Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hawa watu tunatakiwa tuwakate ili tupunguze gepu....bila hivyo mlima utaongezeka urefu.
 
Ngoja nijimwagie maji kidogo then nijisogeze kibanda umiza kusuport chama langu.
GGMU
 
Leo nina goma jipyaaaa la kupoza machungu, incase mambo yakienda alijojo
Hhaha mkuu leo mkosi tu asubuhi na mapema kimenuka kwa mchepuko..kuna bwege ananidai pesa kitambo najua kasahau leo kanikazia..nimetandika mkeka mchana arsenal kachana. Sasa na man u akipigwa ndiyo nitajua kwa nini alikiba aliimba "maumivu per day"
 
Jose Mourinho amesema mchezo mkubwa baina yake na Guardiola hautabiriki lakini Pep amedai kuwa atafuraha mechi hiyo dhidi ya mahasimu wake
Zlatan Ibrahimovic, Phil Jones na Nemanja Matic wapo tayari kwa mechi ya Man United watakapoikabili Man City kwenye mechi inayosubiriwa kwa hamu kwenye jiji la Manchester, mubashara kupitia Goal.
Timu hizo mbili zinazoongoza Ligi Kuu zitakutana katika dimba la Old Trafford - matangazo yote ya mechi hiyo yatakuwa mubashara kupitia Goal.com - timu ya Jose Mourinho inataka kupunguza pengo la pointi dhidi ya City.

Timu yake ikiwa inajiandaa kwa mtanange huo, Mreno huyo amesema mechi kubwa huwa zina changamoto ambazo hazizuiliki.
"Soka halitabiriki," Mourinho alisema. "Kama meneja, naweza kujaribu kuelezea mipango ya mchezo na kuonyesha mwelekeo wangu lakini huwezi jua nini kitatokea. Kuna mambo mengi ambayo yapo nje ya uwezo wangu ambayo yanaweza kuubadili mchezo kabisa.

Kwangu mimi, ni mechi kubwa nyingine dhidi ya timu kubwa katika nchi hii. Tumekuwa timu bora kuliko mwaka jana - Nadhani pia Man City ni bora zaidi ya msimu uliopita."
City hawajafungwa katika ligi msimu huu lakini wamepoteza mechi yao ya kwanza katika kampeni za msimu huu katikati ya wiki baada ya kufungwa 2-1 na Shakhtar Donetsk Ligi ya Mabingwa.
Ukiona Mo Anaongea Kwa Kutojisia Na Kuweka Umakin Katika Team Bass Jua Hapo Kuna Ushindi Mnono

Mara Nyingi Mo Akizungumzia Mechi Kwa Dharau Huwa Anafungwa Au Ku Draw
 
Back
Top Bottom