yake kama wanavyofanya manchester city kwa makocha wao.
fikiria alipokuwa chelsea aliwasajili robben, wright phillips, drogba, ferreira, essien, mikel obi, darmian duff, carvalho na kwa kutumia mfumo wake pendwa wa kupaki basi aliwapa ubingwa miaka miwili mfululizo na alitudhalilisha sisi wazee wa attack attack chini ya sir alex ferguson

kwa kutumia mfumo wake pendwa wa kupaki basi amefikisha point 81 msimu uliopita huku baadhi ya mechi ni wachezaji wenyewe ndio walizifanya ziwe ngumu.
nadhani sote tunakumbuka kwenye mechi ya leicester city marcus rashford alikosa magoli ya wazi akiwa peke yake na goli sasa kwa nini tumlaumu mourinho kwa makosa ya rashford kukosa umakini hali ya kuwa bodi inafahamu fika ya kwamba mourinho hana tabia ya kumfundisha mtu mpira?
“We have top players and, sorry if I'm arrogant, we have a top manager,
Please don't call me arrogant, but I'm European champion and I think I'm a special one.

je mwenye makosa ni mourinho au ni bodi yetu ya manchester united?

natamani hii comment aisome rafiki yangu radika peke yake na pro mourinho lakini ndio haiwezekani
hahahahaaaa hii comment wasije wakaiona Darmian na Daud1990 na anti mourinho wengineo humu ndani.
ila thread imechangamka sana siku hizi
kuna mchangiaji mmoja alimstishia mwenzake humu ndani atampiga ngumi huko huko aliko nikabaki najiuliza swali inamaana hizi keyboard za siku hizi zina uwezo wa kufanya mashambulizi kwa mtu aliye mbali?
ngoja nywila (password) yangu niitupe baharini nisije nikarushiwa ngumi za keyboard.
kinyonga 😎😎
mourinho oyeeeeee zidane wa nini wakati bodi imeridhishwa na basi letu?
0_GP22587500.jpg
Kwa ruhusa yako naomba nami leo niandike kidhungu;

You have nailed it all - thank you!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
How comes acheze ovyo na ashinde?? The team which plays well is awarded 3 points and the only criterion in footbal is a win or a draw. There is no any other measurable criterion you can apply to determine a team which plays well. Other isssues are mere illusions based on feelings of individuals.

Sent using Jamii Forums mobile app
Time will tell us

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhai wa kufungwa na brighton 3? Au kucheza mpira wa kuzuia tu ndio uhai?
Hivi kuna timu isiyopigwa? Mwaka jana madrid kapigwa nyumbani na real betis ilikuwaje? Tuwe na subra bana
 
Ole Gunnar Solskjaer made his United bow #OnThisDay in 1996...

366 games
126 goals

Muda mwingi aliutumia akiwa bench na kuuguza majeraha lakini alifanya vitu vikubwa mno
FB_IMG_1535171717408.jpg
 
Sasa man u jumatatu mtafua dafu mbele ya Pochettino? Mara ya mwisho mnakutana alikupiga. Kama kiungo mnayotegemea ndo aina ya pogba na asipobadilika basi jiandaeni na kipigo kingine maana hakuna namna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jamii forums Where we Dare to Talk Openly!
huyu Damushin wa leo na wa jana ni watu wawili tofauti lakini cha kushangaza wote wanatumia account moja hapa JF.
hahahahahahahahahaha (하하하아하하하아) naandika hii comment nikiwa najicheka mwenyewe kwanza na naamini na leo mutanivumilia kama jana nilipotofautiana na jose mourinho na falsafa zake.
naanza na nukuu zifuatazo zilizotolewa na watu muhimu sana ndani ya klabu yetu ambao kwa sasa wametufanya mashabiki tugawanyike pande mbili.

