Mbeky
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 672
- 520
Hilo la United kuchukua ubingwa last season kwa gap kubwa limeshaongelewa na kutolewa maelezo sana humu...
Pia huwezi kufananisha hali ya United na timu yoyote yenye kocha mpya, for Christ sake. United ilikuwa chini ya SAF kwa miaka takribani 27! Unaelewa maana ya timu kuwa chini ya kocha mmoja kwa miaka 27?!? Ina maana philosophy ya timu ilikuwa shaped na huyo mtu! Anapoingia mtu mwingine, siyo kazi rahisi ati!
Mimi naona DM kajitahidi sana: msimu wake wa kwanza, kaipeleka timu 1/4 ya UCL! Kuna makocha wamehaha misimu kibao kujaribu kufika hatua hiyo, lakini hola!! Fainali ya Capital One Cup; na kushinda Community Shield. It is a good start; let's see what he can offer in his second season. With new players, he can't have any excuses!
Hilo la Martinez kuwa bora leo, ni ajabu! Huyu si ndiye kocha aliyeishusha daraja Wigan ama? Leo anakuwa bora? Martinez ashukuru aliachiwa timu nzuri na DM! DM kaachiwa ageing squad, with midfield problems na SAF.
Mwaka jana uliona Rogers alivyochemsha na timu, almanusura kufukuzwa? Angalia sasa hivi anapigania ubingwa!! Rogers hajawahi kushinda ubingwa wowote! Lakini leo anaonekana ni kocha bora EPL!!
Mimi bado naamini katika kumpa msimu ujao tena DM...huku akileta wachezaji wapya kadhaa. Kisha hapo ndipo nitakapoanza kumshambulia akivurunda.
Wewe na mimi tutabaki kulaumu, ila waamuzi wa mwisho ni bodi ya United. Kama bado wana imani na DM, utapoteza nguvu zako bure.
Tumpe msimu ujao, kisha tumjudge kwa kitakachotokea.
hilo swali la Mbeki niliamua nisimjibu kwa sababu wala tusingeelwana. man utd misimu mitatu iiliopita timu inakwenda kwa uzoefu wa Sir Alex ila wachezaji mmoja mmoja wengi ni past their best. ukitoa rooney na van persie sijui mchezaji gani wa man utd anaweza kupata namba first eleven ya man city,chelsea hata liverpool i doubt.
sasa timu hii inayokwenda kwa amri za kijeshi za Sir Alex unampa kocha mpya unategemea ichukue ubingwa??? hata mimi sikutegemea wawe namba saba ila hii ndio reality check timu sio nzuri,jumba bovu limemuangukia Moyes
Suala la midfielders linajulikana tangu enzi za Sir Alex timu haina midfielders wazuri,na kumaliza ligi tukiwa mabingwa kwa point 11 inaweza kuwa down to other teams ku-underperform na sio kuwa sisi ni wakali kivile,Liverpool last season hawakuwa wazuri hivi,hata Chelsea hawakuwa kama season hii na man city wamekomaa kuliko last season.
Sikatai ni vigumu sana kwa kocha kuchukua timu mpya na kuipa ubingwa msimu huo huo ingawa wapo wawezao kufanya hivyo...lakini siamini kama hiyo ni excuse ya mchezo mbovu tulionesha msimu huu..sio excuse ya Moyes kukosa first eleven msimu mzima..pia hiyo excuse iliyomfanya Moyes ashindwe sajiri kipindi cha summer ningemuelewa kama tungeshindwa tetea ubingwa tu lakini sio kustruggle nafasi ya saba huko na hata basi let's say ligi ni ngumu tungependa kuona Manchester inacheza mchezo mzuri nafikiri Moyes akuletwa Man U aishushe timu to zero kwanza ili baadae ndio aanze kuipandisha nachoamini aliletwa aendeleze pale alipoishia SAF kwa namna yake mwenyewe..
Si muhukumu Moyes kwa kutochukua EPL msimu huu namuhukumu kwa namna Manchester inavyocheza namna anavyoset up game plan ya kila mechi namna anavyopanga kikosi namna anavyofanya substitution pale inapoitajika namna anavyowatumia wachezaji kadri ya uwezo wao..wachezaji wamepoteza hali na morali...
Can we stand confidently and say Moyes ameongeza kitu katika timu kiufundi...
Seriously hata mimi nilimuamini Moyes kabisa ila sa hivi namuangalia katika angel nyingine naona NO Something is wrong here..
Mkuu Inzi hapo ntakukatalia Man U aliyoikuta Moyes si sawa na Liverpool aliyoikuta Rogers..
Wasiwasi wangu yasije yakatukuta kama yale ya Liverpool kwa Roy Hudson au ya arsenal maana wanashindwa kuelewa tatizo ni timu au ni kocha kutopata vikombe..napata shaka na ya mbeleni chini ya Moyes
Last edited by a moderator: