Arnold Ringo
JF-Expert Member
- Jan 23, 2014
- 2,318
- 394
Kamanda Nakumbuka yale maneno ya Kamanda Chademakwanza watu walimshambulia huku ndani lakini nayaona yalikua na maana kubwa sana maana rangi za watu zinaanza kuonekanaSikuwahi kufikiri mwanachadema anaweza kuathirika kwa propaganda zinazotengezwa mtaa wa Lumumba.
Mkuu Salary Slip hatuendi hivyo hata siku moja, Huwezi kucheza ngoma inayopigwa na mpizani. wako na kufuatisha midundo yake na mirindimo yake huku ukipiga mruzi na macho umeyafumba huku ukidhani eti unapambana naye... Hakika utatumbukia shimoni..!!! Hiyo unayodai tuifuate ni Demokrasia ya woga na ni ubaguzi wa waziwazi usio na kificho ambao katu sikudhani unaweza kukukumba mtu kama wewe.. Inashangaza kwa kweli..!!!!
Tambua mwisho wa Propaganda hii ndio mwanzo wa Propaganda nyingine.. Kamwe kwenye siasa propaganda si kitu cha kukikwepa kwa kufuata namna mpiga propaganda anavyoieneza (Umeamkia wapi leo mkuu?) Hapa ilipo. Chadema imepigwa propaganda kadha wa kadha na za hatari kuliko hizo unazodai eti tuzitende ili kuepukana nazo...!!! Mpaka wapiga propaganda wenyewe ilifikia kipindi wakajiaminisha sasa Chadema INAKUFA..!! Naam walijiaminisha kwamba itakufa kabla ya mwaka 2013 lakini je iko wapi??
Chadema ilidaiwa ni chama cha kikristo (Propaganda hii imewaathiri sana cuf mpka leo) IKAPITA SALAMA..
Chadema ilidaiwa ni chama cha Ukanda wa kaskazini... IKAPITA. SALAMA...
Kama vile haitoshi Chadema ilidaiwa ni chama cha Kigaidi...IKAPITA SALAMA.....!!!!!
Kumbuka propaganda zote hizo kila zinapoibuliwa na wapigaji zinakuwa na matukio kadha wa kadha ya kuisindikiza ili iweze kukubaliwa na wasikilizaji (wananchi) kamwe haivumishwi hivi hivi. Watakudanganyaje kwamba hiki ni chama cha Kigaidi?? Naam hapo watawakamata viongozi kadahaa wa chama na kuwahusisha na matukio hayo... Hapa wenye akili fupi watakubaliana na wapigaji..!!
Kuna watu huwa wanadai chama hiki ni Mpango wa Mungu..... Naam si bure ni kutokana na kuluka vihunzi,Mashimo,Makorongo na kila aina ya Mitego na mpaka tunavyoongea hapa mimi na wewe na wewe kuja na Mada yako hii ni kwamba Chadema ndicho chama kinachoshika nafasi ya pili kwa kuwa na wenyeviti wengi wa Mitaa kiliko chama chochote hapa Tanzina...!!! (Na hii ni baada ya kuungana na vyama vingine vinavyounda UKAWA pamoja na uchakachuaji mkubwa tuliouona ktk uchaguzi huo)
Kwa maoni yangu mimi ningesema.....
HAPO ILIPOSHIKA (CHADEMA) KATU ISIACHIE IENDELEE KUKAZA ZAIDI.
BACK TANGANYIKA
Last edited by a moderator: