Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

15193683_10154241501167746_6059149217118964749_n.jpg
 
picha za vikos zibadilishwe hapo juu za zaman sana

Hapana,

Zibaki hivyohivyo, zinatukumbusha kule tulikotoka. Tunaishi kwa historia, Mwaka wa nne huu unaenda bila SAF, na bado hatujapata kikombe cha EPL.

Tukiangalia picha hizo, Makombe, Vikosi Mameneja nk, Vinatupa mzuka na kutamani kule tulikotoka kiasi cha kupigania Mafanikio yale ya hapo awali.. na kwapamoja kwaimani Yatarudi.

Msingi unaanza kujengwa taratibu pale OT hii ni mechi ya nane tunacheza pale bila kufungwa home. ninahakika kipindi cha mafanikio kinakuja na hakiko mbali..

GGMU GGMU GGMU GGMU
 
Moja ya usajili ambao unasuburiwa kwa hamu na mashabiki wa Manchester united ni wa mchezaji Antoine Griezmann akitokea Atletico Madrid. Rais wa Atletico amesema hivi karibuni kwamba mchezaji wake hana mpango wa kwenda kokote zaidi ya kubaki hapo hapo kwenye club yake ya sasa.
Sasa connection na ushawishi wa club ya Manchester united unaendelea kuonekana hadi kwenye level za familia ya Griezmann. Antoine amekua bila wakala kwa muda sasa akiwa anategemea ushauri wa familia yake kudanya maamuzi yake ya kisoka.
Sasa kaka yake ameonyesha kwamba yeye ni shabiki mkubwa wa Manchester united hasa Wayne Rooney. Mapenzi hayo ameonyesha wakati Manchester wanacheza mechi dhidi ya Feyenoord. Theo Griezmann mtu wa karibu kabisa na Antoine alikua ana tweet live wakati mechi inaendelea akionekana kum-pusha Wayne Rooney aendelee kusukuma gozi uwanjani.
Moja ya tweet zake aliandika, “Come onnn!!!! ROONEY” . Kwenye tweet nyingine pia adhihirisha yeye ni shabiki wa Manchester kwa kuandika ,”Let’s go man united”.
Baada ya tweet hizi jamaa ameanza kuwa maarufu huku mashabiki wa Manchester united wakimjibu tweet zake na kumwambia namba 7 ya Manchester united inamsubiri mdogo wake. Kwasababu Antoine anategemea ushauri wa karibu wa familia yake kwenye mambo yake ya soka. Inategemewa kwamba ushawishi wa kaka yake unaweza kuchangia star huyu kujiunga na kikosi cha O.T.
To be honest, sioni haja ya Antoine kuja OT. Nafikiri United haihitaji mchezaji kama yeye; mbona wapo wengi OT?
 
mourinho ataacha timu yenye nguvu sana naona sasa wameanza kumuelewa na falsafa yake old traford unaanza kuwa uwanja mgumu sana sifa ya mou hiyo



kweli anamuaanda mik
Nitamlaumu fergusona mpaka kesho kwanini aliiacha Man U mbovu kiasi kile mpaka kufikia makocha kutolewa kafara
 
Wakati anastaafu alichukua ubingwa na hiyo timu unayoiita mbovu
Tena angekuchukua miaka miwili mfululizo kabla ya kutuacha tatizo likatokea game ya Everton tunaongoza 4-2 jamaa wakachomoa ndio kilitokea tukakosa ubingwa moyes karithi timu ikiwa bingwa.
 
Wakati anastaafu alichukua ubingwa na hiyo timu unayoiita mbovu
Ni mbinu na ujanja tu ndio vilimfanya achukue ubingwa lakin timu tayari ilishajifia we kutoka 4-2 mpaka 4-4 tena tunaenda pigwa bao la 5 refa anamaliza mechi kutuzibia aibu kubwa iliyokua inakuja.....
 
Back
Top Bottom