Chademakwanza
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 6,346
- 1,872
Tutajua rangi nyingi kwa watu wanaojita makamandaSalary Slip...waangalie wabaguzi hawa.Wanaamini watu wasio wa makabila hayo ni WASALITI.
Tuna safari ndefu sana kama taifa.
Tutajua rangi nyingi kwa watu wanaojita makamandaSalary Slip...waangalie wabaguzi hawa.Wanaamini watu wasio wa makabila hayo ni WASALITI.
Tuna safari ndefu sana kama taifa.
Mbona salary slip kaliweka vizuri jambo hili, hajasema katiba ivunjwe. Amesema iangaliwe ili kuondoa huo unaoonekana ni ukakasi.
Hivi kusema kuwe na ukomo wa uongozi hasa uenyekiti ni dhambi? Kusema mtu aruhusiwe kwenda mahakamani kutafuta haki na hata akishindwa arudishwe kwa kuwa haki itakuwa imetendeka, basi hilo ni dhambi?
Kwamba makabila mengine nayo yapewe nafasi ndani ya chama, ni dhambi?
Contents za hiyo aya ya kwanza inatoa tafsri potufu kuwa chama hakina rasilimali watu wa kufaa kwa nafasi ya mwenyekiti zaidi ya Mbowe.Nadhani unaangalia upande mmoja tu wakuwalizisha magamba. Hujaangalia kitu muhimu sana ambacho inteligence ya chama ndo inachokifanya. Hivi unajua risk ya mtu yeyote kuwa mwenyekiti wa chadema? Siyo kila unayemwona ni mwanachama wa chadema anafaa kuwa kuwa kiongozi wa ngazi ya juu. Fatilia vyama au taasisi zote makini hata kama kiongozi atapigiwa kura bado watakao kuwa shortlisted ni wale kweli yoyote kati yao akichaguliwa chama kitakuwa salama. Kitu cha msingi ni usalama wa chama kwanza demokrasia inakuja juu yake.
Huwezi kukiweka chama mikononi mwa mtu ambaye inteligensia ya chama haimwamini mtu huyo. Zitto kwa mwenendo wake kisiasa hata ccm hawawezi kumpa nafasi yoyote hata akihamia leo. Hawezi kuamimika na hilo ndilo tatizo la Zitto. Zitto naweza kuongoza chama ambacho kila kitu ni yeye na si chama ambacho no taasisi. Zitto hutumia kila jukwaa la aina yoyote kujenga maisha binafsi.
Kwa kifupi ukiangalia usalama wa chama zaidi huwezi kufanya haya unayoyapendekeza ili kuwafutahisha maadui. Hayo yanaweza kufanyika kwenye chama kikubwa na kilichoko madarakani hamna risk ya usalama wa chama kwenye upinzani ukifanya haya safari ya chama itaishia njiani!
Leo salary slip amekuwa mtu wa CCM?Chadema haiwezi kushauriwa na watu wa CCM
Salary Slip kama ulikuwa bado hujafahamu watu ulionao ni wa aina gani.Leo atleast utatambua.Tayari umekuwa msaliti.Ningekuwa na fursa ya kuingia kwenye vikao vya chama haya ningeyaseme huko huko ila bahati mbaya sina nafasi hiyo.
Weka wazo lako mbadala hapa kunikosoa au kuboresha na si kujitia upofu kuwa kila kitu always ni sahihi.
Saidieni viongozi kwa kutoa mawazo mbadala
na si kusubiri ya viongozi tu kila siku.
Kumbuka kuna kitu kinaitwa "constructive criticism" na tuitumie inapobidi na tusiwe blind follower tu.
Hivi wewe unafikiri watanzania wanaohongwa kanga na vitenge wana uelewa kama wako?
Kuna ugumu gani wa kufanya hayo mabadiliko?
Tusitoe mwanya wa propaganda kwa mambo ambayo si ya lazima na yanayoweza kuepukika.
Salary Slip unapoteza muda kushauri yasiyowezekana tena.
Wewe unaonekana kupenda mabadiliko ndani ya chama lkn kiukweli hayo unayoyapinga ndio yalimuua Chacha Wangwe na yaliwaondoa wapiganaji kama Shinza,Mchange,Mwampamba,Mwigamba ,Kitila na hatimae Zitto.
Huo utaratibu wa chama unaoukosoa haukuwekwa kwa bahati Mbaya bali uliwekwa kimkakati.
Ni utaratibu unaolinda tabaka flani kuhidhi chama na rasilimali zaje na kamwe chama hakiwezi kutoka nje ya familia uliyoitaja.
Ukijifanya Mdadisi watakubambika isaliti na utaambiwa wewe unatumiwa na ccm ili kubatilisha hoja zako.
Chadema kwa sasa ilipofika ni sawa na ccm,hawapo tayari kubadulika hivyo dawa ni kuhama vyama hivyo na kujiunga navile vinavyokubali challenge.
NCCR Mageuzi, TLP, CUF. labda ulikuwa bado ujaanza kufuatilia siasa.
soma ushauri wa respect wa boda utaelewa vizuri.amejenga hoja zake vizuri.kikubwa,propaganda haziepukiki na mwisho wa propaganda moja,ni mwanzo wa propaganda nyingine.napenda kuwashauri chadema watekeleze mambo matatu yafuatayo ili kuondoa propaganda chafu zinazosambazwa na ccm na ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa chama chetu.
Wana-chadema,tunapaswa kutambua kuwa watu tunatofautiana katika uelewa wa mambo na katika mapokeo ya taarifa tunazoletewa au kuzisoma.
Kwa maana hiyo basi,mambo haya nashauri yatazamwe upya.
1.ukomo wa kugombe uongozi urudishwe katika katiba ya chama na ikiwezekano ukomo uwe ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano.
2.wanachama waruhusiwe kwenda mahakamni na mtu akishindwa kesi aruhusiwe kuendelea na uanachama wake.
3.mh.mbowe,kipindi chako cha sasa kikiisha,nakushauri usigombee tena na utoe fursa kwa wengine kugombea na wewe kama kiongozi, ujikite katika kuhakikisha chama kinapata mrithi bora,wa kuamimika na mwenye viwango.
Mchango ndani wako ndani ya chama ni mkubwa na wa kuthaminiwa sana ila ni vizuri sasa ukatoa nafasi kwa wengine ili kukinusuru chama na propaganda hizi.
4.japo hatuchagu kiongozi kwa kuangalia kabila lake, lakini ikiwezekana katika uchaguzi wa mwenyekiti ajae jambo hili likaangaliwa kwa mapana na marefu yake.
Wenye akili na upeo wa kuona mbali watanielewa, ila wenye kukariri kuwa chama hakihitaji ushauri wa aina hii, watakuja hapa na vijembe na kejeli.
Niwaambie tu,hata kiburi na kujiamini kwa zitto msingi wake ni uwepo wa hizi propaganda na ndio maana hata anapata public sympathy kutoka kwa baadhi ya watu na watu hao ni wengi tu huku mitaani tunakoishi.fanya utafiti mdogo uone.
Propaganda zingine ni za msimu tu lakini sio hizi nilizoziongelea hapa.
Yangu ni hayo tu.
Leo salary slip amekuwa mtu wa CCM?
Ndicho alichokuwa hajakijua Salary Slip.Sote tulikuwa huko na ukitaka uwe na mawazo huru Chadema hasa kuchallenge kuondoka uhodhi wa chama uliopo pale, ni msaliti na utaondoka tu.
Chadema ina wenyewe.Na wenyewe ndio hao.
Salary Slip kama ulikuwa bado hujafahamu watu ulionao ni wa aina gani.Leo atleast utatambua.Tayari umekuwa msaliti.
Hilo neno usaliti ndani ya Chadema linatumika vibaya sana.
Salary Slip leo naona unakumbana na mihemko ya wanachadema ambao hawataki kusikia hata siku moja wakikosolewa, iwe kwenye vikao ama nje ya vikao. Ona sasa sikutegemea mtu kama wewe ambaye umetoa mawazo mazuri lakini umeanza kushambuliwa.
Haya mambo tunayapuuza lakini ukweli ni kuwa yanatuathiri katika harakati za kuleta mageuzi nchi hii.
Hakuna propaganda nyingine zinazoweza kutusumbua zaidi ya hizi nilizotaja.
Tusiwe rigid badala yake tuwe flexible kama kweli tunataka kushika dola.
Kufanya mabadiliko hayo kuna ugumu gani?
Tambua kuwa wewe unaona hizi propaganda ni upuuzi kwasababu tu wewe ni muelewa ila u anasahau kuwa watu wote sio waelewa.
Hata Ben Saanane aliitwa msaliti na huyu kijana wa Mbowe CHADEMA KWANZA..sasa ni zami ya Salaryslip
Huwezi kua mwana chadema ukaandika huu ujinga alioandika Salary SlipMkuu Salary Slip
Heshima Kwako, Hizo Propaganda Hapa ndani zinaletwa na kushabikiwa na Ma CCM,
Fanya uchunguzi