  • jose mourinho : msimu ujao michael carrick ataungana nami kwenye benchi la ufundi, marouanne fellaini hatma yake haijulikani hivyo basi kama wote wataondoka tunahitaji kuziba nafasi zao na pia tunahitaji kuimarisha kikosi chetu baadhi ya maeneo na tayari nimeshaweka mezani mipango yangu kwa bosi wangu (ed woodward)
  • jose mourinho baada ya kufungwa na sevilla : hivi munadhani sevilla ni timu nyepesi wakati kuna baadhi ya wachezaji wana uwezo wa kuchezea manchester united.
  • jose mourinho : josep guardiola amerithi kikosi bora manchester city kuliko mimi na bado anasajili wachezaji bora, tusipokuwa makini itakuwa ni vigumu sana kuwakamata majirani zetu wenye kelele (maneno ya mwisho nimeongeza mimi)
  • ed woodward : tuko vizuri sana kwenye eneo la kibiashara kuliko timu yoyote duniani na matokeo ya ndani ya uwanja hayaleti athari kubwa sana kwenye biashara zetu.
  • ed woodward: manchester united ndiyo timu pekee yenye uwezo wa kumsajili mchezaji yoyote kwenye soko la usajili bila ya kupata athari yoyote na kwa hilo namuahidi kocha nitayafanyia kazi mapendekezo yake
  • ed woodward : mourinho amefanya kazi ngumu sana hapa manchester united na amezidi kudhihirisha ya kwamba anastahili kupewa mkataba mpya.
upande wa pili wa shilingi tunapaswa tufahamu ya kwamba mourinho huyu ndiye
  1. yule yule aliyewapa ubingwa fc porto kwa mfumu wake pendwa wa kujilinda zaidi huku akimpa nafasi ya uhuru fundi deco souza kuwa kiungo huru.
  2. ndiye yule yule aliyekuja uingereza miaka miwili ya mwanzo na kumdhalilisha ferguson na timu yake na pia kuweka rekodi ya kuchukua ubingwa kwa point 95 na kuruhusu goli 15 msimu mzima kwa kutumia zaidi mfumo wa kujilinda na kumpa nafasi ya uhuru fundi frank lampard, Ina maana hata kocha wetu ferguson hakuwahi kuifikia rekodi yake. na bila ya kusahau msimu wake wa pili alibeba ubingwa kwa kutufunga goli 3 hku wayne rooney akiumizwa mguu na ricardo carvalho mwanadamu aliyemfanya john terry aonekane ni mlinzi bora kumbe ni kama dejan lovren wa liverpool, na kwa ushahidi wa hilo alipoondoka ricardo carvalho ndio ukawa mwisho wa john terry (naruhusu povu kwa mashabiki wa chelsea)
  3. ndiye mourinho huyu huyu aliyeifunga barcelona ya guardiola akiwa na inter milan kwa mfumo ule ule wa kujilinda zaidi na huku akimpa nafasi ya uhuru fundi wesley sneijder.
  4. ndiye mourinho huyu huyu aliyepata dawa ya kupambana na barcelona ya guardiola kwa kutumia mfumo huu huu wa kujilinda kwa kumtumia pepe na msimu wake wa pili akawapa real madrid ubingwa kwa kuweka rekodi ya kukusanya pointi nyingi kwenye historia ya laliga, na pia kutengeneza timu iliyowapa mafanikio carlo ancelotti na zinedine zidane, ina maana hata guardiola hakuifikia rekodi ya kukusanya point 100 na kushinda mechi 32 za ligi kuu kwa msimu mmoja..
maswali tunayopaswa kujiuliza sisi mashabiki, wapenzi na wapiga kelele wa manchester united
  • je wakati bodi ya klabu ya manchester united wanampa kazi jose mourinho walikuwa hawafahamu ya kwamba huyu jamaa anacheza mpira wa kujilinda zaidi?
  • wakati wanampa mkataba walikuwa hawafahamu ya kwamba huyu jamaa hana tabia ya kuwavumilia wachezaji wake pindi wanapokuwa ovyo?
  • bodi walikuwa hawafahamu ya kwamba huyu jamaa ni mtumiaji wa pesa sana kama alivyofanya chelsea na real madrid?
mnamo 28 July 2009 akiwa Inter Milan alizungumza maneno yafuatayo
"I would consider going to Manchester United but United have to consider if they want me to succeed Sir Alex Ferguson. If they do, then of course."
bila ya shaka walikuwa wanayafahamu yote na ndio maana walifikia makubaliano pande zote mbili ya kufanya kazi pamoja.na huyu special one.
sasa kwa nini manchester united wanashindwa kumtimizia mahitaji yake ya kusajili wachezaji haliyakuwa ed woodward ameshajisifu mara nyingi sana ya kwamba klabu ina uwezo wa kumsajili mchezaji yoyote anayetakiwa na mwalimu.
kwa kutumia akili zangu za GPA ya 32 kwa kauli ya ed woodward anamaanisha ya kwamba manchester united wana uwezo wa kuinunua liverpool na wafanyakazi wote na pesa ya kuisaidia bajeti ya wizara ya kilimo ya Tanzania ikabakia.

  1. tukiangalia upande wa pili wa majirani zetu wenye kelele josep guardiola alirithi manchester city ikiwa imeishia nafasi ya 4 kwenye msimu wa 2015/2016 na pia kutolewa nusu final ya mashindano ya champions league na akaanza kufanya mabadiliko makubwa sana ya wachezaji ambao aliwaona hawana faida kiupande wake.
  2. Timu iliishia nusu final kwenye ligi ya mabingwa lakini bado aliwaondoa wachezaji wafuatao kwa misimu miwili hii/
joe hart, bacary sagna, gael clichy, zabaleta pablo, alexander kolarov, samir nasri, jesus navas, wilfried bony, mangala, martin demicheliss na kelechi iheanacho.
ukiangalia list ya wachezaji hawa pia kwenye timu yetu utagundua kuna wachezaji vilaza kuliko walioachwa na guardiola.
na kwa akili zangu za GPA ya 40 ukiniambia nichague kati ya ashley young + luke shaw dhidi ya alexander kolarov nitamchagua alexander kolarov mmoja kuliko hao wawili kwa pamoja
msimu wake wa kwanza akafanya usajili wa wachezaji wafuatao​
claudio bravo, ikay gundogan, john stones, nolito, leroy sane na gabriel jesus.

