Managing Director - TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Managing Director - TANESCO

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Mchaga, Sep 18, 2009.

 1. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wakuu nafasi ya Managing Director Tanesco imetangazwa ipo katika majira na mwananchi ya leo Ijumaa 18.09.2009.

  Wenye uwezo jitokezeni mlitumikie shirika na mlete mabadiliko, ni nafasi nzuri ya kuonyesha unachoweza kufanya ndani ya shirika la TANESCO.

  Nawatakia watakaomba kila la kheri.
   
 2. w

  wasp JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanangu pale TANESCO kuna fitna/majungu sana. Nadhani Dr. Rashid ameona kufanya kazi pale kunatosha bora angalie ustaarabu mwingine.
   
 3. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,471
  Likes Received: 1,420
  Trophy Points: 280
  ila MD TANESCO si huwa anateuliwa na mh. rais sasa huu utaratibu wa watu kuomba kazi umeanza lini
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  kwa sasa nafasi kama hizoo zinatangazwa waombaji wanajitokeza na baada ya usaili majina matatu yanapelekwa kwa mkuluu kwa uteuziii...

  mara nyingi ni changa la machoo tuu kwani mteulee lazimaa mkuluu amkubaliiii na sio vyinginevyoooo
   
 5. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  May be wanajaribu kupata new people with different kind f exposure...

  Recently Tanesco imekuwa ikitangaza sana nafasi za kazi I'm not sure kama watu wanajiondoa au kampuni inakuwa, ila ya MD imekuwa ni mpya kwangu!

  Wenye uwezo wajaribu na wakipata wafanye mabadiliko shirika likue...
   
 6. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ni kweli huwa inafanyika vetting kwa watu watatu then mkuu anachagua jina moja, lakini kwa taratibu kazi kama hizo kwa sasa lazima itangazwe sidhani kama kuna changa la macho...
   
 7. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kweli mkuu wenye uwezo wajaribu wafanye mabadiliko na si kuendelea kulalamika katika vijiwe NAFASI NDIO HIYO CHANGAMKIA...
   
 8. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Lakini tangazo lenyewe mbona limekaa ndivyo sivyo? linasema muombaji awe na digrii ya uhandisi AU utawala,hii imekaaje wadau,yaani inayumkinika umwambie mwombaji awe na digrii ya udaktari au sheria kwa kazi hiyo hiyo moja? inakuja kweli au iko namna ili xyz atengenezewe ulaji hata kama hana sifa? kwa nini wasiseme tu kwamba mwombazi awe na digrii ya uhandisi na shahada ya uzamili ya utawala (MBA au Msc Management)?
   
 9. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Najua kwa kawaida wanasema ni siri kati ya Muajiri na muajiriwa lakini roughly, mshahara wa MD wa Tanesco unaweza kuwa shilingi ngapi?? Nisije nikaacha kwenye 'majani mabichi' nilipo sasa nikaenda kwenye 'majani yaliyokauka'???
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  MD kama 10m hivi kwa mwezi....safari za kumwagana.....allowance kibao ten precent usisemee....
   
 11. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Katika magazeti ya jana jioni Badra Masoud ambaye ni afisa uhusiano na habari wa Tanesco amesema hatambui hilo tangazo limetoka wapi na kuyatahadharisha magazeti yaliyotoa tangazo kuwa wasitegemee malipo kutoka tanesco.
   
 12. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kichekesho kweli! Matangazo wameyatoa kny magazeti mengi sana mbona....mi niliona kny The Guardian pia......nani alipeleka huko? Huyu naye anajichanganya kweli!
   
 13. 911

  911 Platinum Member

  #13
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Gazeti la Majira linaripoti hivi:

  TANGAZO la kazi kwa nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), lililotolewa kwenye baadhi ya magazetijana, limezua utata mkubwa huku kila upande ukidai kutolitambua.

  Utata huo uliibuka baada ya Menejimenti ya TANESCO kueleza kushtushwa na tangazo lililotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo.

  Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Ofisa Uhusiano wa TANESCO, Bi. Badra Masoud, alisema ofisi yake haina taarifa zozote za kuwepo tangazo linalohitaji mtu mwenye sifa za kuwa mkurugenzi wa shirika hilo. Nafasi hiyo kwa sasa inashikiliwa na Dkt. Idrisa Rashid.

  "Matangazo yote yanayotolewa na shirika hili hupitia ofisini kwangu kabla ya kutolewa magazetini, nasikitika kusema kuwa tangazohilo silitambui na sasa nipo Bagamoyo kwenye mkutano," alisema.
  Bi. Badra aliongeza kuwa ofisi yake haitahusika na gharama za tangazo hilo magazeti.

  Haijafahamika kwamba tangazo kwa hilo linatokana na kumalizika mkataba wa ajira kwa nafasi hiyo au ni kusitishwa kwa sababu za kiutendaji.

  Naye Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Aloyce Tesha alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema TANESCO ni shirika la umma linaloendeshwa na Bodi, hivyo jukumu la kutangaza nafasi ni la Bodi si serikali.

  "Serikali huandaa sera na kanuni kwa ajili ya mashirika ya umma lakini haihusiki katika kuendesha mashirika hayo, Mwenyekiti wa Bodi wa shirika hilo ndiye mwenye mamlaka ya kutoa tangazo hilo,"alisema.

  Aliongeza kuwa wizara yake haitahusika na gharama zozote za tangazo hilo wala uwajibikaji wowote kwakuwa, limetolewa na Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO na si wao.

  "Tangazo lingekuwa ni letu mngeona tumeweka saini yetu sisi na ndio maana mnaona amesaini Mjumbe wa Bodi ya TANESCO kwa hiyo waondiyo wenye majibu yote kuhusiana na nafasi hiyo kutangazwa,"alisema Bw. Tesha.

  Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bw. Peter Ngumbulu kwa njia ya simu ili kujiridhisha juu yauhalali wa tangazo hilo, lakini jitihada hizo hazikufanikiwa.


  Habari hii imeandaliwa na Christina Gauluhanga, Elisante Kitulo, Benjamin Masese na Makumba Mwemezi.
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kazi kweli kweli huyo Badra yupo yupo tu hapo hajui hata majukumu yake da kichekesho kweli kweli.
   
 15. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Inasemekana tangazo limetolewa na Board of Directors ya Tanesco.
   
 16. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180

  Rashid hakuondoka kwa ridhaa yake bali contract yake inakwisha mwezi ujao na isingeweza kuwa renewed kwasababu atapandishwa kizimbani hivi karibuni kujibu mashtaka juu ya madudu aliyofanya akiwa BOT na hapo Tanesco!!
   
 17. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #17
  Sep 21, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) is a company incorporated under the Companies Act, Cap 212 and is wholly owned by the Government of the United Republic of Tanzania.

  Its Head Office is located at Umeme Park Building, Ubungo Dar es Salaam. It is a vertically integrated utility company and is responsible for generation, transmission, distribution and marketing of electricity in mainland Tanzania and Zanzibar.

  TANESCO's vision is to add value and make the company commercially and financially viable in order to expand electrification in the country, especially in the rural areas.

  In light of this, TANESCO would like to recruit a dynamic, experienced and qualified individual to fill the position of Managing Director to effectively and professionally manage the utility.

  Vacancy: Managing Director

  Job Summary

  The Managing Director is the Chief Executive Officer (CEO) of the company and is responsible for providing effective leadership to TANESCO with the aim of achieving short and long term sector and company objectives.

  He shall be responsible for good governance, strategic direction and guidance of the business of the company.

  He/she will report to the Board of Directors and will be accountable for the achievement of productivity, budgetary and profitability targets through cost effective measures.

  Key Responsibilities

  1. To formulate strategies and oversee implementation for the generation, transmission and distribution of electricity on mainland Tanzania and Zanzibar;
  2. To prepare company operational reports, financial statements, corporate plans and budgets and submit to the Board for information and/or approval as the case may be.
  3. To prepare and submit significant litigation decisions and settlements to Board for information and/or approval.
  4. To provide link with the government and the donor community through the ministry responsible for the energy sector, the Treasury, and other state organs.
  5. To advise the Board on the appointments of and changes in the . Company's team of top executives.
  6. To constantly improve organizational structures and processes to generate higher productivity and revenues to the company.
  7. To manage business risks and build a strong corporate image;
  8. To manage all company resources and promote a strong corporate image; and
  9. To promote manpower development and capacity building while also providing a motivating work environment to staff, characterized by low turnover and high morale.
  10. To promote the good image of TANESCO etc.

  Qualifications, Skills and Knowledge

  • The ideal candidate for this position should possess:
  • A Bachelor's Degree in Engineering (Electrical) or Management. A postgraduate qualification in a relevant technical or business related field will be an added advantage;
  • A minimum of 15 years working experience, five of which should be in a Senior Management position, preferably in the energy sector;
  • Excellent organisational, communication and interpersonal skills and the ability to interact professionally with diverse groups of people;
  • Knowledge of Tanzania's power industry business environment and a good track record in change management;
  • Proven ability in networking, developing cohesive business partnerships, negotiating and effectively sustaining relationships with Governments/International bodies and major business customers; and
  • Strategic and analytical skills coupled with a high level of ethics, integrity and transparency.

  General Terms and Condition of Service for the post

  • Successful candidates will be appointed on a three years contract period (after successful probation) which may be renewable.
  • Competitive remuneration and other benefits as they may be approved by the Board from time to time.
  • All officers of the Company are required to comply with the Company's and Public Service Code of Conduct.
  • Other terms and conditions of service are as per the Company Staff Benefit package and as will be reviewed and promulgated from time to time.

  Mode of Application

  Applications enclosing certified copies of relevant certificates and awards, two recent coloured passport size photographs and curriculum vitae (CV) should reach the undersigned not later than 2nd October 2009.

  The CV should include names, addresses, contact telephone numbers and email addresses of three academic and work related referees.

  The title of the position applied for should be marked on the envelope.

  Applications for this position are open for Tanzanians only.

  Application letters must be submitted to:

  The Chairman, Board of Directors
  TANESCO
  C/O Company Secretary
  P.O. Box 9024
  Dar Es Salaam, Tanzania

  Fax: + 255(22)2452026

  E-mail: subira.wandiba @ tanesco.co.tz

  +++++++++++++++++++++++++

  Apply people!
   
 18. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Tangazo na qualifications poa. Je hawajaweka mtu wao tayari na hii sio formality tu?
  Mashirika mengine wanapewa kishkaji tu , mara Raisi kamteua fulani kuwa mkurugenzi shirika fulani .......na bla bla kibao.

  Wakuu wa mashirika wanapaswa waombe kazi wafanyiwe interview na due diligence kabla ya kupewa ofisi. Waliopewa kishkaji ndio hao wameyaua yote. Kodemet
   
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  THis time waone aibu jamani maana usiwepo uswahiba na kubebana kama alivyo bebwa IR....hakuwemo hata kwenye last 10 applicants from no where akawa yeye mdio MD uswahiba wake na JK.....this time no...no iwe haki na ukweli
   
 20. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  haya tumelalamika sana humu ndani kwamba kuna watu wanaweza hizi kazi!! tutume cv sasa!!
   
Loading...