Mamlaka za Jiji la Dar zitafute ufumbuzi wa tatizo la ardhi ya mazishi ya ndugu wanaotutoka

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
31,908
33,342
Nimeshiriki mazishi kadhaa katika sehemu mbalimbali za Jiji la Dsm, na kujionea jambo ambalo hakuna mamlaka inayolizungumzia wala kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Jambo nililoliona kuwa na changamoto kubwa ni ufinyu wa maeneo ya kuzika wapendwa wetu, nilichosikitishwa nacho zaidi ni pale baadhi ya maeneo makaburi yalichimbwa na kukuta miili iliyotangulia miaka kadhaa ya nyuma, kwa maneno mengine ni kwamba makaburi tangulizi yanaharibiwa.

Hili jambo linahitaji viongozi wa Mkoa wa Dar na Manispaa zake walitazame na kupata ufumbuzi wa kudumu. Natambua kuwa michango zaidi ya mawazo itatolewa na mashuhuda wengine, ila kwa ufupi hali si shwari.
 
Back
Top Bottom