Acha kabisa dadangu,
Yaani kwasasa ulichonacho unakilinda kwa gharama yoyote kisije kukuponyoka..!! Huoni hata babu Wenger pamoja na ubahiri wake akilalamika kuwa Wachezaji wake Mastaa wanapaswa kuongezewa mishahara ili waendelee kudumu pale Gunners..!!!??
Anajua mziki wake, Alichokipata kwa Fabregas, Framin, Helb, Song na Nasri hataki kimrudie tena. Na vile mashabiki wake wanaubao wa miaka kumi na kitu ndo anazidi kuchanganikiwa.
Soka la leo bila pesa haliendi..!! Upenzi wa timu uliondokaga na kina, Roy Keen, Cantona, Avrin, Bergcamp, Patrick Viera Stive Gerad, Carragher na wengineo, leo ni pesa mbele...!!
Hivi umewahi kufikiri maishani mwako kuwa Wenger atatoa Paun 42 kununua kiungo mmoja tu.... Narudia, Kiungo siyo Mshambuliaji...!!!!