Nani mbabe (Ep 2): African Lion vs Silverback Gorila

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,730
10,033
Katika muendelezo wa wababe katika viumbe leo hii tunawakutanisha wafalme wakali wawili kutoka barani Afrika. Je, ni nani ana advantages kubwa kumshinda mwenzake?

images.jpeg

The king of the jungle or the dangerous Gollila nani atashinda pambano hili?

Simba na Sokwe/gollila karibu wote wanakuwa na uzito sawa wanaposhabihiana kiumri. Lakini namna yao ya maisha na tabia zinatofautiana sana kwa kila mmoja. Tofauti na wanyama wengine, pair hii ya mkutanisho haina matokeo ya kufahamika au kutabirika. Wote simba pamoja na gollila wanagawana nguvu sawa lakini kila mmoja zikiwa za kipekee.

SIMBA: Wanajulikana kama wafalme wa mwitu. Watu kote duniani wanamchukulia kama alama ya nguvu na mamlaka. Ni wapili kwa ukubwa duniani katika jamii ya paka baada ya tiger. Ni paka wanaoishi kijamii kwa umoja katika kundi lijulikanalo kama PRIDE.

UKUBWA NA MUONEKANO
  1. Simba ni jamii pekee ya ambayo paka ambayo wanatofautiana kimaumbile kulingana na jinsia. Wakiume ni wakubwa kuliko wakike.
  2. Urefu wa mwili wa simba ni kutoka 4.5 - 6.5 feet ( 1.7 - 2m), mkia wa 26 -40 inch(0.6 - 1m)
  3. Uzito ni kati ya 120 mpaka 190 kg.
  4. Wote simba wa kike na kiume ni paka wenye nguvu sana za misuli, kichwa pamoja na masikio ya duara. Simba wakubwa wa kiume pekee ndio wana muonekano wa brown, ukutu au manyoya yafananayo na nywele nyeusi toka Shingoni mpaka kifuani.
MAKAZI NA WAPATIKANAPO
  • Simba wana jamii ndogondogo zilizojitenga kwa ukubwa tofauti.
  • Kihistoria, simba waliweza kupatikana karibu eneo lote la afrika, lakini kwa sasa wamepungua na wanapatikana zaidi afrika mashariki, afrika kaskazini magharibi na kusini.
  • Kutokana na uharibifu wa binadamu kwa wanyama hawa, kwa kidogo sana wanapatikana katika eneo dogo sana huko Gir forest national park India, Asia.
  • Simba wanapendelea kukaa maeneo yenye vichaka vichaka na majani mengi na yalio karibu na vyanzo vya maji.
UWINDAJI
  • Simba wanapendelea kuwinda katika maeneo yaliyo wazi na kwa makundi. Simba hawapatikani katika misitu mizito yote duniani.
CHAKULA/DIET
  • Simba ni carnivores maana yake ni wala nyama.
  • Mawindo ya simba kawaida huwa nyumbu, pundamilia, swala na mara chache sana wanyama kama nyati na twiga na wanyama wengine wakubwa.
  • Muda mwingine simba huwinda tembo wadogo, vifaru au viboko.
  • Simba pia hunyanganyana chakula, hufukuza fisi na wanyama wengine walao nyama kwenye windo alilopata kuliua.
MBIO/SPEED
  • Simba anaweza kukimbiza windo lake kwa kasi kubwa, mfano anaweza maliza kiwanya cha mpira ndani ya sekunde 6 hadi dakika 2.
TABIA
  • Simba anaweza kuchukua muda wake mwingi kupumzika tu, hata hivyo huchukua mpaka masaa 20 kwa siku kwa ajili ya kulala.
  • Wakati wa mapunziko, simba hupata muda mwingi wakiwa pamoja kijamii wakipiga stori za hapa na pale, kusimuliana visa na mikasa ya wanayopitia kwenye mizunguko yao ya kila siku.
  • Maisha ya katika kundi huruhusu simba kuwinda chakula chao pamoja simba majike hugawanyika pande tofautitofauti kumzunguka windo walilokusudia.
  • Pamoja na nguvu walizonazo, simba mara nyingi hushindwa zaidi kuliko kufanikiwa kuua windo lao.

GOLLILA/ SILVERBACK GOLLILA: Golila wa kijivu ni moja ya jamii za sokwe wenye miili mikubwa iliyosheheni misuli na nguvu za kutosha. Sifa moja wapo ya gillila hawa wenye manyoya ya kijivu mgongoni huonyesha ni gollila wakiume waliokomaa. Silverbak gollila huishi zaidi katika masitu mikubwa katika milima hasa Afrika. Kuendana na ukubwa wa miili yao, silverback gollila anahitaji kula chakula cha kutosha kila siku. Na kuhakikisha wamepata virutubisho vyote muhimu katika miili yao.

