Mambo matatu ya kurekebisha ndani ya CHADEMA

Mambo matatu ya kurekebisha ndani ya CHADEMA

Popote Nchini tanzania kuna wakala au office ya chama hata unge google ungepata mawasiliano ya chama Hata ungetu pm tungekupa utaratibu wakuwasilisha Mawazo yako yangepokelewa na muhusika

Chadema Kwanza

Mlishafanyia kazi mawazo Mangapi mlokwisha pewa?

Chadema kwanza my Foot.
 
Ukomo wa uongozi ni sanduku la kura ndugu.usichecheze muziki walioimba CCM.hata mbowe akiwa mwenyekiti kwa miaka 20 mradi anashinda kwenye sanduku la kura hiyo ndio democracia yenye mipaka
 
Ukomo wa uongozi ni sanduku la kura ndugu.usichecheze muziki walioimba CCM.hata mbowe akiwa mwenyekiti kwa miaka 20 mradi anashinda kwenye sanduku la kura hiyo ndio democracia yenye mipaka
Ukiona wanahaha hivyo jua Mbowe nikiboko kibaya sana kwa ccm na michepuko yao
 
Naona umejivua mahaba na kuamua kutumia kipaji ulichojaliwa na Mungu ili kuwakumbusha wenzako mambo muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa.

Watu hawataki lakini suala la uchagga/ukasikazini, iwe propaganda ama kweli, linakiumiza CHADEMA.

Nakwambia penye ukweli hupewa nguvu japo huchelewa
 
Ukomo wa uongozi ni sanduku la kura ndugu.usichecheze muziki walioimba CCM.hata mbowe akiwa mwenyekiti kwa miaka 20 mradi anashinda kwenye sanduku la kura hiyo ndio democracia yenye mipaka
Mawazo kama haya yanasaidi CCM kupata cha ongea na kamwe hayajengi wala hayasaidii chama.
 
Umejiuliza ni watanzania wangapi wenye uelewa kama wako?

Ni wangapi wenye uwezo wa kuchambua pumba na mchele?

....
Kama kweli ni mwanademokrasia na unaamini katika demomkrasia , Propaganda za Kishenzi/Na kishetani (hasa ukabila, rangi n.k) haziwezi kukutisha. Unachotakiwa kufanya ni kutafuta chanzo cha kwa nini watu hawaelewi sera za chama chako na wanaamini propaganda!

Chakufanya nikuwaelemisha kwa lugha wanayoifahamu kwa kudhibiditisha kuwa propaganda hiyo kutoka kwa kundi lingine inalenga kupotosha msingi wa chama. Na ufafanue huo msingi wa chama mpaka hao unaosema hawana uwelewa wanaelewa. Kikubwa ni ku-walk the talk.

Jukumu hapa ni kuendelea kufanya kazi kwa malengo yale yale ya kuboresha maisha ya watanzania na waafrika kwa ujumla kwa misingi ya kidemokrasia na maendeleo huku tukiimiza kujitegemea ki-uchumi katika kuendesha maisha yetu. Tusije tukafanya kosa la kuongozwa na propaganda za vyama 'hasi' katika maamuzi ya msingi katika uendeshaji wa vyama vyetu.

Dawa ya propaganda ni kuonyesha msingi wa propaganda hiyo uko wapi na tumia msingi huo wa propaganda kumuelewesha yule anayelazimishwa kuamini huyo propaganda athari za anachotaka kuamini.
 
Mapendekezo yako ni mazuri lakini mimi nakushauri yapeleke kwenye vikao vya chama, anzia ngazi ya chini kabisa, watakusikiliza tu usiwe na hofu, hapa JF ni kama umbeya tu wa akina Zitto et al.

Hivi zitto kawaingia akilini kupindukia et? maana taarifa atoe mwingine zitto anakujaje! kaisha waaga achaneninae
 
Napenda kuwashauri CHADEMA watekeleze mambo matatu yafuatayo ili kuondoa propaganda chafu zinazosambazwa na CCM na ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa chama chetu.

Wana-CHADEMA,tunapaswa kutambua kuwa watu tunatofautiana katika uelewa wa mambo na katika mapokeo ya taarifa tunazoletewa au kuzisoma.

Kwa maana hiyo basi,mambo haya nashauri yatazamwe upya.
1.Ukomo wa kugombe uongozi urudishwe katika katiba ya chama na ikiwezekano ukomo uwe ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano.

2.Wanachama waruhusiwe kwenda mahakamni na mtu akishindwa kesi aruhusiwe kuendelea na uanachama wake.

3.Mh.Mbowe,kipindi chako cha sasa kikiisha,nakushauri usigombee tena na utoe fursa kwa wengine kugombea na wewe kama kiongozi, ujikite katika kuhakikisha chama kinapata mrithi bora,wa kuamimika na mwenye viwango.

Mchango ndani wako ndani ya chama ni mkubwa na wa kuthaminiwa sana ila ni vizuri sasa ukatoa nafasi kwa wengine ili kukinusuru chama na propaganda hizi.

4.Japo hatuchagu kiongozi kwa kuangalia kabila lake, lakini ikiwezekana katika uchaguzi wa mwenyekiti ajae jambo hili likaangaliwa kwa mapana na marefu yake.

Wenye akili na upeo wa kuona mbali watanielewa, ila wenye kukariri kuwa chama hakihitaji ushauri wa aina hii, watakuja hapa na vijembe na kejeli.

Niwaambie tu,hata kiburi na kujiamini kwa Zitto msingi wake ni uwepo wa hizi propaganda na ndio maana hata anapata public sympathy kutoka kwa baadhi ya watu na watu hao ni wengi tu huku mitaani tunakoishi.Fanya utafiti mdogo uone.

Propaganda zingine ni za msimu tu lakini sio hizi nilizoziongelea hapa.

Yangu ni hayo tu.

Waambie CCM waliokutuma watafute mbinu nyingine
 
Last edited by a moderator:
Don't allow others to set the agenda for you. We must continue to put them on the defense. We must not take instructions from them. Yaani unashauri tumwachishe Mbowe kugombea tena uenyekiti kwa sababu tu za kikabila?

It is not possible to be a little bit pregnant. Aidha CDM ina principles always au haina at all.

Nimempuuza sana huyu Salary Slip hana lolote bali ni kisemeo cha CCM

Alijificha sana leo kajianika
 
Last edited by a moderator:
Napenda kuwashauri CHADEMA watekeleze mambo matatu yafuatayo ili kuondoa propaganda chafu zinazosambazwa na CCM na ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa chama chetu.

Wana-CHADEMA,tunapaswa kutambua kuwa watu tunatofautiana katika uelewa wa mambo na katika mapokeo ya taarifa tunazoletewa au kuzisoma.

Kwa maana hiyo basi,mambo haya nashauri yatazamwe upya.
1.Ukomo wa kugombe uongozi urudishwe katika katiba ya chama na ikiwezekano ukomo uwe ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano.

2.Wanachama waruhusiwe kwenda mahakamni na mtu akishindwa kesi aruhusiwe kuendelea na uanachama wake.

3.Mh.Mbowe,kipindi chako cha sasa kikiisha,nakushauri usigombee tena na utoe fursa kwa wengine kugombea na wewe kama kiongozi, ujikite katika kuhakikisha chama kinapata mrithi bora,wa kuamimika na mwenye viwango.

Mchango ndani wako ndani ya chama ni mkubwa na wa kuthaminiwa sana ila ni vizuri sasa ukatoa nafasi kwa wengine ili kukinusuru chama na propaganda hizi.

4.Japo hatuchagu kiongozi kwa kuangalia kabila lake, lakini ikiwezekana katika uchaguzi wa mwenyekiti ajae jambo hili likaangaliwa kwa mapana na marefu yake.

Wenye akili na upeo wa kuona mbali watanielewa, ila wenye kukariri kuwa chama hakihitaji ushauri wa aina hii, watakuja hapa na vijembe na kejeli.

Niwaambie tu,hata kiburi na kujiamini kwa Zitto msingi wake ni uwepo wa hizi propaganda na ndio maana hata anapata public sympathy kutoka kwa baadhi ya watu na watu hao ni wengi tu huku mitaani tunakoishi.Fanya utafiti mdogo uone.

Propaganda zingine ni za msimu tu lakini sio hizi nilizoziongelea hapa.

Yangu ni hayo tu.

Salary Slip sikubaliani nawe kwenye mengi lakin nikiri kuwa upo tofauti na wenzako wengi humu kwa sababu pamoja na kushabikia lakini pia unalenga kurekebisha.Hii ni njia sahihi. Maana wengine wakipenda uwa hawawezi kuona kasoro, wao ni ndio, ni sahihi, ni hakuna mapungufu mwanzo mwisho.

Hongera kwa mtazamo wako wa kurekebisha.Chadema inawahitaji watu kama wewe ili isonge mbele.
 
Last edited by a moderator:
Hoja zako ni za msingi zina faida Kubwa sana kwa CHADEMA lakini hapa ulipowasilisha sidhani kama sehemu muhusika
.
 
Haya mambo tunayapuuza lakini ukweli ni kuwa yanatuathiri katika harakati za kuleta mageuzi nchi hii.

Hakuna propaganda nyingine zinazoweza kutusumbua zaidi ya hizi nilizotaja.

Tusiwe rigid badala yake tuwe flexible kama kweli tunataka kushika dola.

Kufanya mabadiliko hayo kuna ugumu gani?

Tambua kuwa wewe unaona hizi propaganda ni upuuzi kwasababu tu wewe ni muelewa ila u anasahau kuwa watu wote sio waelewa.
Nadhani unaangalia upande mmoja tu wakuwalizisha magamba. Hujaangalia kitu muhimu sana ambacho inteligence ya chama ndo inachokifanya. Hivi unajua risk ya mtu yeyote kuwa mwenyekiti wa chadema? Siyo kila unayemwona ni mwanachama wa chadema anafaa kuwa kuwa kiongozi wa ngazi ya juu. Fatilia vyama au taasisi zote makini hata kama kiongozi atapigiwa kura bado watakao kuwa shortlisted ni wale kweli yoyote kati yao akichaguliwa chama kitakuwa salama. Kitu cha msingi ni usalama wa chama kwanza demokrasia inakuja juu yake.

Huwezi kukiweka chama mikononi mwa mtu ambaye inteligensia ya chama haimwamini mtu huyo. Zitto kwa mwenendo wake kisiasa hata ccm hawawezi kumpa nafasi yoyote hata akihamia leo. Hawezi kuamimika na hilo ndilo tatizo la Zitto. Zitto naweza kuongoza chama ambacho kila kitu ni yeye na si chama ambacho no taasisi. Zitto hutumia kila jukwaa la aina yoyote kujenga maisha binafsi.

Kwa kifupi ukiangalia usalama wa chama zaidi huwezi kufanya haya unayoyapendekeza ili kuwafutahisha maadui. Hayo yanaweza kufanyika kwenye chama kikubwa na kilichoko madarakani hamna risk ya usalama wa chama kwenye upinzani ukifanya haya safari ya chama itaishia njiani!
 
Umejiuliza ni watanzania wangapi wenye uelewa kama wako?

Ni wangapi wenye uwezo wa kuchambua pumba na mchele?

Mtu asie na uwezo wa ku-reason akitajiwa alianza Mtei akafuaya Bob Makani na sasa Mbowe wote wakiwa ni wachaga ni rahisi sana kuamini hizo propaganda.

Tusiotoe mwanya wa watu kutengeneza propaganda.

Watanzania wengi hawaelewi chochote... Erka bendi au bongo fleva, gawa ubwabwa khanga na kofia utapata utakacho

We are just ignorant
 
Kwa hapa Tanzania makabila yenye uwezo wa kuendesha vyama vya upinzani na kupata mafanikio ni haya Chagga,Meru,Iraq/Mbulu,Kyusa,Kurya basi.Wengine wote maneno tu.Chadema bado inajengwa sasa unataka wasaliti waje kuongoza Chadema?

Salary Slip...waangalie wabaguzi hawa.Wanaamini watu wasio wa makabila hayo ni WASALITI.

Tuna safari ndefu sana kama taifa.
 
Salary Slip :

1. Are you suggesting kwamba vyama vingine vina Kanuni ya kuzuia Wachagga kugombea uongozi katika chama ili visiitwe vyama vya Wachagga? Sijawahi kusikia Mchaga yeyote kuwa kiongozi wa CCM katika ngazi ya taifa. Labda miaka ya nyuma kabla ya 1992.

2. Vyama vingine vinaruhusu wanachama kupeleka mahakamani mashauri ambayo yamewekewa utaratibu wa kuyatatua katika chama? Je ukiwa mwanachama wa CCM, unaweza kumshitaki Katibu Mkuu wa CCM mahakamani kwa masuala yanayohusu maamuzi halali ya chama? I know pretty well that two wrongs do not make a right. Lakini natizama jambo hili kupitia ushauri ulioutoa wa namna ya kujihami na propaganda. Je ni kwanini Katiba ya Chama au asasi yoyote ile ikataze wanachama kupeleka masuala ya chama mahakamani?
 
Mapendekezo yako ni mazuri lakini mimi nakushauri yapeleke kwenye vikao vya chama, anzia ngazi ya chini kabisa, watakusikiliza tu usiwe na hofu, hapa JF ni kama umbeya tu wa akina Zitto et al.

Unafikiri akianzia huko yatafika?atavuliwa uanachama mara moja.Hapa ni sehemu nzuri kuanza kujenga mtazamo ambao Mbowe mwenyewe na viongzoi wenzake wakiamua watatekeleza au kupotezea.Ila kuanzia kwenye tawi huko my friend, utasikia tu siku anavyofukuzwa uanachama.
 
Huyu chadema kwanza, sijui chagga kwanza kwasababu humu ndani hatuonani kwa sura atakuwa akili hamna kabisa. Wewe mtu anatoa mawazo unasema humu akufai, unataka akatoe ufipa halafu mumtese kama kangezi.
 
Back
Top Bottom