Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,062
- 43,489
1. Hata defense ya van gaal ilikuwa nzuri, tofauti ya van gaal na mou ni kwamba sasa hivi tunafunga zaidi, kipindi cha lvg tulikuwa hatufungi wala hatufungwi draw za suluhu zilikuwa nyingi ama 1-1Southgate aliposema "sitajali hali ya rashford kule man u atakuwepo Russia" unaweza itafsiri hii kauli kwa namna gani!? Kuhusu lukaku nimesema naamini alikuwa na uwezo Wa kusaidia kuliko hapo ila mfumo mbovu Wa Mwl ndo kikwazo. Kuhusu defence kama sikosei tofauti ya magoli ya kufungwa kati ya mou na van gaal ni kama 7 tu hivi. Nasema ni defence mbovu kwa sababu hii ya mou iliundwa na timu nzima na wachezaji wengine walinyimwa nafasi ya kuonyesha uwezo wao kwa sababu wote wanatakiwa kuwa mabeki na viungo wakati ile ya van gaal watu walifunguka zaidi
2. So mtu akijitamba kwa waandishi wa habari na kuongea mambo mengi na asiyatimize tuamini matendo yake ama maneno yake? Nimekuuliza swali uwanjani namna southgate alivyomtumia Rashford kuna utofauti gani na alivyomtumia mou? Hujanijibu unanilitea press conference,
3. Lvg pia hawakupewa nafasi, kila kocha na mfumo wake, ndio maana mou anataka watu wake, kama mchezaji hafit huo mfumo. Mfano lvg ana tabia ya kuchezesha watu namba sio zao toka enzi hizo, di maria kuwa striker, robben kuwa striker, bastian toka winga hadi kiungo mkabaji, rooney striker to midfielder, enrique alikuwa striker mpaka akawa full back, watu nao wanalalamikia hivyo lakini huo ndio mfumo wake.
Kipindi bodi ya man u inamchukua mou ilijua fika ni kocha wa kujihami hivyo ni responsibility yao kumpa wachezaji wanaojua huo mfumo na sio kumpangia mou afanye nini yeye ndio kocha na ana final say, na utamaduni wa man u tunasimama na kocha wetu hadi mwisho wa safari, haya mambo ya kuchukia chukia mengi yanaletwa na glory hunters.