Mambo ya siasa kwenye michezo yasipuuzwe

ankol

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
2,113
3,486
Wasalaam wandugu,
Kuna kitu naona kina puuzwa siku kadiri zinavyokwenda. Ila huenda ikaja kuwa hatari zaidi mbeleni endapo zitaendelea kupuuzwa.
Ni kweli tuna mahaba na vyama vya siasa na wanasaiasa zetu, ila hakuna sehemu nyingine tunayoweza ku express mahaba yetu zaidi ya kwenye kumbi za burudani?
Ubebaji wa mabango kwenye sehemu za michezo zipigiwe marufuku, kwani naona ni time bomb mbeleni huko wenye vyama vingine wakibeba mabango itakuaje?
Naomba jeshi letu adhimu lisiruhusu mabango ya siasa kwenye semehu za michezo, watu wanaenda kuburudika na si kuhubiriwa siasa. itoshe kusema leo mnachekelea mnaona sawa, na haoo wenye vyama vingine wakianza kuweka mabango yao msije kukengeuka maana wenyewe mnalifumbia macho hili.
Ikumbukwe michezo huonyeshwa sehemu yoyote duniani, mtazamaji atakapoona mabangobango atapima hasa iq ya watu wa Taifa letu.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom