Mambo matatu ya kurekebisha ndani ya CHADEMA

Mambo matatu ya kurekebisha ndani ya CHADEMA

Umejiuliza ni watanzania wangapi wenye uelewa kama wako?

Ni wangapi wenye uwezo wa kuchambua pumba na mchele?

Mtu asie na uwezo wa ku-reason akitajiwa alianza Mtei akafuaya Bob Makani na sasa Mbowe wote wakiwa ni wachaga ni rahisi sana kuamini hizo propaganda.

Tusiotoe mwanya wa watu kutengeneza propaganda.
Hivi Bob Makani ni mchaga? Hii ndiyo impact ya propoganda unaaminishwa hata yasiyo ya kweli. Propoganda haitakoma kwa kufanya unavyoshauri. Hata nyie chadema mnapiga propoganda hizo hizo kwa ccm na vyama vingine na kuna watu wanaowaamini.
 
Hii Bob Makini ni mchaga? Hii ndiyo impact ya propoganda unaaminishwa hata yasiyo ya kweli. Propoganda hautakoma kwa kufanya unavyoshauri. Hata nyie chadema mnapiga propoganda hizo hizo kwa ccm na vyama vingine na kuna watu wanaowaamini.
Usishangae kamanda ccm wanatembea na fuko la gawiwo la watu kama wakina Slip
 
Wacheni kongea upumbafu, uwezi kutwambia eti north ndiyo wenye uwezo wacha upinokyo.
 
Don't allow others to set the agenda for you. We must continue to put them on the defense. We must not take instructions from them. Yaani unashauri tumwachishe Mbowe kugombea tena uenyekiti kwa sababu tu za kikabila?

It is not possible to be a little bit pregnant. Aidha CDM ina principles always au haina at all.

ID Yako inajieleza kwanini unatoa povu linapokuja suala la kutoa ushauri chama kiachane na ukabira... tumekupata Bw.Moshi.
 
Napenda kuwashauri CHADEMA watekeleze mambo matatu yafuatayo ili kuondoa propaganda chafu zinazosambazwa na CCM na ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa chama chetu.

Wana-CHADEMA,tunapaswa kutambua kuwa watu tunatofautiana katika uelewa wa mambo na katika mapokeo ya taarifa tunazoletewa au kuzisoma.

Kwa maana hiyo basi,mambo haya nashauri yatazamwe upya.
1.Ukomo wa kugombe uongozi urudishwe katika katiba ya chama na ikiwezekano ukomo uwe ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano.

2.Wanachama waruhusiwe kwenda mahakamni na mtu akishindwa kesi aruhusiwe kuendelea na uanachama wake.

3.Mh.Mbowe,kipindi chako cha sasa kikiisha,nakushauri usigombee tena na utoe fursa kwa wengine kugombea na wewe kama kiongozi, ujikite katika kuhakikisha chama kinapata mrithi bora,wa kuamimika na mwenye viwango.

Mchango ndani wako ndani ya chama ni mkubwa na wa kuthaminiwa sana ila ni vizuri sasa ukatoa nafasi kwa wengine ili kukinusuru chama na propaganda hizi.

4.Japo hatuchagu kiongozi kwa kuangalia kabila lake, lakini ikiwezekana katika uchaguzi wa mwenyekiti ajae jambo hili likaangaliwa kwa mapana na marefu yake.

Wenye akili na upeo wa kuona mbali watanielewa, ila wenye kukariri kuwa chama hakihitaji ushauri wa aina hii, watakuja hapa na vijembe na kejeli.

Niwaambie tu,hata kiburi na kujiamini kwa Zitto msingi wake ni uwepo wa hizi propaganda na ndio maana hata anapata public sympathy kutoka kwa baadhi ya watu na watu hao ni wengi tu huku mitaani tunakoishi.Fanya utafiti mdogo uone.

Propaganda zingine ni za msimu tu lakini sio hizi nilizoziongelea hapa.

Yangu ni hayo tu.
Kwenye hoja namba 2 vipi kwa mwanachama ambaye imethibitika kuwa ana kihujumu chama na kunaviashiria vyote kuwa akiendelea kuwepo ndani ya chama kuna hatari ya chama kufa,nao wakishinda kesi mahakamani wa endelee kuwa wanachama?na hatima ya chama kiusalama itakuwaje?
 
Last edited by a moderator:
Shame on you
Tusipojirekebisha ataandaliwa mwingine na atapita kulekule alikopita Zitto nae ataonekana kaonewa.

Watu tunaleta mawazo kuondoa hizo loophole alafu nyie wengine kazi yenu ni kupiga makofu tu na si kusaidia viongozi kimawazo.

Dawa ya msaliti ni kumuacha ajimalize mwenyewe na si kumwekea vipengele vya kumbana na kumfanya aanze kutafuta huruma nje ya chama na mwisho wa siku anaonekana kaonewa au chama kinaminya haki za watu.

Waacheni watu waende mahakamani na mwisho wa siku watajimaliza wenyewe.

Dawa ya msali si kumkomoa bali ni kumpa haki yake na hatimae atajimaliza mwenyewe.

Katika siasa ukipewa haki pasipo kuungwa mkono ni bure tu.

Mwanasiasa hakubaliki kwa kupewa haki zake za kikatiba n.k bali kwa matendo yake.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,

Mnakumbuka Mlisema CUF Si chama cha Upinzani tena? Kisa kimeungana na CCM Zanzibar? Mnakumbuka mlichosema kwa Mbatia baada ya kupewa Ubunge na Raisi? How comes leo mnashirikiana na watu mnaosema ni CCM B?

Mnaotaka Nyadhifa CDM mtakiua chama kwa tamaa zenu za Madaraka. Pumbavu kabisa, Wingi wa wenyeviti maana yake nini? Hao wenyeviti wanafanya kazi gani kubwa zaidi ya kueneza Propaganda tuu?

Nyie wote mpo kwenye Transition period, Umaarufu wa Pafyum za kichina, Unanukia unapojipuliza ukitoka nje unanuka jasho.

Nakumbuka NCCR enzi za Mrema, Kisha Cuf, Leo Mpo nyie, kesho sijui atakiwepo nani????

Acheni ku invest kwenye Maneno na Propaganda, Watu wanataka waone Output ya kuchaguliwa kwenu.

Nilisema Tz hakuna chama Pinzani. Kwa sababu, viongozi wote wana behavour zinazofanana na chama Tawala. Wote wana kashfa za wizi, Matumizi mabaya ya madaraka, Wote ni Reactive na sio Pro active.. Wote ni waoga wa kukosolewa, wote ni Mamwinyi.. Wote waongo, wote tamaa zimewajaa.

Kwakifupi Siasa za hii Nchi zinachosha, nashindwa kuelewa kwann Wananchi bado wana amini vyama vya siasa vitawakomboa. Hakuna kitu...

Watu hulia na wananchi wanapotafuta Kura tuu, wakishapata Madaraka tunaanza kuona True Pictures...

Nasema tena. PUMBAVU KABISA.

Hapo sasa......

Naona umeamua kuja na Id yako nyingine, naam ile moja haitoshi, umeona ukafukunyue nyingine ili uendelee kupambana..!! Anyway tuko pamoja tunakwenda Sambamba mpaka utakapo elewa kwamba kwa leo umekengeuka.!!!

Kwenye red para ya kwanza;
Hapo unabainisha nguvu ya Propaganda, hii hufanywa na kila chama bila kujari inaelekea chama gani..Naam kama ni mbovu ktk kujibu Propaganda hizo then shimo la kisiasa lipo kwaajili yako utumbukie na upotee kabisa..!!! Halafu pia tambua, Ktk siasa hakuna rafiki wa kudumu na Adui wa kudumu kinachoangaliwa ni Maslahi ya Chama na Taifa. Hapo ndipo utakapowajua Chadema kwamba ni chama cha namna gani? Na hapa inadhihirisha kwamba vyama hivi vitatu vinacheza ngoma ya nani na ni nani anaye chagua wimbo. Kama unaakili japo kidogo huhitaji kujua nani anafaidika kwa hilo...

kwenye Blue;
Tambua na tena elewa, Hapa nilipo sifahamiki kwa Diwani,Mwenyekiti wa kijiji,Mkiti chama kata achia mbali Mbunge,Dr Slaa,Makene na yeyote yule maarufu kwenye chama hiki. Nina kazi yangu ambayo namshukuru Mungu inanitoshereza kulea Familia ya watu kumi. Sina haja ya kujikomba kwenye siasa na wanasiasa ili nifanikiwe iwe kwa kuvizia Cheo makombo ama chochote kile. Na hapa kama hutaki kuamini sina haja ya kukuaminisha ya nini? itanisaidia nini? Mimi nafuata misingi ya chama na kwakweli Chadema imenivutia kuliko chama chochote kile hapa Tanzania (Huyo ni mimi wala si wewe hutaki acha)

