Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

AWB yupo katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba, kwa uongozi ulio makini utapaswa kuchukua hatua ya kumuuza au kumuongezea mkataba mpya ili kuepusha kuondoka akiwa huru mwaka unaofuata.

Man utd wanaelekea kuchagua njia ya kwanza ambayo hata mimi naiunga mkono.
Je United tutaathirika kwa kuondoka kwake, Kiupande wangu sioni athari kubwa sana.
Nimekuwa mpinzani wa AWB tokea siku aliosajiliwa.

Kuhusu Mazroui sina cha kuzungumza, kwa miaka ya karibuni nimepunguza kwa kiwango kikubwa sana kufuatilia timu nyenginezo pindi zinapocheza hivyo simfahamu sana.

Wengi wao wanalalamikia takwimu zake za majeruhi.

Nitafurahi siku moja kama itavunjwa hii laana ya kutokuuziana wachezaji kati ya Man Utd na Liverpool.
Navutiwa na uchezaji wa TAA.

Sahihi Kabisa AWB ni Muda mwafaka kumwachia na Wengine wote ambao Mikataba inaelekea ukingoni akiwamo Maguire, McTominay, Lindelof, Ericksen, Pellistri na Hannibal,

Liverpool
na UTD Kuuziana wachezaji ni ngumu sana kuja isha, Sakata la Mwisho lilikuwaga la Gabriel Heinze. TAA ni RB aliyeibadilisha Nafasi kuwa sanaa kama Busquets na nafasi ya DM. TAA kuna Uwezekano mkubwa atakuja ishia R.Madrid.

Kuibuka kwa YORO na NEVES Kulinifanya angalia Game za LILLE na BENFICA. Kuna RB Kadhaa walinivutia sana Vanderson na Tiago Santos, walipokutana Monaco na Lille, Halafu Benfica Kuna ALEXANDER BAH.

Soko la sasa limejaa Wachezaji wengi ni Suala la Kujua Project yako inataka nini.
 
Mazroui anakupa option zote mbili, nafikiri ndio maana wanamgombania
Mzroui hawezi kutupa hizo option maana atakuwa kitandani akiuguza majeraha. Na defensively hawezi kufikia uwezo wa Bissaka.

Morocco national team anawekwa benchi na Yahya Attiyat Allah upande wa kushoto na kulia anawekwa benchi na Hakimi.

Kama mchezaji anawekwa benchi na mchezaji anayecheza Wydad tu huko EPL ataweza ?
 
Hii saa 12 as uh Man U iko live
Screenshot_20240801_062012_Chrome.jpg

Kuna mida sisi tukiwa tunaendelea na majukum leo wao watakuwa vitandani.
Screenshot_20240801_062517_Chrome.jpg

Bets ni noma
 
Yoro nje wiki 12
Rasmus nje wiki 6

Kwa Upande wangu Hizi Taarifa za Majeraha ni kama Nimependa Muda Zimejitokeza.

Pre-Season, Mwaka Jana Mainoo aliumia kwa Mechi aina hizi, Mbadala akaletwa Mwishoni tena kwa Mkopo Amrabat! INEOS Imeweka Uongozi kwa kufikia sasa Unajitahidi.

UTD inamhitaji sana De Ligt Sababu ndo kwanza ana Miaka 24, Ameanza ng'aa tangu ana miaka 17! Uzoefu wa timu ya Kumiliki Mpira {Ajax}, Kuzuia {Juventus} na Kushambulia {Bayern} Kifupi amekomaa. Atakuwa ni Kiongozi mzuri sana kwa YORO ili asiingie kwenye timu na Pressure. Haya Majeraha yanatoa taswira inabidi uwe na Kikosi kipana chenye Ubora.
 
Nakubaliana na hoja yako mkuu.
 
Tunaibomoa nyumbu kutokea kwa nyuma,

daktari mkuu wa nyumbu katokea arsenal ata mwezi haujafika tangu aanze kazi
Injuries: Yoro, hojlund, rashford
IMG-20240802-WA0001.jpg
 
Katika injuries zote 4, inayoniuma zaidi ni ya Hojlund tu, wengine naona imetokea wakati sahihi ili kutokufanya mambo kwa mazoea alikokuwa nako Erik. Ninaamini Yoro tutapata mbadala kabla dirisha halijafungwa. Ila Rashy na Anthony wapumzike kwa amani kwa sasa kwanza.
 
AMAD anamuaibisha ERIK
Sure, nilisema hapa kipindi cha nyuma makosa makubwa sana kwa Erik ten Hag msimu uliopita hakutumia silaha mbili kuanzia raundi ya 2 yaani Sofyan na Amad.

Erik amekuja kushtuka mwishoni kabisa na hata sasa hivi INEOS wasifanye makosa ya kiufundi tunamhitaji sana Sofyan Amrabat bila kujalisha Ugarte anakuja au lah. Tuna DM mmoja tu mpaka sasa Casemiro na yeye hadhaminiki muda wowote anaweza Kula umeme au pancha.
 
Mzroui hawezi kutupa hizo option maana atakuwa kitandani akiuguza majeraha. Na defensively hawezi kufikia uwezo wa Bissaka.

Morocco national team anawekwa benchi na Yahya Attiyat Allah upande wa kushoto na kulia anawekwa benchi na Hakimi.

Kama mchezaji anawekwa benchi na mchezaji anayecheza Wydad tu huko EPL ataweza ?
Fanya uchunguzi wako vizuri kuhusu national team ya Morocco. Noussair Mazraoui ni kama alivyo Matthijs de Ligt weakness zao kubwa they're susceptible to injuries ila wakiwa fit ni wachezaji wazuri sana.
 
Noussair Mazraoui, Matthitjs de Ligt & Sofyan Amrabat. Hapa at least timu itakuwa ime-balance. Ujio wa Sofyan inabidi uwe separately from original plan bila kujali kitakachotokea kwa Ugarte.
Sofyan Amrabat huyu huyu ambae msimu uliopita alikuwa mzito sana na anapoteza mipira kirahisi?
 
Kama kuna kosa kubwa sana la kiufundi tutafanya ni kuanza msimu rasmi tarehe 16 dhidi ya Fulham tukiwa na kiungo mmoja tu wa chini (Casemiro). Ugarte au Sofyan lazima mmoja awepo kikosini au wote.
 
Back
Top Bottom