Mabadiliko TANESCO yachochee ufanisi wa Shirika, ubora wa huduma na uhakika wa umeme

Sep 13, 2023
35
46
Mabadiliko ya wakurugenzi katika mashirika kadhaa ya umma, ikiwa ni pamoja na shirika la umeme Tanzania, Tanesco yakachochee ufanisi, ubora na uhakika wa huduma za umeme nchini.

Awali, mishale ya lawama za kukatikatika kwa umeme nchini zilielekezwa kwa waziri wa nishati wa wakati huo ambae hivi sasa amehamishiwa wizara nyingine na akaletwa mwingine ambae pia ni Naibu Waziri Mkuu.

Baada ya waziri kuondolewa, mishale ya lawama ikabaki kwa mkurungenzi mkuu wa Tanesco ambae nae vilevile leo hii kahamishwa kwenye shirika jingine la umma na akaletwa mkurugenzi mpya.

Hivyo basi ni matumaini ya watanzania nchini kuwa, waziri mpya wa Nishati na mkurugenzi mkuu mpya wa Tanesco wanakwenda kubadilisha taswira ya Tanesco iliyochafuka machoni mwa waTanzania kuwa, shirika hilo linaendeshwa na watu wasio na uwezo, wala ujuzi wa masuala ya nishati bali siasa na propaganda.

Mabadiliko haya pia, ni ishara kua Rais wa Tanzania anafuatilia kwa karibu sana utendaji wa wateule wake katika maeneo mbalimbali, lakini pia anasikiliza malalamiko ya watanzania kwa njia mbalimbali na hivyo ni vizuri kuendelea tena kawa bidii bila kukoma wala kukata tamaa kuwasilisha malalamiko, ghadhabu na ushauri kwa serikali, kwani yanasikilizwa na yanafanyiwa kazi na Rais na wasaidizi wake.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom