Ile sababu kwamba tunasajili wachezaji wanaoipenda timu pamoja na kuangalia thamani halisi ya soko inaonekana ni utapeli mtupu. Huyu dogo katoka Leicester kaenda Villa lakini sikuona interest toka klabu nyingine kubwa zaidi ya Utd leo hii baada ya kukosa targets zake.
We are officially a mid table team kama usajili wa Tielemans toka Villa unatufurahisha hivi.
fuentte unachosema ni sawa Tielemans, hana jina kubwa lakini sio sababu ya kusema, sio mchezaji mzuri. Kisa hakuna timu nyingine zilizotaka kumchukua, lakini ujue pia hizi sajili za sasa, zimekua pia za kipuuzi sana. Wachezaji wanauzwa kwa pesa kubwa sana, ambayo haiendani kabisa na uwezo wao(akiflop na kushindwa kudelivery hii hasara club mnaibeba wenyewe).Hili suala limetusumbua sana, hasa kipindi cha Ed Woodward. Pia sajili ni kamali, united imekosa target zake muhimu kulingana na falsafa mbalimbali wanazotumia ineos kama:
1:mchezaji kuwa na mapenzi kwa united
2:mchezaji kukubali mshahara isiyo mikubwa
3:mchezaji kuwa na msimamo wa kuja united. N.k
Kosa walilofanya ineos, ni kwenye target yao muhimu, ambayo ilikua ni mateus Fernandes. Kumbuka huyu kashuka daraja na club mbili, Southampton na westham. Hapa united walikua sawa kabisa, kukataa kutoa £85m na mshahara wa £250k kwa wiki. Lakini walichonikela sana, ni kuendelea kumfukuzia mchezaji huyu mda mrefu. wakati ukiacha mateus, kutokua na msimamo thabiti, wa kuja united pia haku meet falsafa wanazotumia ineos kusajili mchezaji. Real Madrid, iliwahi pia kumtaka Mateus Fernandes, chini ya meneja wao mpya Jose Mourinho.
Nafikiria sababu iliyowafanya wao kumpotezea, waliona mateus Fernandes hana thamani hiyo, wanayoitaka westham. Ndiyo tukabakia sisi pekee yetu, kwenye race. Akatokea Tottenham spurs, ambae almanusura nae ashuke daraja. Akatoa hiyo pesa na huo mshahara na hii ni panick buy waliokua wanaitaka westham. Kuhusu elliot Anderson yeye aliweka wazi kwenda Manchester city. Hivyo sioni kosa la united kutemana nae mapema sana. kuhusu Aurelian tchouamen alikua target ya muhimu sana ya united na ineos walikua tayari kutoa £77m hadi £80m. Lakini Madrid wakaamua kumbakisha bila kusahau tchouamen bado alikua na mapenzi ya kubakia Madrid napia asingekubali kushusha mshara kilahisi licha ya kuwa na miaka 26. Hivyo bado mie naona united wako sawa hofu niliyonayo ni kwa huyu andrey Santos maana Chelsea huwa wanatupiga sana.