Habari za siku nyingi ndugu zangu, naomba nitoe muono wangu kuelekea msimu unao kuja kwa upande wetu.
Kwa mtazamo wangu naona tunaenda kuanza msimu huu tukiwa bado sio timu tishio kwenye ligi, na hii ni kutokana na ukweli kwamba timu yetu bado ni dhaifu kulinganisha na wapinzani wetu wakubwa kwenye ligi, mfano, kwa maana ya Man City na Arsenal, huku Liverpool ni ngumu kumsemea. Na pia aina ya usajili unaonyesha kwa kiasi kikubwa ni wa malengo ya muda mrefu.
Kwa malengo halisia nadhani kama tukimaliza msimu ndani ya top four na bonus ya kikombe kingine kidogo kwangu itakuwa ni fair kabisa. Ikitokea zaid ya hapo basi ni Bonus tu.
Kwa upande wa usajili kwa msimu huu nitafurahi zaiidi kama tutasajili DM mmoja wa maana. Hapo kwa mtazamo wangu tutakuwa tayari kuanza msimu mpya. Najua inaweza kuwa ni process ndefu kupata ile cream lakini binafsi naona kuna dalili njema kwa kuangalia sajili zilizo fanyika. Ila tuna kazi nzito ya kupunguza watu wasio faa pia.
PIli nadhani tuna shida kubwa either kwenye timu ya madaktari, ili tuweze kusogea tunahitaji wachezaji wawe fiti kwa muda mwingi. Pamoja na kuwa na timu dhaifu ila Kwa namna moja ama nyingine majeruhi mengi yametufelisha zaidi kwa msimu jana. Kama ni watu wa kujifunza basi naamini uongozi pamoja na medical team wemeliona hilo na watalifanyia kazi.( Kama sababu zipo ndani ya uwezo wa binadamu)
Binafsi naona msimu huu unaweza kuwa ni mzuri kuliko misimu miwili iliyo pita. Na ninaamini tunaweza kuanza kutengeneza identity yetu. Ila kikubwa tusiwe na matarajio makubwa ili tuweze ku enjoy,
GGM