Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Acha mahaba yaliyopitiliza. Kama mtu ameshindwa ameshindwa tu...huyu hafai hapa Man U, aondoke.

Ulisema kwamba hakuna mechi ambayo Mikhi alianza, United ikashinda!! Hili ndilo lililonishangaza kwako wewe unayejiita mshabiki wa Man United. Kwani ni uongo wa mchana kweupe.

Kuhusu kufaa ama kutofaa kwa Mikhi, hili halikuwa jambo ambalo lilinifanya ni-quote post yako.

Btw, a true Man United fan never calls the team “Man U”. Jifunze historia ya timu, na uelewe kwanini ni insult kuiita timu “Man U”.
 
JESSE Lingard. Ndiyo, Jesse Lingard huyuhuyu unayemjua wewe. Ndiye, mchezaji ambaye yupo kwenye kiwango bora kabisa kuliko mastaa wote unaowafahamu wewe huko Ulaya.

Ni Lingard huyuhuyu ambaye mashabiki wa Manchester United hawamkubali sana. Lakini, ukitafuta ukweli na kama unapewa chaguo la kusajili mchezaji kwa sasa kwa kuzingatia ubora uliopo, ukiwekewa Lionel Messi na Lingard, hakuna atakayekushangaa ukimbeba Lingard. Hahahaha. Hii inahusu kiwango cha sasa cha mastaa hao wawili.

Kwenye mabao 14 ya mwisho yaliyofungwa na Manchester United, Lingard amehusika kwenye nusu ya mabao hayo, kiwango bora kabisa ambacho kinamfunika Messi hadi kuingia anga za mpinzani wake wa miaka yote kwenye soka, Cristiano Ronaldo.

Kwa kukusanya rekodi za mechi tisa zilizopita, Lingard amewaburuza mastaa wote wanaonekana kuwa bora huko Ulaya. Katika mechi hizo timu za mwisho, Lingard amefunga mabao saba na asisti mbili. Rekodi bora kabisa, ambayo hata Messi hazifikii, lakini zikimweka kwenye daraja moja na wakali kama Ronaldo, Neymar na mwenzake Kylian Mbappe. Cheki rekodi za mastaa wengine.

Jesse Lingard – mabao 7, asisti 2

Hii inaitwa usiyempenda kaja. Lingard si mchezaji anayeshabikiwa sana huko Man United, lakini ukweli utabaki palepale, ndiye mwokozi wa kikosi hicho cha Old Trafford kwa siku za karibuni. Lingard amekuwa kwenye kiwango bora kabisa, ambapo katika mechi tisa za mwisho alizocheza, amefunga mabao saba na kuasisti mengine mawili.
 
Klabu ya soka ya Manchester United wamewaongezea mikataba wachezaji wake wanne ambao mikataba yao ilikuwa inafikia ukingoni.

Wachezaji hao ambao wameongezewa mikataba hiyo ni Juan Mata, Ander Herrera, Ashley Young na Daley Blind hadi mwisho wa msimu ujao. Wachezaji hao walikuwa wanatakiwa kuondoka bure mwishoni mwa msimu huu lakini United wamewapatia mikataba ya haraka wachezaji hao na kuimarisha ya maadili yao ya uhamisho kwa kuanzisha vifungu vinavyoongeza mikataba yao kwa miezi 12 hadi Juni 2019.

Mchezaji mwengine ambaye anatajwa kutaka kuongezewa mkataba ni Luke Shaw ambaye amewavutia sana mashabiki wa United kutokana na uwezo wake katika wiki za hivi karibuni na inawezekana kupewa mpaka mwisho wa msimu kuthibitisha thamani yake kabla ya uamuzi kufanywa juu yake.

Hata hivyo Marouane Fellaini amekataa kuongeza mkataba mpya na timu hiyo ambapo mwishoni mwa msimu huu atakuwa huru na timu ya Besitkas inaongoza katika mbio za kutaka kumsajili kiungo huyo wa Ubelgiji.

Mourinho hataki kumuuza Fellaini katika dirisha la uhamisho la majira ya baridi na amejiandaa kumpoteza wakati wa majira ya joto. licha ya matatizo yake ya sasa ya kuumia. Fellaini ameanza mechi moja tu tangu mwisho wa Septemba kwa sababu ya kuumia.
 
JESSE Lingard. Ndiyo, Jesse Lingard huyuhuyu unayemjua wewe. Ndiye, mchezaji ambaye yupo kwenye kiwango bora kabisa kuliko mastaa wote unaowafahamu wewe huko Ulaya.

Ni Lingard huyuhuyu ambaye mashabiki wa Manchester United hawamkubali sana. Lakini, ukitafuta ukweli na kama unapewa chaguo la kusajili mchezaji kwa sasa kwa kuzingatia ubora uliopo, ukiwekewa Lionel Messi na Lingard, hakuna atakayekushangaa ukimbeba Lingard. Hahahaha. Hii inahusu kiwango cha sasa cha mastaa hao wawili.

Kwenye mabao 14 ya mwisho yaliyofungwa na Manchester United, Lingard amehusika kwenye nusu ya mabao hayo, kiwango bora kabisa ambacho kinamfunika Messi hadi kuingia anga za mpinzani wake wa miaka yote kwenye soka, Cristiano Ronaldo.

Kwa kukusanya rekodi za mechi tisa zilizopita, Lingard amewaburuza mastaa wote wanaonekana kuwa bora huko Ulaya. Katika mechi hizo timu za mwisho, Lingard amefunga mabao saba na asisti mbili. Rekodi bora kabisa, ambayo hata Messi hazifikii, lakini zikimweka kwenye daraja moja na wakali kama Ronaldo, Neymar na mwenzake Kylian Mbappe. Cheki rekodi za mastaa wengine.

Jesse Lingard – mabao 7, asisti 2

Hii inaitwa usiyempenda kaja. Lingard si mchezaji anayeshabikiwa sana huko Man United, lakini ukweli utabaki palepale, ndiye mwokozi wa kikosi hicho cha Old Trafford kwa siku za karibuni. Lingard amekuwa kwenye kiwango bora kabisa, ambapo katika mechi tisa za mwisho alizocheza, amefunga mabao saba na kuasisti mengine mawili.
Hahahahaha linga mess
 
Forget about that Brazilian Ross Barkley (Long shot merchant) This is how Brazilian magician leaves EPL
d22e0821dd7c60f6e2ade66df2492646.jpg
 
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameendeleza vita ya meneno dhidi ya bosi wa Chelse Antonio Conte, akikumbushia adhabu ya Muitaliano huyo 2012 kwa kupanga matokeo.
Mameneja hao wawili wameingia kwenye mgogoro siku mbili zilizopita Conte akisema kuwa Mourinho ana tabia ya "utovu wa nidhamu pembezoni mwa chaki".
Msemo huo wa Conte aliutoa akimjibu Mourinho aliyebwata kuwa baadhi ya mameneja wa Premier League wana tabia "kama kijana chizi" wakati wa mechi - kauli ambayo ilimlenga bosi wa Chelsea

Muitaliano huyo alidai kuwa Mourinho alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa mbaya wa kupoteza kumbukumbu, akitaja kwa msamiati wa Kiitaliano akimlenga bosi wa Man United.
"Nadhani anahitaji kujichunguza alivyokuwa huko hapo awali - labda alikuwa akijizungumzia alivyokuwa siku za nyuma," alisema Conte. "Labda, wakati mwingine, nadhani anasahau alichowahi kusema zamani, jambo ambalo ni tabia yake.
"Wakati mwingine nadhani analo tatizo, silijui jina, lakini demenza senile... pale unaposahau kile ulichokifanya wakati uliopita.

Baada ya Manchester United kushinda 2-0 dhidi ya Derby County kwenye mechi za Kombe la FA Ijumaa, Mourinho alifufua upya uhasama wao.
"Jambo pekee ninalotaka kusema kumaliza habari ni ndiyo, niliwahi kufanya makosa siku za nyuma kwenye mstari wa chaki," alisema Mourinho.
"Naam, nitapunguza, lakini nadhani bado nitaokesea kidogo. Jambo ambalo halijawahi kunitokea na kamwe halitatoke ni kufungiwa kwa kupanga matokeo.

Hilo halijatokea kwangu na kamwe haitatokea."
Kauli za Mourinho zinarejea adhabu ya kufungiwa mechi nne aliyopewa Conte msimu wa 2012-13 akiwa meneja wa Juventus kwa kushindwa kutoa maelezo ya kupanga matokeo akiwa akiiongoza Siena.
Conte hakuweza kufanya chochote kuzuia skendo ya kupanga matokeo 2011 Siena - na aliwajibishwa.
 
Hii vita ya maneno kati ya mourinho na conte binafsi kwa upande wangu sioni kama ina msaidia mourinho na siipendi anavyofanya ajikite ktk timu yetu
Kosa la Mourinho liko wapi?
Ye aliulizwa swali kwann siku hizi hashangilii (hana mzuka kama kipindi cha mwanzo) ye alijibu kwamba ye sio mjinga mjinga wa kuanza kuruka ruka kwenye touch line (hakumtaja mtu) sasa kale kavaa wigi bingwa wa kubeti kakajishitukia kakajifanya kumtukana jose, kalijua atakanyamazia.
 
Back
Top Bottom