Mambo usiyoyajua kuhusu Nyumbu

Mambo usiyoyajua kuhusu Nyumbu

Ukienda katika mbunga nyingi za wanyama hapa Tanzania utawakuta wanyama aiana ya Nyumbu, wanyama hawa wakati mwingine huitwa zero brain, yaani wanyama wasio na akili. Sababu inayowafanya waitwe hivyo ni uwezo wao wa kutunza kumbukumbu na waoga wao japo ni wapole sana. Wanyama hawa utawakuta kwa makundi mengi nafikiri ndiyo wanyama wengi katika mbuga zetu. Pamoja na wingi wao hauwasaidii kujilinda na maadui.

Katika mbuga ya Serengeti utawaona wakivuka mto Mara kuelekea upande wa pili wa mto, akipita nyumbu moja kati kati ya mto akakamatwa na kuliwa na mamba nyumbu waliobaki husahau na kuendelea kupita hapo hapo na kuliwa wenye bahati huvuka, lakini pia Nyumbu wakiona simba anawanyemelea huwa hawana uwezo wa kujihami, hata simba akiondoka nyumbu husahau mara moja kama Simba alitafuna mwenzao.

Watanzania tuna sifa kama za mnyama nyumbu. Kwa nini ninasema ni sawa na nyumbu; sifa alizonazo nyumbu ndiyo hizo tulizonazo Watanzania. Watanzania ni waoga sana katika Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo nchi ambako nyumbu hupatikana kwa wingi kama walivyo Watanzania katika eneo hili.

Watanzania ni wepesi wa kusahau adui, hupenda kupita njia ile apitayo mnyama nyumbu hata kama kuna hatari. Utawaona Watanzania kwa makundi wakivuka mto mara hata kama baadhi wameliwa na mamba au simba. Simba na mamba huwawinda watanzania na kuwala, hulalamika sana kipindi hicho kuwa simba na mamba wamewashambulia na kuwaua lakini baada ya muda husahau kabisa kama simba na mamba aliwahi kuwadhuru na anaweza kurudia mchezo wa kuwatafuna.

Kwa usahaurifu huu wa Watanzania kwa nini tusiitwe zero brain kama wanyama wetu nyumbu ambao hawaoni hatari iliyo mbele yao? Wakati tukielekea katika uchaguzi wa mwaka huu hatuoni hatari zilizo mbele yetu, tumeshahau tulivyojeruhiwa na baadhi ya wagombea.

Nchi yetu ni masikini japo haistahili kuwa masikini, watu wameweka mapesa nje ya nchi, wamepiga dili kubwa mbalimbali wakituacha hoi bin taabani tukibeba zege la misamaha ya kodi za matajiri.

Kwa kipindi cha miaka 10 kashfa nyingi zilikuwa katika wizara nyeti ya nishati na madini, wizara hii ndiyo imekuwa mto Mara, watanzania tumeliwa ndani ya mto huu ukiacha Simba BoT.

Watanzania sasa utawaambia nini kuhusu simba hawa wanaotaka kuwa viongozi wetu, kama waliweza kututafuna wakiwa watoto je sasa wakiwa wakubwa itakuwaje, mfano kuna watoto walibeba pesa kwenye viroba kutoka pale benki ya STANBIC lakini mpaka sasa mifumo ya usalama ya nchi imepata kiharusi kuwakamata au kuwatambua.

Kuna walio nunua mitambo mibovu kwa pesa nyingi , sasa wanatudanganya eti tuvuke mto mamba hawali nyama ya nyumbu tena, wanakula majani tu. Kwa kuwa watanzania ni zero brain tunaelekea kuamini kuwa mamba wameacha kula nyama sasa wanakula majani.
 
Kati ya wanyama wote wa porini hakuna mnyama anayenishangaza kama nyumbu. Nyumbu ni kati ya wanyama wanaozaliana kwa wingi sana. Idadi yake kwa mbuga kama serengeti inaweza kuwa kubwa kuliko wanyama wote.

