ruralofficer
JF-Expert Member
- Apr 4, 2014
- 2,499
- 3,635
August 12![]()
Tumemaliza vizuri.
Hivi EPL inaanza lini wakuu?
[HASHTAG]#GGMU[/HASHTAG]
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
August 12![]()
Tumemaliza vizuri.
Hivi EPL inaanza lini wakuu?
[HASHTAG]#GGMU[/HASHTAG]
Sent using Jamii Forums mobile app
Waoooohhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
Yaah! uhali gani bibie?cute b tunae humu ila weye ulijichimbia sana umekuwa adimu humu.afadhali wazidi kututia moyo
Yupo huko kwenye kutafuta likes.
Jamaa anaupenda ule uzi aisee,,tukamchukue..Yupo huko kwenye kutafuta likes.
Nakubaliana na Maelezo ya Mourihno,Our Pre season imekuwa nzuri kwa timu safari hii,kiasi flan tumeona uwezo wa timu,wachezaji,we'r happy kwa kweli.Mourinho On Matic Before The Game.
"Matic is a very good player, he has great knowledge of the game, my ideas and how I see football. Matic is the type of player I want in my dressing room."
Mourinho's Post Match Interview
"The club did a fantastic job in getting three of four players. I thank the club for that. I’ll be happier with four out of four.
The players have two days off now because they deserve and then we prepare.
Pre-season was good, I never get tired of repeating how well organised it was. Everything was really good, I'm happy with that.
Next week we get to the serious stuff, Super Cup & the first Premier League match.
Everybody is in the plan, the plan is to have a good squad, not a good team.
Our squad is not so big. We need everybody, it's going to be good and fun to choose the team for every match."
More From Mourinho
"When we paid the amount for Pogba I said that he was not expensive, I don't think Neymar for £200m is expensive.
The problem is not Neymar the problem is the consequence of the Neymar deal. We will see more £80m, £60m players.
What is expensive is players going for inflated fees when they don't have the quality to match."
Nishajaribu wapi amegoma labda tuendelee kumsihi arudi likes tutampa huku za kutosha kila atapotoa kommenti
Hivi anataka likes ili iweje sasa..Nishajaribu wapi amegoma labda tuendelee kumsihi arudi likes tutampa huku za kutosha kila atapotoa kommenti
Kwa kifupi sehemu kubwa ya kikosi chetu kuna mabadiliko makubwa kwa wachezaji wetu tutegemee makubwa msimu huu unaonaza tar 12Nakubaliana na Maelezo ya Mourihno,Our Pre season imekuwa nzuri kwa timu safari hii,kiasi flan tumeona uwezo wa timu,wachezaji,we'r happy kwa kweli.
Nitajaribu kuchambua wachezaji wachache kutokana na muda kwenye hii Pre season.
Tuanze na waliosajiliwa:-
1.Lukaku,kama alivyotegemewa na wengi hakutuangusha,magoli mawili akizifunga timu kubwa tu duniani,shoot on goal 3 na off goal Zaidi ya mashuti 5 katika match zisizozidi tano,tunahitaji nini Zaidi kutoka kwake.
Moto utawaka EPL ikianza,jana katika match na Sampdoria pamoja kuwa hakufunga lakini alionesha kitu katika eneo la mbele akiwa peke yake.
Maoni yangu katika Ushambuliaji,tunahitaji kusajili mshambuliaji mmoja Zaidi kutokana na mashindano tutakayoshiriki na kadri tutakavyofanya vizuri,ili kuwe na rotation nzuri kwa washambuliaji wetu.
Katika 10,Lukaku nampa 8 katika hii Pre season.
2.Leondorf,nimemuona katika match chache za hii Pre season, mwanzoni alikuwa na mapungufu kutokana na ugeni katika kikosi na kucheza katika timu yenye jina na mashabiki wengi Duniani,lakini ameendelea kuimarika kadri muda unavyoenda,Lendorf ni mzuri kwa kuzuia mipira ya Juu,tuendelee kumuamini na tutegemee mabadiliko makubwa kutoka kwake,itapendeza Zaidi kama akicheza na Baily,nampa 6 kati ya 10.
3.Matic,match yake ya jana ndio ilikuwa ya kwanza akiwa na uzi wa Man United,kama ilivyokawaida yake amepiga mpira Mwingi sana katika dimba la chini eneo la kiungo,ameonesha kitu,ameonesha uwahi mpya kwenye timu katika ya Washambuliaji,viungo washambuliaji na mabeki, sasa timu imepata holding midfield wa uhakika,hii inawapa uhuru Viungo wa Ushambuliaji kushambulia Zaidi na hata mabeki wa pembeni kupanda kusaidia kushambulia,tunahitaji nini Zaidi Zaidi ya kutuwezesha kutwaa makombe,Chelsea wametupa Zawadi tuliyostahili.
Kwa match moja tu aliyocheza nampa 8/10.
Kwa wachezaji waliopo kwa Uchache! !
1. Martial, akitoka kwenye matatizo ya kifamilia/kimahusiano,msimu mbaya wa mwaka jana,Martial ameonesha mabadiliko makubwa katika hii Pre season na akiendelea hivi hamna haja ya kusajili winger,assist mbili na tamu za magoli,Dribble za uhakika,uwezo wa kuwakata mabeki Zaidi ya wanne kwa kujiamini tena katika match na timu kubwa kama Man City,Madrid,Barcelona.
Sina shaka na Martial kinachohitajika kwa sasa ni kuamini wa tu na Kocha na kupewa majukumu kamili ya winger moja tupate raha kutoka Katika kipaji hichi,kwangu nampa 8/10.
2. Rashford,Patners hip anayojabu kuitengeneza Mou ni ya utatu pale mbele,Rashford,Lukaku na Mikhityran,nimeshamuelezea Lukaku,kwa kifupi,Rashford ameendelea kuonyesha uwezo wake katika eneo la Ushambuliaji,katika hii Pre season naweza sema amejihakikisha kuwa mshambuliaji wa pili baada ya Lukaku,mabadiliko makubwa katika umilikaji wa mpira,uwezo wa kufunga na pasi za uhakika zinanifanya nimpe 8/10 huyu mtoto kutoka pale Mfenesini Zanzibar.
3. Mikhityran, bado kuna kitu nasubiri kukiona kutoka kwa huyu Fundi wa mpira,naona bado ana vingi Zaidi ya hivi anavyotuonesha,uwezo wa kufunga,kupanga mashambulizi na kumiliki mpira humfanya Mou kutojutia kumsajili,huyu jamaa ni Fundi haswaa huwa namfananisha na Hazard,tutegemee makubwa Zaidi kutoka kwake,kuna kipindi huwa najiuliza kwa nini Mou hana mpango wa kusajili mshambuliaji mwingine?jibu ni kwa sababu ya uwepo wa Mikhityran,Mikh ana uwezo wa kucheza namba zote katika eneo la Ushambuliaji,7,8,9,10 na 11.
Kwa sasa anasogea kutoka eneo la kiungo mshambuliaji na kwenda eneo la Ushambuliaji kamili akiwa sasa na Rashford na Lukaku,tumeona akicheza hivi katika hii Pre season.
Kwangu nampatia 9/10.
Stay tuned sehemu ya pili..tukianza na eneo la Viungo. (Pogba,Pereira,Matta na Herera)
Sent Using Sumsung S6 Edge