Mambo matatu ya kurekebisha ndani ya CHADEMA


Chadema haiwezi kushauriwa na watu wa CCM
 
Nimempuuza sana huyu Salary Slip hana lolote bali ni kisemeo cha CCM

Alijificha sana leo kajianika

Unajua Kamanda Greenwhich kuna watu nilikua nawaheshimu sana kama salary slip lakini nimemweka kwenye kundi lile lile kamanda wangu
 
Last edited by a moderator:
Contents za hiyo aya ya kwanza inatoa tafsri potufu kuwa chama hakina rasilimali watu wa kufaa kwa nafasi ya mwenyekiti zaidi ya Mbowe.

Acha kuwapa watu faida kwa kutoa mawazo ya aina hiyo.
 
Salary Slip kama ulikuwa bado hujafahamu watu ulionao ni wa aina gani.Leo atleast utatambua.Tayari umekuwa msaliti.

Hilo neno usaliti ndani ya Chadema linatumika vibaya sana.
 
Hivi wewe unafikiri watanzania wanaohongwa kanga na vitenge wana uelewa kama wako?

Kuna ugumu gani wa kufanya hayo mabadiliko?

Tusitoe mwanya wa propaganda kwa mambo ambayo si ya lazima na yanayoweza kuepukika.

Salary Slip unapoteza muda kushauri yasiyowezekana tena.

Wewe unaonekana kupenda mabadiliko ndani ya chama lkn kiukweli hayo unayoyapinga ndio yalimuua Chacha Wangwe na yaliwaondoa wapiganaji kama Shinza,Mchange,Mwampamba,Mwigamba ,Kitila na hatimae Zitto.

Huo utaratibu wa chama unaoukosoa haukuwekwa kwa bahati Mbaya bali uliwekwa kimkakati.
Ni utaratibu unaolinda tabaka flani kuhidhi chama na rasilimali zaje na kamwe chama hakiwezi kutoka nje ya familia uliyoitaja.

Ukijifanya Mdadisi watakubambika isaliti na utaambiwa wewe unatumiwa na ccm ili kubatilisha hoja zako.

Chadema kwa sasa ilipofika ni sawa na ccm,hawapo tayari kubadulika hivyo dawa ni kuhama vyama hivyo na kujiunga navile vinavyokubali challenge.
 

Ndicho alichokuwa hajakijua Salary Slip.Sote tulikuwa huko na ukitaka uwe na mawazo huru Chadema hasa kuchallenge kuondoka uhodhi wa chama uliopo pale, ni msaliti na utaondoka tu.

Chadema ina wenyewe.Na wenyewe ndio hao.
 
Chadema wamekiua kwa makusudi,kuna haja ya kuwatazama usalama ambao ni invisible ndani ya chadema,yule alieua NCCR sasa ana mission chadema ,pia yule kada wa ccm aliekuwa mwenyekiti wa TANU youth league kule Kampala bado alisisitiza kuwa kadi ya ccm ni haki yake hivyo haoni tatizo kubaki nayo.

Hawa ndio wanaua chadema,simnakumbuka kuwa mmoja wao ndiyo alienda mwanza kuzirejesha manispaa za Ilemela na Nyamagana ambazo awali ziliongozwa na chadema lkn kwa mapenzi yake kwa ccm akaamua kufukuza madiwani na hatimae zikarudi ccm.

Susi tumeshatangulia mliobaki ndani ya hiyo VICOBA bakini tu sisi tumeshashtuka.
 
soma ushauri wa respect wa boda utaelewa vizuri.amejenga hoja zake vizuri.kikubwa,propaganda haziepukiki na mwisho wa propaganda moja,ni mwanzo wa propaganda nyingine.
 
Ndicho alichokuwa hajakijua Salary Slip.Sote tulikuwa huko na ukitaka uwe na mawazo huru Chadema hasa kuchallenge kuondoka uhodhi wa chama uliopo pale, ni msaliti na utaondoka tu.

Chadema ina wenyewe.Na wenyewe ndio hao.

Nidhamu kwenye chama nimuhimu sana
 
Salary Slip kama ulikuwa bado hujafahamu watu ulionao ni wa aina gani.Leo atleast utatambua.Tayari umekuwa msaliti.

Hilo neno usaliti ndani ya Chadema linatumika vibaya sana.

Hata Ben Saanane aliitwa msaliti na huyu kijana wa Mbowe CHADEMA KWANZA..sasa ni zami ya Salaryslip
 
Last edited by a moderator:
they say: it is very possible for the one who has no power to be very undemocratic once he has that power. so it is very possible kwa chadema kua madikteta once they assume our highest office in the country.
 
Salary Slip leo naona unakumbana na mihemko ya wanachadema ambao hawataki kusikia hata siku moja wakikosolewa, iwe kwenye vikao ama nje ya vikao. Ona sasa sikutegemea mtu kama wewe ambaye umetoa mawazo mazuri lakini umeanza kushambuliwa.

Mkuu, Hayo Mawazo ni Mazuri kwa CCM, CHADEMA hatuyataki, yachukueni basi mkaya implement
 


Mkuu Salary Slip

Heshima Kwako, Hizo Propaganda Hapa ndani zinaletwa na kushabikiwa na Ma CCM,
Fanya uchunguzi
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…