Kuna mambo mawili yanayonishangaza sana kwa nyumbu. Kwanza ni woga wake wa kukabiliana na adui pamoja na wingi wake. Simba anapovamia kundi la nyumbu wanabakia kutokuwa na umoja na hivyo kuuwa kirahisi wakati huo huo jirani yake wanaofanana kwa kila kitu Mbogo si rahisi simba kumvamia kijinga kumfanya kitoweo. Nyumbu hawana ushirikianao kabisa katika kubakabiliana na adui wao.
 
Kati ya wanyama wote wa porini hakuna mnyama anayenishangaza kama nyumbu. Nyumbu ni kati ya wanyama wanaozaliana kwa wingi sana. Idadi yake kwa mbuga kama serengeti inaweza kuwa kubwa kuliko wanyama wote.

Kuna mambo mawili yanayonishangaza sana kwa nyumbu. Kwanza ni woga wake wa kukabiliana na adui pamoja na wingi wake. Simba anapovamia kundi la nyumbu wanabakia kutokuwa na umoja na hivyo kuuwa kirahisi wakati huo huo jirani yake wanaofanana kwa kila kitu Mbogo si rahisi simba kumvamia kijinga kumfanya kitoweo. Nyumbu hawana ushirikianao kabisa katika kubakabiliana na aduo wao.

Unamaanisha CUF au?
 
kaaazi kweli!
 
Akili za watanzania hata Nyumbu ana afadhali.
 
Bora nyumbu wana afadhari sisi ni wa kipekeee.Mtu alituibia akaja na mkataba wa kitapeli richmond nchi nzima tukalia kwa uchungu.Leo miaka nane baadae tumesahau kabisa Lowasa yuko mtahani anadunda anatakuwa raisi
 
Bora Nyumbu wakati mwingine wanajiongeza kwa kutumia akili ndogo tu waliyonayo kuliko wa danganyika.
 
Nyumbu anaweza kutumia akilu yake ndogo kujikimu na watoto wake. Wadanganyika hata mlo wa siku hawawezi. Shida kila kona. Midomo tuuu na mipasho ya kishenzi mwanzo mwisho.Ukimpa book anakupigia kura. Bila kuangalia hatima yake kesho.
 
Huo ndiyo uhuru huria ambao haufai hata kuigwa na hata hao nyumbu wanaozungumzwa hapo. Mtu anayejiondoa hata utu wake na kujipachika sifa anayoona inafaa ili tu kufurahisha genge, mtu huyo ni wakuogopwa kama gonjwa hatari la ukoma, kwa mazingira ya sasa ukiwa Afrika ya Magharibi anapaswa kuogopwa kama ebola. Hata haya huna? Wewe ni mtu au jitu tumwa?
 
tusiwalaumu sana ila tutafute solution na vipi tunaweza kuwasaidia hawa nyumbu.
 
tusiwalaumu sana ila tutafute solution na vipi tunaweza kuwasaidia hawa nyumbu.

Ni hatari sana mtu kujiona anakili sana kumbe akili hiyo wenzake wanamuona kuwa ni mgojwa wa akili, na hata msemo wa kiswahili unatuambia akili nyingi huondoa maarifa. Lakini hawa watu waamini wako sahihi mwishowe wanao jiamini kipumbavu huangamia wakidhani wako sahihi na kuwatuhumu na kuwalinganisha wenzao kama nyumbu.
 
Its the case of comparing the comparable,mnafananishwa kwa kuwa mnafanana,haihitaji akili kubwa kujua,mafuriko yaliyoikumba dar juzi ni kielelezo tosha cha akili za nyumbu,mnaishi mabondeni,mvua ikinyesha inawasomba mnahama, jua likiwaka mnahamia tena mabondeni,akili za nini hizo?
 
Watumwa utawajua tu teh teh teh!
 
Nyumbu anaweza kutumia akilu yake ndogo kujikimu na watoto wake. Wadanganyika hata mlo wa siku hawawezi. Shida kila kona. Midomo tuuu na mipasho ya kishenzi mwanzo mwisho.Ukimpa book anakupigia kura. Bila kuangalia hatima yake kesho.

Naona unahangaika ku edit post yako mwenyewe ikionyesha jinsi gani unashikiwa mawazo na kutumika!tulia utaelewa tu namaanisha nini!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom