Mambo matatu ya kurekebisha ndani ya CHADEMA

Kumbe JF ni sehemu ya propaganda tu? mimi nilidhani JF ni mahala pa kupeana mawazo kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu kumbe siyo. Hapa ni propaganda tu kama wenzetu wa Yanga walivyoambiwa bishana hadi ufe hata kama unaujua ukweli. ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA VIONGOZI WA JUU WA CHAMA.
Katiba ya chama haijataja kuwa Jf ndio sehemu yakusemea matatizo au dukuduku la Mwanachama

Chadema Kwanza
 
Hatuwezi kupewa ushauri na fisi tukaufuata tukaacha kusimamia katiba namisingi yake

Chadema Kwanza
Mbona salary slip kaliweka vizuri jambo hili, hajasema katiba ivunjwe. Amesema iangaliwe ili kuondoa huo unaoonekana ni ukakasi.

Hivi kusema kuwe na ukomo wa uongozi hasa uenyekiti ni dhambi? Kusema mtu aruhusiwe kwenda mahakamani kutafuta haki na hata akishindwa arudishwe kwa kuwa haki itakuwa imetendeka, basi hilo ni dhambi?

Kwamba makabila mengine nayo yapewe nafasi ndani ya chama, ni dhambi?
 
Umejiuliza ni watanzania wangapi wenye uelewa kama wako?

Ni wangapi wenye uwezo wa kuchambua pumba na mchele?

Mtu asie na uwezo wa ku-reason akitajiwa alianza Mtei akafuaya Bob Makani na sasa Mbowe wote wakiwa ni wachaga ni rahisi sana kuamini hizo propaganda.

Tusiotoe mwanya wa watu kutengeneza propaganda.

Mkuu hizo sio propaganda huo ndio ukweli, Na hicho ndio kichomponza Zitto pale alipotia nia ya kugombea uenyekiti na akataka kuirekebisha hali hiyo.
 
chikutentema kwa hiyo unataka kusema CHADEMA ni kusanyiko la wasaliti? Hakuna wa kumuamini mwenzake, mnatizamana kwa tahadhari kubwa? Waacheni wenzenu watoe mawazo yao.

Kwa sasa kuna kifungu ndani ya katiba ambacho kinazuia wanachama kwenda mahakamani na huko tunakoelekea itkuwa ni mrufuku kutoa mawazo ambayo ni kinyume na mawazo ya viongozi: ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI!

Kama ninyi hamshirikiani kwa tahadhari basi hatushangai siri zenu (serikali na chama kuvuja), pia kifungu hicho mbona hata katiba yenu inacho kama mmetoa nambie, jikiteni ktk Jurisprudence mjue why katiba za vyama na vilabu huweka kipengele hicho ulomwenguni.
 
Last edited by a moderator:
Chacha Wangwe aliliona hilo alipojaribu kutaka kulirekebisha kilichompata R.I.P.
Zitto aliliona hilo alipotaka kulirekebisha aliitwa msaliti.
Mnakumbuka shuka wakati kumrkucha.
Mnafunga banda wakat Farasi kesha toka.

Zitto ni mpango wa mngu katka siasa zs Tanzania.
 
Mbona salary slip kaliweka vizuri jambo hili, hajasema katiba ivunjwe. Amesema iangaliwe ili kuondoa huo unaoonekana ni ukakasi.

Hivi kusema kuwe na ukomo wa uongozi hasa uenyekiti ni dhambi? Kusema mtu aruhusiwe kwenda mahakamani kutafuta haki na hata akishindwa arudishwe kwa kuwa haki itakuwa imetendeka, basi hilo ni dhambi?

Kwamba makabila mengine nayo yapewe nafasi ndani ya chama, ni dhambi?

Kuangalia kipengele ndio kukivunja huo utaratibu haupo Chadema Asante

Chadema Kwanza
 
Napenda kuwashauri CHADEMA watekeleze mambo matatu yafuatayo ili kuondoa propaganda chafu zinazosamhuubazwa na CCM na ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa chama chetu.

Wana-CHADEMA,tunapaswa kutambua kuwa watu tunatofautiana katika uelewa wa mambo na katika mapokeo ya taarifa tunazoletewa au kuzisoma.

Kwa maana hiyo basi,mambo haya nashauri yatazamwe upya.
1.Ukomo wa kugombe uongozi urudishwe katika katiba ya chama na ikiwezekano ukomo uwe ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano.

2.Wanachama waruhusiwe kwenda mahakamni na mtu akishindwa kesi aruhusiwe kuendelea na uanachama wake.

3.Mh.Mbowe,kipindi chako cha sasa kikiisha,nakushauri usigombee tena na utoe fursa kwa wengine kugombea na wewe kama kiongozi, ujikite katika kuhakikisha chama kinapata mrithi bora,wa kuamimika na mwenye viwango.

