Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kuna vitu watu wakihoji hua wanaonekana kufatilia maisha ya mtu. Mfano wote watakaohoji mbinu za Josee katika mechi kubwa..
Mou kawa mwoga sana kwa wenzie,,

Kando na ushabiki wenzetu wapo vizuri sana,, wachezaji wana ubora wa hali ya juu na timu pia ina muunganiko

Man Utd bado haijawa na muunganiko mzuri na pia tunamkosa sana Double P... Mbali na udhaifu wa hapa na pale jamaa ni mhimu sana kwa timu yetu..
Timu bado inahitaji wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu,,

Naweka akiba ya Maneno ila kama May ubingwa wa EPL utaingia katka kabati za OT bahati itakuwa upande wetu..

Yote na yote GGMU.. Still We Have A Dream ila isije kuwa Nightmare...
 
17ab1de159f7c5037a0242b7915550e4.jpg
Mashabiki wa Chelsea na Arsenal wakikatiza kwenyw uzi wetu
Maisha haya!
Waweza kulalamika kuwa kwako panaungua kumbe pa majirani zako pameteketea kabisa. Tena yule kijana wetu Tom ndio kapigilia msumali wa mwisho penye sanduku
 
stress zinapungua niw atletico anatoa raha kuna jamaa nacheck nae game ya barca na atletico hapa anashauri miaka mitatu ikiisha tumvute Diego simeone aje OT
 
  1. Belo maneno yako yapo sahihi ya kwamba game plan ya mourinho imefanya kazi lakini suali la kujiuliza inamaana mechi zote za liverpool kwenye uwanja wa Anfield tutaendelea kucheza kwa kiwango kama hichi utafikiri timu ya Shaba ya pemba?
  2. nawakumbusha tu wapenzi wenzangu wa manchester united tutakapotembelea viwanja vya emirates na etihad tutacheza tena mpira kama huu na eti sababu kubwa ni wapinzani wetu wanamiliki sana mpira kuliko sisi na ushahidi wa hili jaribunui kurejea mechi za msimu uliopita.
  3. inamaana mechi zote tutakazocheza ugenini dhidi ya timu yenye winga wazuri mlinzi wa kushoto atakuwa matteo darmian,mwanadamu ambaye ndani ya dakika 90 anavuka mara 5 tu kwenye mstari wa kati.Kwa mchezaji aina ya darmian hata kama winga wako ni neymar basi ataonekana kilaza, nashindwa kuelewa kwa nini mourinho alishindwa kumruhusu aende juventus.
  4. jamani hawa wachezaji wetu huwa hawafanyi mazoezi ya kumiliki mpira, kwa sababu tukikutana na timu inayomiliki mpira kidogo wanapoteana uwanjani utafikiri kama wamefungwa mawe miguuni.
  5. lukaku anapaswa kuangalia video za messi apate kujifunza utulivu anapokuwa kwenye eneo la hatari, haiwezekani kila mechi awe ni yeye tu anayekosa magoli ya wazi. akiendelea na tabia hii ipo siku atamtapisha mtu.
  6. kwa mpira tuliocheza leo phil jones hapaswi kuendelea kukaa manchester united kwa sababu anacheza na vilaza, namuonea huruma sana kwa jinsi anavyojituma
  7. mwisho niwambie washabiki wa liverpool wanaopita kwenye thread hii ya kwamba kama munataka ubingwa basi munapaswa kwanza mutafute mshambuliaji, haiwezekani munaingia kwenye boksi la adui mara 20 lakini kipa wa timu pinzani anaokoa shambulizi moja tu la hatari
only city na liva ndio tutacheza kama tulivyocheza leo ila hao wengine mwanzo mwisho tutaupiga wa kutosha tu
 
..walisema kwamba hatutamiss pogba lknykweli ni kwamba tunamuhitaji sana huyu jamaa..especially kwny match kubwa kamahii ya liverpool..leo midfield ywtuilikuea imekufa kabisa yan..mipira haiendi mbele!
 
Jones dah acha tu na mimi nimeyawaza hayo je katika big 6 zote tutacheza hivi kisa tunatafuta point moja?
Sijabahatika kuiona hii game kutokana na majukumu,nilikuwa safarini afu safari ya masaa zaidi ya 14.

Lakini kwa kufatilia comments za humu na baadhi ya clip,nimeona nichangie kidogo.

Mkuu Bello na wengine,ni kweli timu ilicheza chini ya kiwango kwa macho ya mashabiki lakini ilicheza vizuri kwa macho ya walimu/wataalamu.

Target ya EPL ni kushinda taji kwa point nyingi mwishoni mwa Ligi,ili kushinda EPL unatakiwa kushinda match nyingi zaidi na kuzuia kufungwa match nyingi.

Sasa tunacheza kwa tahadhari zaidi,tunaweza kufungwa match chache mno au tusifungwe kabisa na kuwa na droo chache sana.

Ukiacha hizi timu kubwa 4 katika top 4 sioni timu nyingine ya kutusumbua kutoa droo nasi au kutufunga.

Kwanini tumecheza hivi Annfield, sababu kuu ni moja kati ya nyingi,Mwalimu alifanya kitu kinachoitwa risk analysis takers katika kushinda.

