Mfiaukweli
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 5,636
- 8,779
Ndugu zangu,
Baada ya Mbowe kuja na povu huku akimdhihaki Lowassa baada ya kukitelekeza Chadema huku akitamba kuwa kaondoka yeye (Lowassa) na familia yake hakuna aliyemfuata.Niliamua kunyamaza kimya na kufanya utafiti kabla ya kujibu.
Nilianza kufuatilia kundi la "ulipo tupo" na kubaini wamemfuata,niliangalia majimbo ya Dar mfano Ubungo,Kawe,Kibamba na Segerea kwa kweli huku mbeleko ya Lowassa iliwabeba wagombea udiwani na ubunge wa Chadema mwaka 2015 nako hali ya Chadema ni mbaya.
Nikifanikiwa kupita maeneo ya Moshi,Siha,Hai na Rombo wengi wameondoka Chadema kimyakimya.Pia nimepita majimbo yote ya mkoa wa Arusha huku ndio kabisa Chadema inapumulia mashine,baadaye nikaenda mkoa wa Manyara huku hata ule upinzani mdogo umeyeyuka.
Zaidi,kwa haraka haraka nikaangalia wale wenyeviti wa baadhi ya mikoa na wilaya wote wameondoka Chadema.
Baadhi waliobaki Chadema ni Sumaye,Mahanga na Salim Ally pamoja na kundi la kijasusi ambalo limesheheni "wasiojulikana" ambao wanabaki kufanya kazi maalum ya kumsaidia Kada Mbowe kudhibiti wajuaji na viroboto.
Utafiti hupingwa kwa utafiti si vilio,kejeli na matusi.
Nawasilisha.
Naomba maana ya hayo maneno mawili kwenye bold. Na analysis yangu juu ya "utafiti" wako inanifanya nihitimishe KUWA WEWE NI MZUSHI (in case hujui: "baadhi" inamaanisha kuna sehemu iliyobaki na "wote" hakuna kilichobaki).
Asante kwa kuleta kichekesho.