Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Tunaelekea kuanza msimu wa 2015/16;
-Hatuna CB wa kueleweka na mustakabali wa DeGea haujajulikana. Sidhani kama huu msimu ni mtu wa kutumainiwa sana, ingefaa angeondoka tujue moja.
-Ndo msimu wa LVG ku-deliver, wana wa united hawatavumilia makosa ya kizembe. Hasa maswala ya kujaribu mifumo, ameshakaa vya kutosha. Akivurunda nadhani Ed Woodward hata mvumilia.
-Ndo msimu unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa United hasa baada ya kurudi kwenye Champions League. Wanataka kuona team yao inafanya vyema kwenye UCL.
 
MAN UNITED-NAMBA ZA KILA MCHEZAJI:
1 . De Gea
4 . Jones
5 . Marcos Rojo
6 . Evans
7 . Memphis
8 . Mata
10 . Rooney
11 . Januzaj
12 . Smalling
13 . Lindegaard
14 . Chicharito
16 . Carrick
17 . Blind
18 . Young
19 . Wilson
20 . Sergio Romero
21 . Ander Herrera
23 . Shaw
25 . Valencia
27 . Fellaini
28 . Schneiderlin
31 . Schweinsteiger
33 . McNair
35 . Lingard
36 . Darmian
42 . Blackett
44 . Pereira
50 . Johnstone.
 
Huyu mkaburu msimu huu atuambii kitu, akuna cha philosophy wala philokhadija timu ikizungua atembee maana ndio visingizio vyake, kama atoleta beki wa kati inamaana anaona waliopo wanatosha, na timu msimu huu imebalance vizuri kuliko msimu uliopita na ameshaspend pesa mingi tu na tunawachezaji wa kushindana katika makombe yote ya ndani, yote ya yote hope tutakuwa na msimu mzuri kuliko hii 2 iliyopita #GGMU
 
Ameni na yeye atokomelee France msimu ujao kama alivyofanya Dada Maria

Hivi unakuja kwenye Page za watu unaanza kurusha matusi bila hata kutukanwa, Zinakutosha kweli Wewe? Kwanini usitulie ukachambua mpira kama wewe ni Mchambuzi wa soka? Kama huwezi si utulie tu uwe msomaji. Kinachokucheketua ni nini sasa wewe!!

BACK TANGANYIKA
 
Pepo linaloikumba Jezi namba 7 lishindwe na lilegee na kutokomea kabisa,kwa Depay likae naye mbali kabisa,wote tuseme Amen......

Ukitaka kuangalia sana, Baada ya Ronaldo kuicha jezi hiyo, wengi waliokuwa wakipewa ni Wachezaji ambao walionekana tayari ni maarufu kuanzia kwa Owen, Valensia mpaka hivi majuzi kwa De Maria.

Wachezaji, Mashabiki na Timu nzima ya Man U walijenga matuamini makubwa kwa wachezaji hao kutokana na umaarufu wao na namba ya jezi waliyokabidhiwa. Matokeo yake tunaona ni wachezaji hao kucheza Underpreassure kutokana na matumaini makubwa kwa Mashabiki na Wachezaji wenzao waliyojitwisha.

Hii ni tofauti kidogo na jinsi Alivyokabidhiwa Ronaldo jezi hiyo toka kwa Beckham, maana Ron alikuwa hafahamiki kwa yeyote, Mashabiki wakamuona Feggie chizi kwa kumkabidhi jezi maarufu mchezaji asiyefahamika na ambaye kiwango chake hakijulikani. Achia mbali umri wake mdogo..!!

Kwa muktadha huo, Ukiangalia kiwango cha Depay na namna alivyotua ndani ya Team na jinsi alivyoaminiwa haraka haraka na Wachezaji wenzake, Bechi la Ufundi na Mashabiki kwa ujumla, Namuona Dogo akienda kutoboa chini ya jezi hii. Hii kwanza ni kutokana na waliovaa jezi hii tangu kwa Ron, hakuna aliyeperfom kiasi cha kumbebesha yeye matumaini makubwa kama waliokuwanao Mashabiki kwa wachezaji waliopita wakivaa jezi hii. Hapa ninahakika Dogo anaenda KUTOBOA... tusubiri.

Nikija kwa sala yako, let me say Amen.

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom