Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Man city hawana lolote hao mechi yao dhidi ya west ham waliponea chupuchupu west ham kama wangekomaa kama jinsi walivyo komaa kwa Chelsea city wangepoteza
Kwa hizi statistics unasema Man City aliponea chupuchupu kufungwa na West Ham..!?
Screenshot_2017-12-10-14-34-07.png
Screenshot_2017-12-10-14-33-40.png
Screenshot_2017-12-10-14-33-17.png


Itakuwa ni MGONJWA wa AKILI wewe,sio bure..!
 
Tanesco matakataka sana ndy maana nafisadi wanajipigia Pesa kama watakavyo
Umeme umewaka dakika 10 zilizopita...umekatika tena! Hawa TANESCO ingekuwa amri yangu ningefutilia mbali hili shirika. Hii ni mara ya nne ndani ya masaa manne!
 
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amewataka wachezaji wake kuepuka mipira ya adhabu karibu na goli lao na kutopaki basi wakati watakapowakabili watani zao wa jadi Manchester United kwenye Uwanja wa Old Trafford leo Jumapili.

Guardiola amewaonya wachezaji wake kuacha kutengeneza mazingira ya mipira ya adhabu katika mchezo huo muhimu zaidi kwao.

Kocha huyo Mhispania, anahofia Man United inaweza kupata mabao kupitia mipira ya adhabu endapo Man City haitakuwa makini.

Man United ina wachezaji wengi warefu kulinganisha na Man City. Romelu Lukaku, Nemanja Matic, Chris Smalling na Zlatan Ibrahimovic ni wachezaji warefu ambao watakuwa tishio kwa Man City.

Kiungo wa pembeni aliyerudishwa kucheza beki wa kushoto Ashley Young amepata umaarufu kwa mashuti ya mpira wa adhabu.

Inakadiriwa kuwa watu zaidi ya bilioni moja watakuwa wakitazama pambano la Manchester United dhidi ya Manchester City.

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba ataukosa mchezo huo akitumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu baada kuonyeshwa kadi nyekundu katika pambano lililopita dhidi ya Arsenal baada ya kumkanyaga mlinzi wa kulia, Hector Bellerin na pia atazikosa mechi dhidi ya Bournemouth na West Brom.

Wengine watatu watakaokosa mechi hiyo ni mabeki watatu, John Stones na Benjamin Mendy wa Manchester City na Eric Baily wa Manchester United wote hawa ni majeruhi.
 
Chelsea jana kapoteza point 3, Arsenal leo kapoteza point 2, baadae kidogo Liverpool atapoteza point 2, Man City atapoteza point 3 na Man Utd atapata point 3

Ikifika mwezi wa 5 tutaona nani yupo juu

GGMU
Inawezekana lakini walopoteza wote walikuwa away
 
Sasa ndugu zangu mkishinda leo ni vema na haki ila mkishindwa kuutafuna huo mfupa nyumbani ni aibu sana
Nawatakia mchezo mwema
 
Back
Top Bottom