Kama shabiki wa Man united wa miaka zaidi ya 20 ambaye nilishuhudi nyakati nzuri za mafanikio ya Man united chini ya Sir Alex Ferguson na CEO David Gill, nawasiwasi nyakati zile nzuri zinaweza zisirudi hivi karibuni. Baada ya kufanya tathmini juu ya uelekeo wa hii Man united chini ya INEOS matumaini yangu yameshuka sana hivyo nimejiandaa kwa miaka kadhaa ya maumivu.
Zifuatazo ni sababu (red flags) zifuatazo zinafanya nipoteze matumaini na uongozi wa INEOS
1. FAILURES YA INEOS KWENYE CLUB NYINGINE
Kabla ya Man united, INEOS wamekuwa wakimiliki club mbili za mpira wa miguu ambazo ni OGC Nice ya ufaransa na FC Lausanne-Sports ya Uswisi. Katika club zote hizi wamefeli vibaya. OGC Nice imenusurika kushuka daraja msimu uliopita kwa kumalizi nafasi ya 16 kati ya 18 na Lausanne Sports imewahi kushuka daraja chini ya uongozi wa Ineos na mpaka sasa bado ina struggle. Haya yote ni matokeo ya maamuzi mbalimbali mabovu ya Ineos kwenye usajili wa wachezaji, uteuzi wa makocha na overal poor management. Sitaki kuwa mjinga kuamini kuwa hawa hawa Ineos ambao wamekuwa wakifanya maamuzi mabovu kwenye club hizo ndio watafanya maamuzi mazuri kwenye club kubwa na yenye presha kubwa kama Man united. Mashabiki wanaosema "trust Ineos" are just too naive.
2. WALIVYO SHUGHULIKA NA SWALA LA KOCHA TEN HAG
Wakati msimu wa 2023/2024 ukielekea tamani ilikuwa wazi kuwa jahazi la Man united limemshinda Ten Hag. Man united walitolewa hatua ya makundi kwenye UEFA kwa kushika nafasi ya mwisho yani walizidiwa point kwenye group na club za Galatasaray na Copenhagen na walimaliza ligi wakiwa nafasi 8 kwa kupata points 60 ambazo ni lowest tangu msimu wa 1989/1990.
Kitu pekee postive msimu ule ilikuwa ni ushindi wa FA cup. Licha ya kushinda FA cup wengi walitarajia Ten Hag kufukuzwa sababu ukiacha kushinda FA overal hali ya timu ilikuwa mbaya sana lakini cha kushangaza Ineos walimwongezea mkataba. Uamuzi wa komwongezea mkataba Ten Hag ulikuja kuwa proven wrong sababu msimu unaofuata perfomance ya timu ilikuwa mbaya zaidi kiasi cha kufanya Ten hag kufukuzwa miezi minne tu baadae akiacha Man united ikiwa nafasi ya 14 kwenye ligi. Hii ni ishara kuonyesha kuwa maamuzi ya Ineos sio ya kuamini.
3. KUMPA KAZI RUBEN AMORIM
Simaanishi kuwa Rumen Amorim ni kocha mbovu sana lakini kumpa kazi ya kuifundisha Man united ilikuwa uamuzi mbaya. Udhaifu mkubwa wa Amorim ni kutegemea kwa asilimia 100 mfumo mmoja tu wa back 3, tena ni wa 3-4-3 tu, inamaana hujui mfumo mwingine tofauti na huo. Hata kocha kama Antonio Conte ambaye wakati mwingine anaonekana kama Chief architect wa mfumo wa back 3 huwa anbadirisha mfumo mara kadhaa kutokana na hali ya mechi na wachezaji alionao kama alivyofanya kwenye misimu yake miwili ya mwisho Napoli.
Hii ilifanya Liverpool ambao walitangulia kuwa interested naye waghairi wazo la kumwajiri awe mrithi wa Klop. Sababu ili aweze kufanikiwa atawalazimisha mnunue wachezaji wengi wapya na kubadilisha kabisa structure ya timu na apewe miaka ya kutosha kuweza kubadirisha structure ya timu na kujenga upya kitu ambacho ni kigumu kwa timu hizi kubwa zenye presha. Tatizo ni kuwa akishindwa kufanikiwa mtalazimika muanze tena kujenga upya timu from zero na kuirudisha upya kwenye structure yake iliyozoeleka.
Ineos wakijua wazi kuwa Man united haina wachezaji wa mfumo wa 3-4-3 na mfumo huo ni kinyume na tradition na Identity ya Man united, wakamuajiri Amorim. Matokeo yake ni kuwa na msimu ambaya zaidi tangu miaka mingi kupita na Amorim kuwa na lowest winning rate kuliko makocha wote wa Man united katika era ya EPL.
4. TIMING YA KUMFUKUZA AMORIM
Sina shida na Amorim kufukuzwa, mwenyeye nilitaka afukuzwe mapema sana sababu kwanza alionekana kuelemewa na ugumu wa kazi ya Man united (hakuwa metally matured enough kwa kazi yenye presha kama Man united) ndio maana mara nyingi alionekana kuwa mtu ambaye yuko nervous kwenye touchline kitu ambacho hakikuwa kuzuri kwa wachezaji. Just imagine mpo vitani harafu mnamwona kamanda wenu ambaye ndio anatakiwa kuwapa tactic za ushindi anatemeka. Pili mfumo wa back 3 mara nyingi ni kwa team zenye underdog mentality, mara chache sana utaona timu kubwa yenye kutawala soka la ulaya na kutawala uwanjani inatumia mfumo wa back 3 hivyo wazo kuwa Man united itakuwa permanently back 3 team made me sick.
