Matatizo ya nyumbu nayaweka katika sehemu kuu tatu
1. Nyumba mpo wazi sana, hii inafanya muda wote kipa anakua kwenye pressure kubwa.
Beki watatu wabovu hata huyo mmoja martinez nae ataoneka mbovu pia
2. Kiungo kinakatika sana, hasa kwenye switch positions, unaweza ukawakuta wote wapo upande mmoja. Ikitokea team pinzani inapiga pass ndefu ya kuamisha uwanja viungo wanaanza kukimbiza upepo na ndipo wapinzani wanakutana na aya ya 1. Mashambuliz kama hayo yakipigwa matatu basi 1 lazima liwe goli
3. Washambuliaji wenu ni butu. Ndio ni butu. Sio jambo la kujivunia mfungaji bora wenu aje kuwa bruno tena wakati sesko, cunha, mbeumo, raashford wapo
Nini kifanyike
Overall restructure, fumua kikosi chote. Hapo itahitajika sio chini ya misimu mitatu. Laiti mngeanza mwaka juzi leo tungekua tunaongea lugha moja na arsenal
Kwanza mjenge timu ya kuleta ushindani, hiyo team ikikaa vizuri mnakazia sasa kuwa na timu ya kuchukua makombe
Profile kama maino, yoro, santos, heaven, zirkzee ndio iwe priority yenu. Wanapata msaada watu kama bruno, martinez, raashford, cunha
Wafuatao hawakustaili kuwa Manchester united, hasa ukizingatia ukubwa wenu
Maguire
Shaw
Dalot
Mount
Mazroui
Mbeumo
Casimiro