Kwenye Bolded;
Ndugu nakupa pole sana, Eti unasema kazi ya wenyeviti wa chama hiki(Chadema) wanaeneza Propaganda?? Akili chovu kabisa hii....!!!! Njoo hapa Tdm, wenyeviti hawa tangu wamechaguliwa ni watu wanaowajibika kwa wananchi kwa kuumiza kichwa ni namna gani watawatumikia nje ya mfumo mbovu waliouzoea, Na hapa ninapo sema na wewe huko Sogea juzi wameshirikiana na wananchi kubuni na kujenga kituo cha afya (Ambacho hata hivyo wenye akili chovu kama wewe wamezuia kwa madai ati sehemu wanayotaka kujenga ni yao) Daaah ccm imeathiri watu vibaya sana...!!!!!

Kwenye Green;
Waswahili wana msemo kwamba aisifuye mvua imemnyea...!!! Hapa unatuonyesha tabia zako mbaya za uchafu na kujifanya wajisafisha kwa Perfume...!!! Naam umejidhihirisha wewe ni mtu wa namna gani? sina haja ya kuongeza maana waswahili hawapungukiwi misemo pale waliposema "Kinywa huumba"...!!!

Kwenye Purple;
Sasa hapa nani anapiga propaganda ndugu yangu? Sisi tunakufahamisheni ninyi mliokengeuka kwamba uelewa wenu ni finyu.. Na maskini wa Mungu hatukufahamisheni haya hivihivi bali kwa hoja mwanana. Kumbe kwenu kufanya hivyo ni Maneno matupu na Propaganda...Hahahahahah akili zilizojichokea hizi... ebooooooooo..!!!!!

Kwenye red para ya mwisho;
Hayo ni mawazi yako mfu na uzuri nilikwisha kusema hapo mwanzo ikiwa Mungu kanipa kinywa,masikio,Ubongo na ktk kuvitumia silipii kodi yoyote then nani wa kuniamulia cha kusema?.... Ndiyo kaka/Dada umetimiza matakwa ya ubongo wako kupitia kinywa chako ulichopewa na Mwenyezi Mungu, ambaye wakati akiumbahivi viungo katu hakusema wala hakukupangia limit ya kuongea..!!! Then sisi tusemeje??? Tukisema thibitisha huo wizi,uwongo na kila. ulichodai hapo utaanza kujiumauma..... Akili mfu hizi!!!

Hiyo para ambayo sijaibold wala kui-color, kwakweli ndipo inapoonyesha umtu wa namna gani? Na kwakweli unapaswa kuhurumiwa kwakutoifanyia kazi akili,Ubongo uliopewa na Mwenyezi Mungu..

Na kama huu tunaoandika hapa niUPUMBAVU KABISA....Then kaka/dada yangu sioni jina sahihi la kutumia kwa hiki ulichopost hapa, ila itoshe tu kusema, UMEKENGEUKA.

Nb
Nategemea kuona Id yako ya tatu hapa ndani, na utazifukunyua zote leo. Hebu Njoo!!!

BACK TANGANYIKA
 
Salary Slip

Unamtibu Mgonjwa ambae wenyewe wameshmkatia tamaa.

usifikiri hicho ulichoandika Mbowe hakioni,wanajua wanachokifanya na kwa bahati Mbaya wapo vijana wameahiriwa mitandaini kupambana na hoja kinzani dhidi ya tishio lilote la wakubwa kupokonya power yao.

Wapo tayari hata kuua ilimradi wabaki madarakani.

Hujui kuwa hata Mugabe ,Museven na Kagame wanawashauri,umewahi kujiuliza kwanini hawapishi wenzao madarakani?

Ifike wakati nawe ukate tamaa na kijiandaa kisaikolojia kung'atuka.

Mbowe kawekeza sana Chadema na huu ndio muda mgodi unatema,akibaki na wabunge watano naamini atang'atuka tu maana atakuwa hana chakupoteza tena.
 
Ohooooo...good, ukweli ni kwamba wapinzani wa chadema hawatakosa propaganda. Na kwa bahati mbaya ni propaganda zinazoenda mbali ya utanzania na za kujitoa ufahamu...tumeruka viunzi....kilichokuwa kikubwa ni kile cha u-ghaidi (bahati nzuri washiriki wa ughaidi huu kutokea ccm wameisha tubu).

