Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,183
- 37,487
So far so bad, two matches to go man u tumefunga magoli 44 kati ya mechi 36 tulizocheza hadi sasa, ( amazing) goli tisa tu mbele ya Norwich anaekomaa kutoshuka daraja, msimu wa 2011/12 tulifunga magoli 89 inamaana msimu huu tumefunga nusu,
Toka nimeanza kuipenda Manchester nakumbuka msimu wa 2004/05 ndio msimu ambao tulikua na goli chache sana goli 58, japokua history inaonesha msimu wa 1989/90 tulikua na goli 46 tulimaliza wa 13, mwaka 1988/89 goli 45 tulimaliza wa 11, msimu uliopita tulikua na goli 62.
Game saba tumecheza nyumbani bila goli ( Newcastle, shittty, west ham, Chelsea, soton, PSV, Middles borough)
Game sita za away bila goli ( arsenal, palace, stoke, WBA, spurs, looserfool) jumla utaona tumecheza mechi 13 bila kupata goli lolote, huku tukiwa na namba ndogo sana ya shoot on target ( Ngongo huu ndio mpira wa kushambulia, attacking football unayoitaka?)
Tunaongoza kuwa na clean sheets nyingi kwenye ile top eight si kwa sababu tunadefence nzuri bali ni sababu ya uwepo wa de gea langoni,
AU hii inakuaje? Tunagoli chache na clean sheets nyingi au hii sio defensive football?
Kuna sehemu nilikua nacheki ni timu moja tu toka serie A, EPL na la liga ambayo ilimaliza ndani ya top six ikiwa na goli chini ya 50 ( Villarreal msimu uliopita) ndani ya miaka mitano iliyopita.
Toka primier league ikaanza timu zilizomaliza ndani ya top six na goli pungufu ya 50 ni
Betis '95,
Arsenal '96
Aston Villa '97
West Ham na Mallorca 99
Aston Villa na Alavés '00
Betis in '02, Celta Vigo in '03
Aston Villa, Sampdoria na Palermo '04
Everton, Bolton, Livorno* na Sevilla '05
Celta Vigo na Osasuna 06
Villareal '07
Racing Santander '08
Sampdoria '10
Villareal '15
Sasa ukiangalia kwenye orodha hiyo ukiachana na arsenal ya Bruce, hizi timu zingine zote ni average timu ambazo zilikamua above their weight, and that is the level we've dropped to.
Still watu wanamkataa mou kwamba hana attacking football, is this an attacking football tunayoitaka?
Ngongo
Mkuu herrera kwanza ni lazima ufahamu kipa ni sehemu ya wachezaji so David de Gea ni mchezaji wa Man Utd.Pili unatakiwa ukubali mchango wa Van Gaal wa kumbakiza de Gea kikosi wakati Real walipokuwa wanamyemelea kwa kasi ya ajabu.Pili fahamu ni Van aliyecheza karata ya kumsignisha mkataba mrefu ambao kama Real watamtaka itabidi wavunje kibubu.
So far Man imebakiza mechi mbili ambazo tukishinda zote tuna uhakika na nafasi ya nne (it's within our reach) na usisahau FA Cup tuna nafasi kubwa pia.
Nakubaliana na wewe msimu huu tumefunga goli chahche sana,lakini tunasahau msimu uliopita mashabiki wengi walikuwa wakipiga kelele Rooney aongoze safu ya ushambuliaji bahati mbaya kiwango chake msimu huu kilitetereka sana na pai kuumia hilo si kosa la kocha bali hiyo ni sehemu ya mpira wakati mwingine unawaza hivi matokeo yanakuwa tofauti.
Tukubaliane majeruhi wengi walichangia timu kutetereka sana,bahati mbaya hilo halisemwi sana hasa na vyombo vya habari vya UK ambao ajenda yao kubwa ilikuwa ni ku attack mikakati yote ya Van Gaal.Mfano vyombo vingi vya habari vya UK vimekuwa mstari wa mbele kumponda Van Gaal katumia 250 million lakini havisemi kauza wachezaji wangapi ?.Ni kwanini hawasemi 250 less wachezaji aliwauza na wengine waliondolewa kwenye payroll ?Fedha kiasi gani zilipatika kwa mauzo ya Di Maria,Fletcher,Chicharito,Rafael,Nani,Kagawa,Evans,Welbeck & Cleverley.
Mashabiki wa Mourinho wanasahau mafanikio yote aliyopata Chelsea yalitengenezwa na Ranieri ambaye kaonyesha kipaji cha hali ya juu kwa kuchukua ubingwa kwa bajeti ndogo sana.Nauliza Mourinho alipokuwa Spain alitawala ligi ya kule alichukua vikombe mara ngapi ?.
