Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Sioni vizuri naomba mnionyeshe Manure United iko wapi
IMG-20180321-WA0045.jpg
 
Man Utd Managers Win Percentages:

MOURINHO 61.8%
FERGUSON 60.1%
MANGNALL 54.1%
MOYES 52.9%
VAN GAAL 52.4%
BUSBY 50.5%
ATKINSON 50%
WALLWORTH 50%
GIGGS 50%
DOHERTY 46.9%
ALBUT 44.6%
WEST 40.7%
SEXTON 40.3%
DUNCAN 39.1%
BENTLEY 39.1%
CHAPMAN 39.1%
CRICKMER 39%
O’FARRELL 37%
 
naona mnamfananisha Mata na takataka zenu acheni ujinga Mata ni bora ndani ya uwanja kuliko hizo takataka zenu na nje ya uwanja Mata still ni best!
 
Manchester United wamefikia makubaliano na Zlatan Ibrahimovic na kuvunja mkataba. Jamaa nasikia anatimkia LA Galaxy
 
BEKI wa Manchester United, Marcos Rojo amesema si kitu alichokipokea vizuri kuhusu usajili wa Alexis Sanchez.
Si unajua Rojo na Sanchez picha huwa haziendi kabisa. Mara zote walizokutana wamekuwa wakipigana sana rafu, iwe kwenye timu zao za taifa au kwenye klabu zao Arsenal na Man United.
Lakini sasa bifu lao linapaswa kumalizika kutokana na kuwa wachezaji wa timu moja na Kocha Jose Murinho amemwambia asithubutu kumchezeana rafu mazoezini.
Kwa sasa Rojo na Sanchez watazungumza na kucheka, lakini hicho si kitu kilichowahi kutokea huko nyuma.

Rojo, ambaye amesaini kuichezea Man United hadi mwaka 2021, alisema: “Alexis ni mchezaji mahiri, lakini hatukuwahi kuwa marafiki si ndani wala nje ya uwanja. Tunapokutana kwenye mechi ni mwendo wa kuchezeana rafu tu. Zaidi ya hilo limekuwa nikimtolea lugha mbaya na yeye pia anajibu mapigo.
“Hivyo nilipogundua anajiunga na United, nilisema: ‘Oh, dah, huyu mtu anakuja hapa.’ Tulikuwa Dubai kipindi usajili wa Alexis ukikamilishwa. Nilikuwa nimeketi kimya kwenye kiti ndipo Kocha Jose Mourinho alipokuja na kunigusa kwenye beki, akiniambia: ‘Tunamsajili Alexis. Sitaki umchezee rafu mazoezini.’ Kisha akaangua kicheko.”

Wakati huo huo, Sanchez mwenyewe amefunguka na kudai mambo aliyoyatarajia wakati anatua Man United hayakwenda kama alivyopanga. Staa huyo amefunga bao moja tu katika mechi 10 alizocheza kwenye timu hiyo yenye maskani yake Old Trafford.
 
STAA Antoine Griezmann amemwambia swahiba wake Paul Pogba kuna njia moja tu ya kuwaziba midomo watu wanaokosoa uchezaji wake ambayo ni kucheza soka la kiwango cha juu.
Pogba amekuwa akishambuliwa kila kona kwa wiki za karibuni kuwa anacheza soka la kichovu ambalo haliendani na thamani ya pesa iliyolipwa na Manchester United kupata saini yake ilipomnasa kutoka Juventus kwa karibu Pauni 90 milioni.
Lakini, Griezmann amemwambia swahiba wake huyo walipokutana kwenye kambi ya Timu ya Taifa ya Ufaransa kwamba acheze mpira ndipo atakapoweza kuwathibitishia vinginevyo watu wanaomsema. Pogba ameanzishwa mara nne tu katika mechi 11 za mwisho za Man United na kumekuwa na ripoti kuwa ametibuana na Kocha Jose Mourinho.
Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps alidai Pogba hawezi kuwa na furaha kutokana na hali inayoendelea Man United, lakini Griezmann amekuwa na maoni tofauti.

Amekuja kwenye timu akiwa na tabasamu pana usoni mwake, alisema Griezmann, ambaye leo Ijumaa usiku anaweza kuwamo kwenye kikosi cha Ufaransa kitakachochuana na Colombia.
"Ameonekana kuwa na furaha. Si kitu rahisi kutocheza kwenye klabu yako na unaona kiwango kimeshuka. Iliwahi kunitokea, hivyo nafahamu vyema."
Pogba hajafunga wala kupiga pasi ya asisti kwenye kikosi cha Man United kwa mechi tisa sasa, tangu alipofanya hivyo kwenye mechi ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stoke City, Januari 15 mwaka huu.
 
Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic yuko mbioni kujiunga na miamba ya Marekani, LA Galaxy baada ya kuondoka Manchester United.

Ibrahimovic amefunga mabao 29, katika mechi 53, alizocheza Man United, ambayo amekubali kuvunja nayo mkataba kabla ya kumalizika mwisho wa msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa Sweden mwenye miaka 36, amecheza mechi saba tu tangu alipoumia mguu wake Aprili mwaka jana.

"Ni muda wa kuondoka baada ya misimu miwili ya mafanikio Manchester United," aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.

"Jambo zuri limefikia mwisho. Asante kwa klabu na mashabiki, wachezaji na makocha na viongozi wote waliokuwa pamoja name katika kutegeneza historia yangu hapa."

Ibrahimovic alijiunga na miamba hiyo ya England akitokea Paris St-German mwaka 2016.
 
Mourinho: “I understand the frustration, I understand the sadness of being knocked out in the Champions League, but I don't understand anything more than that.” [HASHTAG]#mufc[/HASHTAG] [CNN]

Mourinho: “I think really at this moment in the Premier League we have one team, one club clearly better prepared than us in the past few years to be first and we have 18 clubs behind us. One in front of us, 18 behind us.” [HASHTAG]#mufc[/HASHTAG] [CNN]

Mourinho: “In the future we want to have 19 clubs behind us but this is the reality. And the reality is for people with a brain, with sense, with common sense, with knowledge of what sports is, we are in a moment of transition.” [HASHTAG]#mufc[/HASHTAG] [CNN]

Mourinho: “Being in a moment of transition and still manage to do what he did last season and win trophies and to do what we are trying to do this season, which is still trying to win a trophy, and try to be second. I think we are in a good position.” [HASHTAG]#mufc[/HASHTAG] [CNN]
 
Tunaomfahamu Mourinho na kuielewa performance ya club tumeisha muongezea mkataba.

Wanaoponda na kubwabwaja - Mourinho Out! "tunaheshimu maoni yao, machungu wanayopitia huko mtaani tunayaelewa" lakini very soon watatembea wakikenua meno nje kama wamekatwa lips kwa furaha.
 
Back
Top Bottom