Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ni dhahiri huyu tunampata na nirasmi sasa utd inaenda kuwa timu ya ushindani kwan shida kubwa ya utd ukiacha zile ndogo ndogo kama za kiungo na gosl keeper, ni kupachika magoli. Tumekuwa hatufungi magoli licha ya nafasi nyingi tunazotengeneza. Sasa usajili wa wakati huu utaleta magoli na assist za kutosha.
 
Flop Hilo hamna kitu hapo mchezaji anamuogopa Kai ni mchezaji huyo😂😂😂
 
Sesko ana jina kubwa?
 
GK si huyo tunamtaka kwa mkopo...golikipa wa kimataifa unamtaka kwa mkopo ..haya...striker si ndio huyo sesko tunajivuta kama wenye mabusha Hadi Newcastle wameshatuma ofa na inaelekea kukubaliwa ...
 
GK si huyo tunamtaka kwa mkopo...golikipa wa kimataifa unamtaka kwa mkopo ..haya...striker si ndio huyo sesko tunajivuta kama wenye mabusha Hadi Newcastle wameshatuma ofa na inaelekea kukubaliwa ...
Sizani kama sesko ataenda Newcastle, kumbuka makubaliano na club. Ni tofauti kwenye kukubaliwa na mchezaji. Mwenye presha kubwa sana na mchezaji(sesko) ni Newcastle sababu ya Isak anayetaka kuondoka hivyo Newcastle wanataka striker kwa hali yoyote kabla EPL league haijaanza.

According to Fabrizio romano, ni kwamba Newcastle wamekataa ofa ya pound million 120, iliyopelekwa na Liverpool ili kumchukua isak. Kwahyo hapa utaona hata Liverpool pia wanaomba sesko aende Newcastle hii itasaidia wao kumpata isak. Tukirudi kwa man united ni kutokana na sera yake mpya ya usajili inayotaka mchezaji kuipenda club na hii amelisema hata Flano maana tumeona kwa mbeumo pia alivyowakataa Tottenham.

Ndio maana Manchester united, kupitia kwa director Christopher vivel ambaye alishafanya kazi na leipzig, wanafanya contact na mchezaji sesko pamoja na agent wake. kuhusu malengo ya club n.k na sesko amekubali kuchezea man united hata kama hatupo UEFA champions league. Lakini pia wameshafanya contact na leipzig na wako tayari pia kutoa pesa kwa leipzig. Lakini ambacho hawataki man united ni kuingia kwenye mtego wa Newcastle na leipzig kwa kutoa pesa kubwa kwa sesko.
Ndio maana wanamsubiria sesko ambaye amesema mda c mrefu atamake decisions baada ya kuongea na familia yake kuhusu future yake na club ipi ataenda kuchezea kati ya Newcastle na Manchester united.
 
Dah mlolongo wote huu aise tunapitia magumu kweli kweli 😀🍺 Sasa familia ikisema nenda Newcastle itakuaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…