Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Nilichojifunza mechi ya leo dhidi ya Arsenal.

David De Gea kwasasa ndio kipa bora barani Ulaya sio tena EPL.

Toni Valencia anazidi kutakata licha ya umri kuendelea kusonga mbele, jamaa alistahili kitambaa cha unahodha, anaongoza kwa mfano.

Ashley Young ni kama amezaliwa upya. Kwasasa ni mtu muhimu katika safu ya ulinzi ya United.

Lingard licha ya kutokukubalika na mashabiki wengi wa United, ni mchezaji anayejua kutimiza vyema majukumu anayopewa na kocha.

Marcos Rojo awapo mzima, basi timu nayo inakuwa salama hasa kwenye mipira ya juu.

Na mwisho kabisa, Man United bado yupo kwenye mbio za Ubingwa, anakimbiza mwizi kimya kimya.

TUKUTANE Mwezi MAY!!!!
 
Baada ya mechi hii nimeamua kutoka Chelsea na kuhamia Man U kuunga mkono juhudi za Mourinho kuutafuta Ubingwa, maana kila anachofanya Mourinho ni yale yale tuliyokuwa tunayapigania huku Chelsea kwa miaka mingi, hivyo hakuna haja ya kuendelea kupingana na Man U. Narudi Nyumbani

HAHAHAHA.... the best comment of the day
 
Mkuu kama uliona gemu kabla vile......
Hakika mipira ni hesabu......
Kapewa kadi mtu muhimu sana katika timu..

Ila ile naona kama refa kakurupuka sana maana lengo la pogba lilikuwa ni mpira, naona kama aliugusa kwanza..
 
24293983_10155903973718598_4330896933173827651_n.jpg
 
Back
Top Bottom