Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

23172916_2054488204568277_6553524256027943008_n.jpg
 
Baada Ya Lukaku Kufichwa na Christensen Mashabiki Wa Manure Waliamua Kuingia Mtaa wa Jirani Na Kuita Reinforcement (Msaada) a.k.a Aguero...

23316594_2054722297878201_3735287579117011843_n.jpg
 
Kuna ndugu zetu wamechezea 3 lakini sioni wakishambuliwa kama Manchester United, hebu mtuache kidogo msipunguzie machungu yenu humu mnatujazia thread tu wakati hamna cha maana mnachoandika.
 
Pogba, Zlatan, Kurejea..!

Jose Mourinho amekaribisha mapumziko ya mechi za kimataifa na ameweka wazi wachezaji wawili wa Manchester United Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic wapo katika " nafasi nzuri "

Pogba na kiungo mwenzake Michael Carrick wamekuwa majeruhi tangu mwezi Septemba huku wachezaji majeruhi wa muda mrefu Ibrahimovic na Marcos Rojo bado hawajarejea dimbani.

Kikosi cha Mourinho kinaelekea mapumziko ya mechi za kimataifa baada ya kichapo cha 1-0 kutoka kwa Chelsea na kuwa nyuma ya pointi ya 8 dhidi ya vinara Manchester City , lakini kocha huyo ametoa taarifa chanya kuhusu wachezaji waliokuwa majeruhi.

" Tuna kundi la wachezaji ambao tuna matumaini kwamba watapona haraka iwezekanavyo."

"Lazima wafanye mazoezi kwa juhudi kila siku lakini sasa hivi wapo kwenye nafasi nzuri. Pogba, Ibrahimovic, Rojo, Fellaini."

" Wapo kwenye nafasi nzuri kwahiyo nafikiri kwamba tunaelekea katika hii sehemu ya msimu , kipindi cha Christmas na baada ya hapo tukiwa katika nafasi imara kwa maana ya kikosi."

Katika kipindi cha mwezi Desemba ambapo kuna na mechi nyingi za kucheza kocha wa United Mourinho ana matumaini kwamba wachezaji wake waliobaki ambao hawatokuwa katika mechi za kirafiki za mwezi huu watakuwa wamepata muda mzuri wa kupumzika.

" Wachezaji wengine wote wa kimataifa wameondoka na tumebakiwa na wengine wachache .. kama [Chris] Smalling na [Ander] Herrera na kiukweli wanastahili baada ya kucheza mechi nyingi wiki ya kupumzika ambayo nitawapa." Amesema Mourinho.
 
Back
Top Bottom