Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hii mechi ya leo inaleta mashaka, wadachi wamepokea pesa kwa mpira waliocheza. Walikuwa wanawapa mipira Man United wafunge na Feyenoord walikuwa wanatembea uwanjani badala ya kukimbia na kukimbiza mpira.

Mou na Man United naona wameamua kuwapatia Feyenoord 20% ya mapato ya T-shirt.
Naona simba ishakuharibu
 
Naona simba ishakuharibu
Sio Simba. Ni gongo ndugu. Si unaelewa viwanda vya gongo salama vinajengwa kwa mwendokasi?

Wewe kama umeitizama hii mechi kwa macho matupu bila miwani au miwani ya 3D huwezi kuelewa nilichokieleza. Endelea tu kunywa gongo lako, ukiamka namba inakusubiri uisome.
 
1480027487427.jpg


Herrera alikuwa sahihi,

Iceman umechanganya record ya European na Epl. Hongera kwako mkubwa Rooney si kazi ya kitoto kufikia record hii
 
Sio Simba. Ni gongo ndugu. Si unaelewa viwanda vya gongo salama vinajengwa kwa mwendokasi?

Wewe kama umeitizama hii mechi kwa macho matupu bila miwani au miwani ya 3D huwezi kuelewa nilichokieleza. Endelea tu kunywa gongo lako, ukiamka namba inakusubiri uisome.
Kwahiyo na Arsenal nao juzi walipewa hela, maana kiwango chao kilikuwa chini
 
Mikhitaryan anaanza kuonyesha confidence yake..jamaa atatusaidia Sana !
 
mourinho ataacha timu yenye nguvu sana naona sasa wameanza kumuelewa na falsafa yake old traford unaanza kuwa uwanja mgumu sana sifa ya mou hiyo



kweli anamuaanda mik
 
Moja ya usajili ambao unasuburiwa kwa hamu na mashabiki wa Manchester united ni wa mchezaji Antoine Griezmann akitokea Atletico Madrid. Rais wa Atletico amesema hivi karibuni kwamba mchezaji wake hana mpango wa kwenda kokote zaidi ya kubaki hapo hapo kwenye club yake ya sasa.
Sasa connection na ushawishi wa club ya Manchester united unaendelea kuonekana hadi kwenye level za familia ya Griezmann. Antoine amekua bila wakala kwa muda sasa akiwa anategemea ushauri wa familia yake kudanya maamuzi yake ya kisoka.
Sasa kaka yake ameonyesha kwamba yeye ni shabiki mkubwa wa Manchester united hasa Wayne Rooney. Mapenzi hayo ameonyesha wakati Manchester wanacheza mechi dhidi ya Feyenoord. Theo Griezmann mtu wa karibu kabisa na Antoine alikua ana tweet live wakati mechi inaendelea akionekana kum-pusha Wayne Rooney aendelee kusukuma gozi uwanjani.
Moja ya tweet zake aliandika, “Come onnn!!!! ROONEY” . Kwenye tweet nyingine pia adhihirisha yeye ni shabiki wa Manchester kwa kuandika ,”Let’s go man united”.
Baada ya tweet hizi jamaa ameanza kuwa maarufu huku mashabiki wa Manchester united wakimjibu tweet zake na kumwambia namba 7 ya Manchester united inamsubiri mdogo wake. Kwasababu Antoine anategemea ushauri wa karibu wa familia yake kwenye mambo yake ya soka. Inategemewa kwamba ushawishi wa kaka yake unaweza kuchangia star huyu kujiunga na kikosi cha O.T.
 
Kidogokidogo tutafika, wanasema "hata roma haikujengwa kwa siku moja"
 
Back
Top Bottom