Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Kwani cdm nani ana mvuto kuzidi nape?

heu toa upumbavu wako hapa..kama huna cha kuongea kaa kimya....yaani wewe na akili zako unamuona nape ni mwenye upeo na akili timamu?
 
Kunenge,Kaka hili neno kuzaliwa upya umeliazima kutoka kwenye biblia nakupa pole sana
sababu Kwenye biblia Yesu anamaanisha kuzaliwa upya kutoka katika wafu, sasa kwani ccm imeishakufa,
au ndio unaichuria dakika za mwisho mwisho?
 
Ijivue gamba la UFISADI au hilo halivuki!
 
kama ni falsafa ya kujivua gamba basi watajivua sana magamba hadi kufa kwao..........:rip:CCM.
 
Tutakapokuwa tukiandamana nchi nzima, tutataka kujua hayo magamba yametupwa wapi!
 
Mvuto ndio nini? watanzania hawataki mvuto wa mtu,

watanzania wanataka kuona serikali inajielekeza

katika kushughulikia mambo ya msingi kwa ufanisi wa mipango, mikakati, mahamuzi na vitendo.
watanzania wanataka kuona serikali yao inajielekeza katika kupambana na rushwa na ufisadi.
wanataka kuona serikali inayojielekeza katika kuboresha huduma za afya, elimu, ufafiri na usafirishaji.
serikali inayojielekeza katika kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa ya watanzania wote
serikali inayoendeshwa kwa misingi ya sheria na utawala bora

Haya mabadiriko ya watu yatakuwa na msingi kama watu hawa watakuwa na uwezo wa kufanya
mabadiliko ya kisera na namna chama hicho kitakavyojielekeza katika kuisimamia serikali kuu
ama sivyo hawa wanaweza kuresign mapema zaidi.
 
sasa mwataka ****** ajivue nae gamba si maandiko yatatimia ya kuwa kimekosa dira na mwelekeo....saratani bado inakitafuna kujivua gamba bado hakujasaidia kitu wanahitaji x-ray ya nguvu la sivo 2015 watakiona cha moto.wasiwasi wangu MUkama ana skendo kibao,Nape ndio kabisa zero, Zakhia mhhhhhh hata uwaziri ulimshinda nashangaa hadi leo hajapanda Kisutu kwa tuhuma za ufisadi wa majengo pacha na EPA, KInana sidhani kama ana jipya.Ni sawa na kuweka kiraka kilichozeeka kwenye nguo iliozeeka...
 
Ndugu zangu uimara wa chama unategemea sana uongozi thabiti wa mwenyekiti wa chama.Hawa wote mliowalazimisha kujiuzulu walikuwa wanafanya hayo walioyafanya kwa baraka za mwenyekiti!...

Kumbukeni msemo wetu wa enzi zile "Zidumu fikra za mwenyekiti"...hii ilitokana na uongozi dhabiti wa Mwalimu Nyerere katika kukiongoza chama mpaka watu wakatamani fikra zake zidumu.John Chiligati ana upeo na uwezo mkubwa tu wa kiuongozi kuliko hata hawa mlioteuwa,..George Mkuchika vilevile na hata Makamba ambaye aliyokuwa anayafanya alijua mwenyekiti wake atayafurahia!...

Ninachosema hapa ni kwamba mlichokifanya mmetoa jasho na wala siyo gamba!..Gamba lenyewe ni mwenyekiti ambaye marafiki zake ambao ni manyangumi ya ufisadi yanakiyumbisha chama huku yeye akitabasamu.
 
CCM imeshaoza vibaya mno, hawawezi kutoa gamba, labda watoe na minofu yote iliyoza, kubadilisha secretarieti pekee hatasaidia kurudisha mvuto kamwe
 
Agree, lakini ataweza kuongoza majeruhi wengi namna hiyo? na How strong he is to handle kundi la RA au EL plus Makamba?
Hapo utingo shughuli ndipo ilipo watu kama akina Lowasa, Chenge, Rostam ataweza kuli-handle hilo kundi
 
wadau naleta hoja jamvini na kuuliza uteuzi wa nape nnauye kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa ccm ni kurudisha imani ya chama kwa vijana na kuachana na mafisadi?

1. Najiuliza hivi kutokana na nape kukubalika sana na vijana ila hakubaliki na uvccm ila walio nje wana mkubali sana kwa hoja na misimamo na mitazamo yake ambayo mara nyingi imekuwa iki wakwaza waliokuwa vigogo wa ccm na uvccm

2. Kuhusu mafisadi, nape amekuwa na mtazamo tofauti na usiokubaliana na mtazamo wa kundi la mafisadi, kwa uteuzi huu ina maana jk ameamua kuwatosa swahiba zake?

3. Hivi karibuni uvccm walitoa tamko la kuendelea kung'ang'ania nape kuvuliwa uanachama wa jumuiya hiyo na sasa ana kuwa bosi wao je viongozi wa jumuiya hiyo wako salama kweli au mvurigano ndani ya chama unaendelea?
 
Wadau napenda kuweka hoja barazani nikiamini kwa uteuzi wa zakhia meghji kuwa katibu wa uchumi na fedha ccm bado hawaja jivua gamba lolote, bado raia tunakumbuka kashfa zake alizokuwa nazo

1. Nadhani hatujasahau maelezo yake tata ya fedha za benki kuu mpaka akaja kudanganya taifa ni pesa za usalama wa taifa then baadae kusema gavana kampotosha

2. Nani kasahau blanda na uozo alioufanya akiwa waziri wa mali asili na utalii?

Swali ambalo najiuliza ni kwanini jk anaedelea kumng'ang'ania wakati huu wanadai wanajivua gamba?au zile tetesi mtaani kuwa ni mkwe wake zina ukweli?
 
Infinite solution na kama ccm ni waungwana ni kustep down wameshasaturate wachie wengine wareform nchi watarudi tu wasijali hata ufanye substitute ngapi barcelona wakishakuzidi wamekuzidi banaaa alaaa
 
Nyoka ni nyoka tu hata akijivua gamba bado ataendelea kuwa nyoka; chama kimevurugika sasa kikijivua gamba maana yake kitakuwa kikali zaidi kwa kutetea ufisadi...Tafakari!!!!!
 
Wadau nimesoma katika gazeti moja wamemnukuu mkuchika akielezea kuhusu kujiuzulu kwa sekretarieti ya chama na kamati kuu akisema wameamua kuafanya hivyo ilikuleta uhai mpya wa chama.
Amedai kamati kuu mpya itakuyoundwa wamekubaliana haitajumisha watu wenye kofia mbili ili kuwapa muda mwingi wa kufanya shughuliza chama sasa kwa habari zinazo julikana mpaka sasa na hazijakanushwa mpaka sasa wateule wapya wana kofia mbili tayari hebu mkuchika jitokeze ukanushew taarifa hizo au utoe ufafanuzi vizuri

1. Nape ni mkuu wa wilaya
2. Dr. Zainabu nchimbi mkuu wa wilaya
3. Zakhia meghji - mbunge wa kuteuliwa

au mnaendeleza kawaida yenu ya kuropoka?
 
Ubunge lakini hawakupewa na CCM, ni wannchi waliwapa. Siasa sio kama mathematics kuwa logically if x>0 then it means X is positive number!

na uanachama wa ccm hawakupewa na wapiga kura, so chama kina haki ya kung'oa shina. Kama wana uwezo wa kushikilia matawi yao, good!
 
Back
Top Bottom