Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

51d58cbbf1576cdcd2da3db1b48d91be.jpg
a24493ca9001c53ab554a48041d2ab72.jpg
 
Sikupata tabu wakati wanamponda mou,Pogba na ibra nilijua it's just a matter of time well done Lads


To be Honest Ni Kweli Ibrahimovic Katuprove Wrong!!! Lakini Uongeleeni Mpira Kisport Zaidi Musiongelee Kisiasa!!!
Mwanasiasa Akishakuwa Madarakani Hata Akiharibu Basi Chama Chake Kitamsifu na Kukataa Kuboronga Kwake!! Lakini Mpira Hauko Hivyo! Mchezaji Akiboronga Hata Hike 2nd Half Katika Mechi Moja tu Basi Anapaswa Kuongelewa Performance Yake...

Ni ukweli Usiofichika Kuwa Takriban Mechi 10 za Awali Za EPL (Toa 3 za Mwanzo) Ibrahimovich alikuwa Flopi Na Useless! Sasa Kwanini Asijadiliwe Kipindi Kile???
Hivi Hujui Kuwa Hata Neymar Jr sasahivi Yupo Katika Diffficult Time na Tayari Watu Wanaanza Kuquestion Kiwango Chake???
Hiyo Ndiyo Soka Mkuu...

Sasahivi Ni Kweli Ibra Katuprove Wrong Kwa Kurudi Katika Form, So no need to question his performance....
 
Watu ni wa ajabu sana mkuu, kuna timu zinafanya hovyo, kuna talents nyingi zinapotea huko nje, lakini as long as sio sehemu ya manchester basi hawana shida nazo, kitu kidgo tu kikitokea manchester basi ni stori ya dunia.

Waliongea sana oooh mata lazima auzwe cha ajabu soon mata ataongeza mkataba miaka minne, alipokuja Zlatan oooh mzee so far ana goli 12 goli moja nyuma ya costa, yaani kila kitu mou atakacho kifanya basi ni tatzo, sasa wanataka Rashford amuweke benchi Zlatan, yaani zlatan awe anamuangalia Rashford anachofanya uwanjan then nae ndio aje afanye hivo HAHAHAAAA. Hawa watu wanatofauti gani na moyes aliyesema akina vidic na rio waangalie cd za jagielka ili wajifunze kitu

Dah, umenikumbusha kitu kilichonifanya nifute matumaini yangu kwa Moyes, nilikuwa namkubali sana na nilihisi atatufikisha mbali, ila alipoongea hiyo kitu basi tena.
 
Sikumaanisha Hivyo Mkuu!! Namaanisha Kuwa Mourinho Anaendeleza Falsafa Yake Ya Kuwapoteza Vijana Hasa Pale Ninapomuangalia Very Talented Boy Anthony Martial na Depay Wanapopoteza Ndoto Zao...
Manake Mchezaji Kipaji Aliyekuwa Na Ndoto Za Kucheza One of the Top Club in Europe Halafu Akaishia Everton ni Ridiculous.....
Ndiyo Mana Nikasema Rashford Naye Huyo....
Acheni unafik, nafasi si walipewa wakazingua? Wamerejeshwa wazee timu inafanya vyema, utd si kituo cha kulea yatima, wakitaka namba wapige kazi, wakizingua tutawapanga hata kama ni vizee vinavotembelea mkongojo mradi watimize wajibu wao na timu ishinde, au unataka wapangwe vijana waharibu ili muje kufanya fujo na dhihaka? Mutasubiri sana
 
karibu ingawa nakuona kama mpya uku.
Asante kwa ukaribisho, japo pia si mpya, sema huwa sichangii sana, ila huwa nasoma tu. Na ukaribisho kwenye jukwaa hili, nilifanyiwa mwaka 2011 kama sijasahau.
 
Back
Top Bottom