Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Yatahadharisha Uwepo wa Mvua Kubwa Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Mafia Jumapili, 12 Novemba 2023

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA imetahadharisha uwepo wa mvua kubwa kwa Jiji la Dar es Salaam kwa siku ya kesho, Jumapili Novemba 12 2023.

Utabiri wa TMA unaonesha mvua hiyo itakayoenea hadi katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tanga,
Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia na mikoa ya Lindi pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa ya TMA imeandikwa:

"VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KUJITOKEZA KATIKA MAENEO MENGI YA MIKOA YA TANGA, MOROGORO, PWANI (UKIJUMUISHA VISIWA VYA MAFIA) NA DAR ES SALAAM PAMOJA NA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA."

Mvua hizo zitaleta athari za mafuriko kwa baadhi ya maeneo, pamoja na n kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi hivyo sekta na taasisi zinatakiwa kuchukua tahadhari.

Screenshot 2023-11-11 at 18.46.56.png
 
Hata sasa hivi maeneo ya City Center mvua ni kubwa mno hadi game ya Man u na Luton inakata kata.
Man u tunapata goo
 
Back
Top Bottom