Uwezo wa timu pinzani,uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na uwezo wa kumiliki mpira wa timu zote.

Mou aliona Liver wana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira kuliko sisi katika match hii,analysis zake zimemuonesha hivyo,alichambua uwezo wa mchezaji mmoja mmoja,Liver walituzidi katika baadhi ya nafasi hasa katika eneo la kiungo.

Analysis zinaonesha Mou ni fundi katika tactics za kuzuia,huku Klop ni fundi katika kushambulia hasa katika game kubwa kama hii.

Tulikosa wachezaji muhimu wazuri waliomajrehu,yeah tuna kikosi kizuri lakini na wachezaji wanapishana katika rates uwanjani,Kwa Sasa Fellain na Pogba ni watu muhimu sana.

Sawa kwa kikosi kilichoanza,De Gea,Valencia na Matic nafikiri ndio wachezaji wenye rates za juu,jaribu kufatilia taarifa za vikosi vya mwezi vya EPL.

Harera ni mchezaji mzuri lakini bado hajarudi kwenye kiwango Chake, afu Hererra na Matic wote ni wachezaji wa aina moja ndio mana imekuwa rahisi kwa Fellain kuwa mbadala wa Pogba au kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.

Kukosekana kwao kumepelekea Mou kushindwa kutumia mfumo sahihi wa kushambulia tunapocheza na timu inayoshambulia kama Liverpool/Man City.

Ni kweli tutacheza hivi Etihad,hata mimi na support mbinu hii kutumika Etihad,Liverpool alifunguka Etihad akala mkono sijui.

Liverpool walikuwa wana nafasi kubwa ya kushinda game hii lakini wajilaumu wenyewe kwa ubutu wa washambuliaji na viungo wao.

Ingekuwa kwa Viungo na washambuliaji wa Man city nadhani tungekuwa tunaongea vingine.

Man United bado wameonesha ubora wao katika kuzuia mashambulizi,kazi kubwa kwenye match hii ilikuwa kwa Mabeki wetu,tutoe pongezi kwa beki zetu na kipa walifanya kazi nzuri sana.

Mou ameona pengo katika nafasi ya kiungo anapokosekana Pogba na Fellain,nadhani atayafanyia kazi kwa kuwatrain Matta na Mikh kuwa mbadala wanapokosekana viungo wa kumiliki mpira na kushambulia kwa wakati mmoja.

Fellain ni mzuri kwa kuzuia,kuhold mipira na kushambulia.

Pogba ni mzuri kwa Kuhold mipira na kushambulia,mara chache ameonekana akizuia.

Matic ni Mzuri kwa kuzuia na kuhold mipira ni mara chache akishambulia.

Herera wa msimu uliopita alikuwa ni Mzuri wa kuzuia,kumiliki na kushambulia tulishuhudia mashuti mengi kutoka kwake.

Herera wa msimu huu bado anahitaji match nyingi kuwa fit kufanya kazi zote hizi lakini bahati Mbaya kwenye hizi nafasi kuna Pogba,Matic na Fellain aliyejipambanua vizuri.

Tunakosa Winger aina ya CR7/De Maria,kwenye match ya leo tulihitaji mawinga wenye kasi zaidi ili kushambulia kwa kutumia Wings zetu na kumlisha mipira Lukaku,mana eneo la kati tulizibitiwa kimpira.

Liverpool walikuwa na Sarah na kiungo wa aina yake Coutihno.

Valencia hakucheza kama wings zaidi kutokana na uwepo wa Sarah.

Nadhani January Mou ataingia sokoni kununua winger zaidi ya mmoja kwa match za aina hii

Ila bado nasisitiza Mikh anatakiwa kufanya kazi ya ziada, bado hajaonyesha kiwango kinachosubiriwa,Mata umri umeshaenda sasa.

But usitegemee mpira wa aina hii tutakapocheza Old Trafford na Liverpool/Man City,labda wakosekane wachezaji muhimu.

Sioni Chelsea msimu huu wakiwa wazuri,nadhani wao ndio watakaotuzuia sisi kwenye match zote tutakazokutana nazo.

Bado nahitaji muda kuchambua mchezo wetu na totenham,totenham hawatabiriki ingawa huwa tunawafunga Acha nijiridhishe na analysis zangu nije kuandika makala kuhusu wao.

Asernal sifikirii hata kuandika makala,sijaona kipya katika kikosi chao, sio mbinu za kocha wala mchezaji mmoja mmoja,Ushauri wangu kwa Asernal ni kumfukuza Kocha wao kwa kumpa majukumu ya Mkurugenzi wa Ufundi na kumtafuta kocha Mpya.

Kwenye Match na Liverpool tulicheza sahihi kwa game plan iliyokusudiwa.

Match na liver imeshapita,tu jiandae na Benfica na zinazofuata.

Uzuri wknd hii wakubwa wote wamekufa na wao,tusubirie matokeo ya Man City.

Ibra Kadabra,Caric wapo njinai kurudi uwanjani ameanza mazoezi na kikosi cha kwanza sasa,hali kadhalika Fellain.

Hawa match za mwanzoni mwa November tutakuwa nao.

Newfame.
hakeemlucious@gmail.com
 
Back
Top Bottom