Wakati matokeo ni mabovu sana kila mtu akitegemea Amorim kufukuzwa Sir Jim mmilliki wa Ineos alitokea kwenye media na kutangaza kuwa Amorim hatafukuzwa bali atapewa miaka miwili zaidi ila wakaja kumfukuza miezi miachache baadae sio kwa sababu ya matokeo mabaya bali kwa sababu aliwakosoa kwa kuhindwa kumsajilia wachezaji ambao wanafaa kwa mfumo wake wa back 3 kipindi cha dirisha la January. Hii imesababisha kuleta mgawanyiko mkubwa kwa mashabiki wa Man united, naombea mgawanyiko huo usiwepo kwa wachezaji.
5. USAJILI WA WACHEZAJI
Kuna watu wanasifia Ineos kwa kusajili wachezaji kwa bei ndogo, ni kweli wanasajili kwa bei ndogo ila wana sajili wachezaji average ambao hawaji kuongeza ubora wa timu na lengo lao ni kupunguza matumizi ya club ili mwisho wa mwaka waje kupata gawio kubwa. Baadhi wana argu kuwa mbona zamani tulikuwa tunasajili wachezaji wa gharama lakini timu haikufanya vizuri. Jibu ni kuwa kipindi kile chini ya Ed woodward hatukua na mkurugenzi wa michezo wa mkurugenzi wa usajili wenye uwezo hivyo tulikuwa tunasajili wachezaji wa gharama kwa kufuata trend za mitandao bila kufanya ananlysis kama wanafaa kwa timu. Kusajili wachezaji kwa gharama haimaanishi kuwa ndio watafeli, mchezaji kama anafaa na ni bora hatutakiwi kukwepa kutumia gharama. Man city imekuwa ikitumia pesa kusajili wachezaji wazuri na wanaofaa ndio maana wametawala soko la uingeleza kwa miaka kumi sasa.
Wachezaji walio sajiliwa na Ineos katika msimu wao wa kwanza ni Ugarte (mbovu), De ligt (reject wa Bayern na injury prone), Mazraoui ( sio mbaya ila ni average squad player na reject wa Bayers), Zirkzee (mbaya), Yoro ( bado apewe muda). hawa wote ukitoa Yoro walisajiliwa kwa kuwa walikuwa wanapatikana kwa bei ndogo. Msimu uliopita tumesajili Mbeumo, Cunha na Sesko ambao wameonyesha kuwa bora na wameleta mabadiliko kwenye timu toka kuwa moja ya timu iliyofunga magoli machache zaidi (44) msimu wa 2024/2025 hadi kuwa moja wapo ya timu zilizofunga magoli mengi zaidi (69) msimu wa 2025/2026. Mafanikio haya yaliletwa na matumizi ya pesa kwenye usajili na sio kwa kutafuta cheap option kwani hao wote walisajiliwa kwa zaidi ya 60m kila mmoja.
Usajili wa msimu huu unavyoenda unanifanya niamini kuwa ule wa msimu jana haukuwa kwa matakwa ya Ineos bali ulifanyika sababu Amorim alikuwa anawakazia wamletee wachezaji wenye ubora anao taka. Msimu huu sababu hawana kocha ambao anawa presha kwenye kusajili ndio maana wanasajili average players wa bei chee. Sitaki kuwa mjinga niamini moja kwa moja kuwa Andree Santos ambaye alikuwa hapati namba Chelsea iliyokuwa na hali mbaya msimu ulio pita ndio aje aongeze ubora kwenye kikosi chetu kama walivyofaya wakina Cunha mpaka pale atakapokuja ku perfom kinyume na matarajia, ambayo ni sawa na ku bet.
6. KOCHA MICHAEL CARRICK
Sitaki kumuhukumu moja kwa moja Michael Carrick kuwa sio kocha mzuri ila bado hajafanya ya kutosha kwenye game kuonyesha kuwa yeye ni kocha bora anaeweza kuipaisha Man united. Watu wata point alivyo iwezesha Man united iliyokuwa ina struggle chini ya Amorim kumaliza nafasi ya tatu lakini hiyo haitoshi. Alichofanya Man united hakina tofauti na Middlesbrough. Alichukua MIddlesbrogh ikiwa nafasi ya 21 na kuipandisha mpaka ikamaliza ligi ya Championship ikiwa nafasi ya 4.
Msimu uliofuata akaanza kushuka ambapo msimu wa pili timu ilimaliza nafasi ya 8 na msimu wa tatu nafasi ya 10 na akafukuzwa kazi. Wataalamu wanasema kilicho muangusha Carrick ni kutegemea mbinu moja ya ku shambulia kwa transantion na counter attack na kokosa mbinu za kudungua defense ya timu ambayo inakaa nyuma. Hivyo baada ya timu cha Championship kumjulia walikuwa kila wakicheza na Middlesbrough hawafunguki, wanakaa nyuma hivyo kufanya Carrick kupotea. Hiki nakiona kikitokea msimu huu kama Carrick hajabadirika.
Msimu uliopita Man united ilikuwa inacheza kama underdog kwenye mechi nyingi hivyo timu zilikuwa zinafunguka na kuwaruhusu Man united pata space za kutosha kushambulia ila msimu huu timu nyingi zitakuwa zinaiheshimu Man united hivyo hazitakuwa zinaipa space Man united kama msimu jana.
C&P
mtechnical