wakati huo huo nasisitiza tena alirithi timu yenye wachezaji kama david silva, yaya toure, kevin de bruyne, sergio aguero, vicent kompany, otamendi nicolas, fernandinho, raheem sterling na ukiangalia kwa umakini utagundua ya kwamba ni yaya toure pekee ndiye asiyekuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
sasa kwa nini mourinho aliyerithi timu yenye wachezaji kama smalling, jones, young, shaw, valencia, lingard, mata mvivu,rooney kibonge awekewe ngumu kwenye usajili?
.
msimu wake wa pili akawaongezea mafundi wafuatao​
kyle walker, ederson, bernardo silva, danilo, laporte, benjamin mendy na msimu huu kamuongezea ryad mahrez.

ukija huku kwetu utastaajabu ya mussa na farao
  1. wakati guardiola anamuondoa nolito kwa kutokuendana na falsafa yake msimu wake wa pili alionekana malaika lakini mourinho alipomuondoa mkhitaryan kwa kushindwa kuwa kwenye kiwango msimu wake wa pili alionekana ni shetani.
  2. wakati guardiola anathubutu kufanya usajili wa makipa wawili ndani ya kikosi cha kwanza kwa bei iliovunja rekodi anaonekana ni malaika lakini special one anapoweka maombi ya kuongezewa mlinzi mmoja wa kati mwenye roho ngumu kama bonucci kwa ajili ya kukaza basi lake anaonekana ni shetani.
  3. wakati guardiola anasajili walinzi wawili wa kushoto huku akimuondoa mlinzi mwengine mahiri ambaye ni kolarov anaonekana ni malaika lakini huku kwetu the special one anapoomba apewe fungu la usajili kwa ajili ya alex sandro anaonekana ni shetani asiye na uvumilivu, unabaki kujiuliza kama ni guardiola je angeliendelea kumtumia luke shaw na ashley young kama walinzi wake haliyakuwa amemuondoa alexandre kolarov na gael clichy?
  4. kama guardiola aliweza kuwandoa wachezaji kama mangala na demichelis je kama angelikuwepo manchester united angeliendelea kufanya kazi na wachezaji kama smalling na phil jones.?
bodi ya klabu wanapaswa waendelee kumpa fedha za kutosha jose mourinho bila ya kuhoji matumizi yake kama wanavyofanya manchester city kwa makocha wao.
fikiria alipokuwa chelsea aliwasajili robben, wright phillips, drogba, ferreira, essien, mikel obi, darmian duff, carvalho na kwa kutumia mfumo wake pendwa wa kupaki basi aliwapa ubingwa miaka miwili mfululizo na alitudhalilisha sisi wazee wa attack attack chini ya sir alex ferguson

kwa kutumia mfumo wake pendwa wa kupaki basi amefikisha point 81 msimu uliopita huku baadhi ya mechi ni wachezaji wenyewe ndio walizifanya ziwe ngumu.
nadhani sote tunakumbuka kwenye mechi ya leicester city marcus rashford alikosa magoli ya wazi akiwa peke yake na goli sasa kwa nini tumlaumu mourinho kwa makosa ya rashford kukosa umakini hali ya kuwa bodi inafahamu fika ya kwamba mourinho hana tabia ya kumfundisha mtu mpira?
“We have top players and, sorry if I'm arrogant, we have a top manager,
Please don't call me arrogant, but I'm European champion and I think I'm a special one.

je mwenye makosa ni mourinho au ni bodi yetu ya manchester united?

natamani hii comment aisome rafiki yangu radika peke yake na pro mourinho lakini ndio haiwezekani
hahahahaaaa hii comment wasije wakaiona Darmian na Daud1990 na anti mourinho wengineo humu ndani.
ila thread imechangamka sana siku hizi
kuna mchangiaji mmoja alimstishia mwenzake humu ndani atampiga ngumi huko huko aliko nikabaki najiuliza swali inamaana hizi keyboard za siku hizi zina uwezo wa kufanya mashambulizi kwa mtu aliye mbali?
ngoja nywila (password) yangu niitupe baharini nisije nikarushiwa ngumi za keyboard.
kinyonga 😎😎
mourinho oyeeeeee zidane wa nini wakati bodi imeridhishwa na basi letu?
0_GP22587500.jpg
Great thinker's comment

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani wolves ndio wangekuwa utd dhidi ya city leo. Ni timu iliyopanda daraja lakini city wanapata tabu sana.
Hii game inatuonyesha kuwa utd hatuna mtu sahihi kama mwalimu wa timu.
 
Back
Top Bottom