Kuwa chdema ingekufa.....ulikuwa mpango kamambe ukimhusisha zzk ( ili halina ubishi tena). Salary slip ungana nami kukemea usaliti wa huu mbaya kutokea uliofanywa na zzk dhidi ya chama kilichomlea).


Kutompa barua zzk ambayo aliisubiri iliaitumie alivyo jua na badala yake yeye kushauriwa atoe barua ( kumbuka kuairishwa kwa hotuba yake juzi kutimiza shart hili) ni ushahidi mwingine kuwa zzk alikuwa na ratiba zake kichwani.


Tushukuru mahakama (probably) baadhi ya watendaji wa mahakama hiyo waliotonya mpango mzima wa ujanja wa zzk

Na labda nicrhukue msemo wa huyu jamaa...'ukombozi kwanza demokrasia baadae'....
 
Unaelewa maana ya propaganda? Ukweli hauitwi propaganda. Propaganda no uwongo unapkaeibiana na ukweli na asiyejua Kuwa ni uwongo hiamini kuwa ndiyo ukweli wenyewe. Maswaala yote uliyoyataja ndiyo ukweli wenyewe hivyo hiyp siyo propaganda
 
Binfsi nitaungana na wanamapinduzi wa kweli ambao wanatamani kuona kile wanachohubili ndichi kinafanyika na si ujanjaujanja wa watu kupiga pesa huku tukiendelea kuwashangilia.

Mbowe wahimize vijana waendelee kukusaidia kukulinda mitandaoni lkn Vita dhidi ya ufisadi lazima wanyonge tuungane kuwaunga mkono wale wanaoupinga kwa vitendo.
 
Unaelewa maana ya propaganda? Ukweli hauitwi propaganda. Propaganda no uwongo unapkaeibiana na ukweli na asiyejua Kuwa ni uwongo hiamini kuwa ndiyo ukweli wenyewe. Maswaala yote uliyoyataja ndiyo ukweli wenyewe hivyo hiyp siyo propaganda

You nailed it,umetumia busara sana kutifautisha propaganda na ukweli (fact)
 
Hivi Bob Makani ni mchaga? Hii ndiyo impact ya propoganda unaaminishwa hata yasiyo ya kweli. Propoganda haitakoma kwa kufanya unavyoshauri. Hata nyie chadema mnapiga propoganda hizo hizo kwa ccm na vyama vingine na kuna watu wanaowaamini.

CCM imempofusha macho huyo.Ni vijaba wa Zitto hao wanajifunua!
 
Binfsi nitaungana na wanamapinduzi wa kweli ambao wanatamani kuona kile wanachohubili ndichi kinafanyika na si ujanjaujanja wa watu kupiga pesa huku tukiendelea kuwashangilia.

Mbowe wahimize vijana waendelee kukusaidia kukulinda mitandaoni lkn Vita dhidi ya ufisadi lazima wanyonge tuungane kuwaunga mkono wale wanaoupinga kwa vitendo.

Freeman Mbowe ataendelea kuongoza Chadema walau miaka 15 mingine ijayo.
 
Ohooooo...good, ukweli ni kwamba wapinzani wa chadema hawatakosa propaganda. Na kwa bahati mbaya ni propaganda zinazoenda mbali ya utanzania na za kujitoa ufahamu...tumeruka viunzi....kilichokuwa kikubwa ni kile cha u-ghaidi (bahati nzuri washiriki wa ughaidi huu kutokea ccm wameisha tubu).

Kuwa chdema ingekufa.....ulikuwa mpango kamambe ukimhusisha zzk ( ili halina ubishi tena). Salary slip ungana nami kukemea usaliti wa huu mbaya kutokea uliofanywa na zzk dhidi ya chama kilichomlea).
Ni kweli ndugu yangu ila tambua kuna propaganda za msimu na propaganda zinazoishi.

Propanga za msimu hutokomea zenyewe ila propaganda zinazoishi tunazilea wenyewe na ndio mbaya zaidi.

Waliobuni propaganda hawakuwa wajinga bali walijua wanafanya nini.

Hata mapungufu madogomadogo kama haya ya kikatiba yanaweza kugeuzwa propaganda au kuwa msingi wa uzushi wa propaganda fulani fulani
 
Back
Top Bottom