Mamilioni wamehama CHADEMA kumfuata Lowassa kimya kimya

Mamilioni wamehama CHADEMA kumfuata Lowassa kimya kimya

Nasikia waganga wa mlingotini sasa hivi ni matajiri
mwaka wa nne huu mnalia lia kuhamahama, mzee wenu huko kashikwa pabaya ataita hadi waganga nyumba nyeupe
 
Huyo ni kati ya vijana wasiyo jitambua ndani ya ccm
Ikiwa mamia wamehama kimya kimya kuja ccm kinachowapa jeuri ya kutumia nguvu kubwa ili mshinde chaguzi ni nini?
 
Umekosea sana kwa kumwita "kaka" huyo ni dada
Duh...!hii si itakuwa hatari sana kwa Chadema kuelekea 2020?.
Any way, naunga mkono hoja ya mtafiti wetu Kaka Wakudadavua, kuwa utafiti hupingwa kwa utafiti, japo ule utafiti wa Twaweza kuhusu kupungua umaarufu, haukupingwa kwa tafiti bali kunyanganya passport ya mtafiti!.
P
 
Unavyoandika as if Lowassa ni mpinzani wa kwanza kurudi CCM.

Ngoja nikusaidie, upinzani ni spirit sio viongozi. Ndio maana viongozi wanakuja na kuondoka, na wengine mpaka wanakufa. Lakini upinzani haujawahi kuisha.
 
Mi nacho elewa watu sasa wameamua kuwa wanafiki siku ziende jiwe amalize muda wake aende ila in short hakubaliki.
 
UKIONA MTAFITI ANATANGULIZA SENTENSI; "UTAFITI HUPINGWA KWA UTAFITI" JUA TAYARI HIZO NI PUMBA KWA MSHAHARA WA BUKU SABA UTAFANYAJE UTAFITI? HUU ULOULETA HUMU NI USHILAWADU TENA WA KIBASHITE
 
Umekosea sana kwa kumwita "kaka" huyo ni dada
Huyo ni kaka, alijitambulisha kwangu kama kaka, wengi wanamchanya na yule naibu waziri wa sekta yangu, sio yeye, naibu waziri hawezi kuwa kilaza kama huyu kaka kila siku ana posti utumbo humu na makorokocho kibao.

Huyu kaka ni kilaza fulani, wakati waziri ni kipanga fulani, kichwa cha UDSM.
Alipokuwa Chadena alikuwa ni think tank, sasa hayupo ona Chadena inavyo yumba, sasa yuko CCM, angalia jinsi CCM iinavyo chanua.
P
 
Nadhani watu wameamua kutofanya Siasa kutokana na mazingira na kuendelea na mishe mishe zao,maana Si kila mtu ni jasiri kusimama,maana saizi jela nje nje
Huyu aliyeleta maada hii amramua kujifurahisha mwenyewe,ni upuuzi mtupu,Hebu ngoja tufanye free & fair election uone moto wake
 
Ndugu zangu,

Baada ya Mbowe kuja na povu huku akimdhihaki Lowassa baada ya kukitelekeza Chadema huku akitamba kuwa kaondoka yeye (Lowassa) na familia yake hakuna aliyemfuata.Niliamua kunyamaza kimya na kufanya utafiti kabla ya kujibu.

Nilianza kufuatilia kundi la "ulipo tupo" na kubaini wamemfuata,niliangalia majimbo ya Dar mfano Ubungo,Kawe,Kibamba na Segerea kwa kweli huku mbeleko ya Lowassa iliwabeba wagombea udiwani na ubunge wa Chadema mwaka 2015 nako hali ya Chadema ni mbaya.

Nikifanikiwa kupita maeneo ya Moshi,Siha,Hai na Rombo wengi wameondoka Chadema kimyakimya.Pia nimepita majimbo yote ya mkoa wa Arusha huku ndio kabisa Chadema inapumulia mashine,baadaye nikaenda mkoa wa Manyara huku hata ule upinzani mdogo umeyeyuka.

Zaidi,kwa haraka haraka nikaangalia wale wenyeviti wa baadhi ya mikoa na wilaya wote wameondoka Chadema.

Baadhi waliobaki Chadema ni Sumaye,Mahanga na Salim Ally pamoja na kundi la kijasusi ambalo limesheheni "wasiojulikana" ambao wanabaki kufanya kazi maalum ya kumsaidia Kada Mbowe kudhibiti wajuaji na viroboto.

Utafiti hupingwa kwa utafiti si vilio,kejeli na matusi.

Nawasilisha.
Baada ya kuhama wakajenga viwanda mamilioni kimya kimya pia
 
Kwa taarifa yako Lowassa hakuja na kura yoyote ukiachia tamaa ya kina Mbowe na genge la kutaka pesa na kuishia kukitia chama nuksi. Ndani ya cdm Lowassa alikuta chakula mezani, halafu akaishia kuwa mgawaji. Lowassa hakuwa na mchango wowote kwa chama hasa kwa mantiki ya siasa zaidi ya yeye kukitumia chama kukidhi matakwa yake. Na kama kuna waliomfuata waendelee na akiona kuna yoyote aliyemuacha ahakikishe anaondoka.

Huyo mzee hawezi siasa na hatakaa aziweze maana alizoea siasa za kubebwa na vyombo vya dola. Nitajie siku uliyomuona Lowassa akijenga hoja zaidi ya nusu saa, zaidi ya kusikia wapambe wake wakisema kwamba ni mtu wa maamuzi magumu. Alaaniwe Mbowe na genge lake kukitia chama nuksi kwa tamaa ya vipande 30 vya fedha.
Wewe kijana kuwa makini usije ukashughulikiwa na vijana wa mbowe wasiojulikana, huwezi kumlaani kiongozi wetu mpendwa hadharani namna hii. Amekitoa mbali sana hiki chama. Kila jambo alilolifanya, alifanya kwa nia njema ya kukijenga chama chetu ikiwemo kubadili gia angani.

By the way, Ukitaka kujua nguvu ya Lowassa muulize Halima Mdee, Mnyika na Kubenea. Sasa hivi wanahaha kutafuta shughuli za kufanya mtaani maana ubunge mwisho 2020. Mtu pekee wanaemtegemea kuwapa kiki ni Lissu. Nae hawana uhakika nae ndo maana unaona anarudi September hii ili wakamtest kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kama Umaarufu wake ni halisi au wa kwenye mitandao.
 
Back
Top Bottom