Top 4 ngumu wakuu, njia pekee ya kurudi UCL ni kushinda Europa League.
nakumbuka baada ya kufungwa na chelsea kwenye Carling cup nilizungumza maneno kama yako wewe kama ni vigumu kwetu sisi kupata nafasi ya nne na tunapaswa tupiganie zaidi EUROPA na nikajaribu kutoa sababu zangu kutokana na mechi zinazotukabili kwenye ligi na EUROPA na nikajaribu kukumbushia changamoto tulizo kumbana nazo tulipokabiliana na wapinzani wetu kwenye mechi za mwanzo, nakumbuka member mmoja anaitwa
Inartia yeye pekee ndiye alikubaliana na mawazo yangu ila nashukuru kadri mechi zinavyochezwa na wengine mumeanza kuona ukweli halisi wa timu yetu.
bado tuna mechi mbili pungufu ya wapinzani wetu wakuu wa kihistoria liverpool na wametupita kwa points 6 ila nikiangalia ratiba ya mechi zetu zilizobakia nabaki njia panda kuhusiana na nafasi ya nne. kama tunataka nafasi ya nne nilazima timu hizi zifuatazo tuzifunge
chelsea - nyumbani (hatujawafunga misimu 3)
tottenham - ugenini (tuliwafunga nyumbani)
man city - ugenini (walitufunga nyumbani)
arsenal - ugenini (mechi ya kwanza suluhu nyumbani)
burnley - ugenini (mechi ya kwanza tulitoka suluhu nyumbani)
sunderland - ugenini (tuna rekodi mbaya uwanja wao)
everton - nyumbani (mechi ya kwanza suluhu na tunacheza nao Jumanne)
je kwa style yetu ya kushambulia wachezaji 4 tu ndani ya box tutaweza kushinda mechi hizi zote?
hivi tokea aondoke SAF tushawahi kuifunga timu pinzani mabao 5.