UKUBWA NA MUONEKANO
  1. Silverback ni wakubwa sana. Urefu wao wanaposimama wamenyooka ni kuanzia mita 1.7 - 1.9.
  2. Na uzito mpaka kilo 160. Masikio ya silverback yanaonekana madogo kwa kichwa chake.
  3. Wakiume wana mnyanyuko mkubwa wa mfupa juu ya mafuvu yao na mgongoni. Inayosapoti misuli ya taya zao na meno.
  4. Silverback gollila pia wana manyoya mengi na ni mengi kuliko jamii nyingine za gollila.
  5. Silverback hupata muonekano huo wa kijivu mgongoni kati ya umri wa miaka 12. Watoto wa kiume ambao bado hawajapata muonekano huo huitwa "BLACKBACKS".
MAKAZI NA WAPATIKANAPO
  • Silverback gollilas wanapatikana zaidi nyanda za juu na chini katika misitu ya kiikweta afrika karibu na pwani ya Cameroon mpaka Jamhuri ya afrika ya kati, Equatorial Guinea, Gabon, Nigeria, DRC,, Angola na Republic of Congo.
  • Misitu ya wazi ya kitropia inayoruhusu mwanga mwingi kufika ardhini, inatoa makazi bora zaidi kwa gollilas.
CHAKULA/DIET
  • Gollila ni wala majani. Hata hivyo, hula chochote kinachokatiza mbele yao kama wadudu au wanyama wadogo waliopo kwenye eneo au matawi wanalokula majani.
  • Gollila pia wanakula mimea na magogo waliyooza. Silverback wanakula 40 pound (18 kg) kila siku.
TABIA
  • Gollila ni wanajamii wakubwa wanaoishi katika vikundi vya kifamilia vijulikanavyo kama TROOPS.
  • Wakiongozwa na kulindwa na dume kuu la kundi. Wanawake 3 - 4 waliokomaa kwa dume 1 au 2, watoto na vijana 3 - 6 na vichanga kutoka familia moja.
  • Silverback wazee pia wanaweza kuwepo kati ya sehemu ya wanafamilia.
  • Kundi kibwa la gollilas linaweza kuwa na jumla ya washiriki 20.

===>NANI ATASHINDA KATIKA PIGANO KATI SIMBA NA SILVERBACK GOLLILA?
images (2).jpeg
images (1).jpeg


GORILLA
  • Meno makubwa ya gollila sio makhususi kwa ajili ya nyama, ila kwa kujilindia, Na bado inatosha kwa mlinganisho kwa wanyama wala nyama kama mshindani wake: Simba dume!.
  • Mikono ya silverback gollila ina nguvu sana hata kama hana kucha kama za simba.
  • Anauwezo wa kutengeneza silaha kwa kutumia miti na mawe yanayomzunguka.
  • Kama simba atajaribu kumshambulia silverback kichwani, anaweza kutumia nguvu zake za mikono kushusha uzito wa maana na labda hata utakaoweza kumuua.
SIMBA
  • Simba ni wawindaji kiasili.
  • Hata kama hawalingani level moja ya kiakili na mshindani, simba kimwili kajengwa kwa ajili ya kuwinda.
  • Kucha za kutisha za simba pia zinaweza kusababisha vidonda vikubwa katika mwili wa gollila, hata kuendelea kuhangaika kujitoa katika taya za simba.
  • Simba pamoja na nguvu za kiwindaji, bado ana ujuzi wa kishambulizi.
  • Kutokana na uwezo wake mdogo wa pumzi, itamtegemea na ukubwa wa namna atakavyoanzisha shambulio kwa adui yake.
HITIMISHO: kulingana na uwezo wa kila mmoja kwa ufupi kama ulivyoelezewa na huu ndio uamuzi binafsi nani anauwezekano mkubwa wa kuibuka mshindi.

~ Faida moja atakayoipata simba ni kama wakipigana usiku. Silverback gorillas wana uoni zaidi au pungufu zaidi kuliko binadamu, ambapo ina maana ana uoni hafifu wakati wa usiku. Kwa sababu gollilas wanategemea zaidi mwanga, hivyo kuwakutanisha wawili hawa usiku kutampa silverback gollila uwezekano mkubwa wa kushindwa.

MSHINDI: Silverback Gorilla. 🥇
 
Back
Top Bottom