Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Advantage Pep!

Can Guardiola continue his winning record against Mourinho in today's Manchester derby?
24862502_10155945352098598_2318649716403071110_n.png

Hapo mechi nyingi za ile barcelona nzur ya xav,mess na iniesta


Everton na leicester city kila mmoja walishamtia salala nne achilia mbali chelsea kumpiga home and away.
 
Hapo mechi nyingi za ile barcelona nzur ya xav,mess na iniesta


Everton na leicester city kila mmoja walishamtia salala nne achilia mbali chelsea kumpiga home and away.
yaaaa alipokuja epl wamegawana kila mtu kashinda game 1 na sare 1
 
Jose Mourinho amesema mchezo mkubwa baina yake na Guardiola hautabiriki lakini Pep amedai kuwa atafuraha mechi hiyo dhidi ya mahasimu wake
Zlatan Ibrahimovic, Phil Jones na Nemanja Matic wapo tayari kwa mechi ya Man United watakapoikabili Man City kwenye mechi inayosubiriwa kwa hamu kwenye jiji la Manchester, mubashara kupitia Goal.
Timu hizo mbili zinazoongoza Ligi Kuu zitakutana katika dimba la Old Trafford - matangazo yote ya mechi hiyo yatakuwa mubashara kupitia Goal.com - timu ya Jose Mourinho inataka kupunguza pengo la pointi dhidi ya City.

Timu yake ikiwa inajiandaa kwa mtanange huo, Mreno huyo amesema mechi kubwa huwa zina changamoto ambazo hazizuiliki.
"Soka halitabiriki," Mourinho alisema. "Kama meneja, naweza kujaribu kuelezea mipango ya mchezo na kuonyesha mwelekeo wangu lakini huwezi jua nini kitatokea. Kuna mambo mengi ambayo yapo nje ya uwezo wangu ambayo yanaweza kuubadili mchezo kabisa.

Kwangu mimi, ni mechi kubwa nyingine dhidi ya timu kubwa katika nchi hii. Tumekuwa timu bora kuliko mwaka jana - Nadhani pia Man City ni bora zaidi ya msimu uliopita."
City hawajafungwa katika ligi msimu huu lakini wamepoteza mechi yao ya kwanza katika kampeni za msimu huu katikati ya wiki baada ya kufungwa 2-1 na Shakhtar Donetsk Ligi ya Mabingwa.
 
Mimi ni meneja mwenye uwezo wa kucheza mechi hizi katika hatua kubwa kama hivi. Ndio maana tupo hapa," alisema Pep Guardiola. "Nitafurahia mechi, ni wazi. Nasubiri kwa hamu kufika pale na kucheza. Napenda kucheza kwenye uwanja ule, tutafanya kila tuwezalo kuwafunga. Baada ya kushikana mikono.
"Kushinda, kusare au kufungwa, hatuendi kushinda au kupoteza Ligi ya Uingereza. Ni mechi muhimu kwa sababu tunaweza kushinda pointi, lakini ni hivyo hivyo kwao pia. Tunachowaza ni namna ya kucheza vizuri na kushinda mchezo."

Habari za Timu

Ingawa Ibrahimovic, Jones na Matic wapo kamili kwa upande wa United, kiung Marouane Fellaini atakaguliwa kwanza kuelekea mechi hiyo.
Paul Pogba anaanza kuitumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu Jumapili baada ya kadi nyekundu dhidi ya Arsenal, ataungana na Michael Carrick na beki Eric Bailly kushuhudia jukwaani.

Kiungo wa Manchester City David Silva yupo fiti kwa safari ya Old Trafford baada ya kupata majeraha madogo lakini nahodha Vincent Kompany bado yu shakani kwa mechi hii kutokana na tatizo ambalo halijawekwa bayana.
Beki wa kushoto Fabian Delph amepona maradhi yake lakini mabeki John Stones na Benjamin Mendy bado wanaendelea kuuguza majeraha.
 
Back
Top Bottom