Mchango ndani wako ndani ya chama ni mkubwa na wa kuthaminiwa sana ila ni vizuri sasa ukatoa nafasi kwa wengine ili kukinusuru chama na propaganda hizi.

4.Japo hatuchagu kiongozi kwa kuangalia kabila lake, lakini ikiwezekana katika uchaguzi wa mwenyekiti ajae jambo hili likaangaliwa kwa mapana na marefu yake.

Wenye akili na upeo wa kuona mbali watanielewa, ila wenye kukariri kuwa chama hakihitaji ushauri wa aina hii, watakuja hapa na vijembe na kejeli.

Niwaambie tu,hata kiburi na kujiamini kwa Zitto msingi wake ni uwepo wa hizi propaganda na ndio maana hata anapata public sympathy kutoka kwa baadhi ya watu na watu hao ni wengi tu huku mitaani tunakoishi.Fanya utafiti mdogo uone.

Propaganda zingine ni za msimu tu lakini sio hizi nilizoziongelea hapa.

Yangu ni hayo tu.

Salary slip hili angalizo lako limekaa vyema sana. Na mimi nashauri hizi nafasi zote za kuchaguliwa na wananchi kama udiwani, ubunge nk ziwe na ukomo na mwisho iwe miaka kumi na tano. Uenyekiti wa chama mwisho iwe miaka 10. Ila vigezo vya uongozi viwe uwajibikaji na sio jinsia, kabila au umri.
 
Last edited by a moderator:
Napenda kuwashauri CHADEMA watekeleze mambo matatu yafuatayo ili kuondoa propaganda chafu zinazosambazwa na CCM na ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa chama chetu.

Wana-CHADEMA,tunapaswa kutambua kuwa watu tunatofautiana katika uelewa wa mambo na katika mapokeo ya taarifa tunazoletewa au kuzisoma.

Kwa maana hiyo basi,mambo haya nashauri yatazamwe upya.
1.Ukomo wa kugombe uongozi urudishwe katika katiba ya chama na ikiwezekano ukomo uwe ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano.

2.Wanachama waruhusiwe kwenda mahakamni na mtu akishindwa kesi aruhusiwe kuendelea na uanachama wake.

3.Mh.Mbowe,kipindi chako cha sasa kikiisha,nakushauri usigombee tena na utoe fursa kwa wengine kugombea na wewe kama kiongozi, ujikite katika kuhakikisha chama kinapata mrithi bora,wa kuamimika na mwenye viwango.

Mchango ndani wako ndani ya chama ni mkubwa na wa kuthaminiwa sana ila ni vizuri sasa ukatoa nafasi kwa wengine ili kukinusuru chama na propaganda hizi.

4.Japo hatuchagu kiongozi kwa kuangalia kabila lake, lakini ikiwezekana katika uchaguzi wa mwenyekiti ajae jambo hili likaangaliwa kwa mapana na marefu yake.

Wenye akili na upeo wa kuona mbali watanielewa, ila wenye kukariri kuwa chama hakihitaji ushauri wa aina hii, watakuja hapa na vijembe na kejeli.

Niwaambie tu,hata kiburi na kujiamini kwa Zitto msingi wake ni uwepo wa hizi propaganda na ndio maana hata anapata public sympathy kutoka kwa baadhi ya watu na watu hao ni wengi tu huku mitaani tunakoishi.Fanya utafiti mdogo uone.

Propaganda zingine ni za msimu tu lakini sio hizi nilizoziongelea hapa.

Yangu ni hayo tu.

CDM ni NGO ya ukanda, ukabila na udini...! Sikipendi hichi ki~NGO cha Kimei na.Mbowe
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hizo sio propaganda huo ndio ukweli, Na hicho ndio kichomponza Zitto pale alipotia nia ya kugombea uenyekiti na akataka kuirekebisha hali hiyo.

Zitto kama muumini wa demokrasia muulize ACT ataenda kupambana na nani kwenye nafasi ya uenyekiti? Muulize pia ilikuwaje binamu yake akapewa ubunge wa viti maalum, ndiomana huwa nasema kupigania neno demokrasia lenye zaidi ya definition 750 ni kazi sana, muhimu ni KUDELETE CCM NA UKOO WOTE WA PANYA.

UKOMBOZI KWANZA DEMOKRASIA BADAE
 
Chacha Wangwe aliliona hilo alipojaribu kutaka kulirekebisha kilichompata R.I.P.
Zitto aliliona hilo alipotaka kulirekebisha aliitwa msaliti.
Huo ndio ujinga mnaojifunzaga hapo Lumumba na Fisi? Kolimba vipi? Kombe vipi?
 
Chacha Wangwe aliliona hilo alipojaribu kutaka kulirekebisha kilichompata R.I.P.
Zitto aliliona hilo alipotaka kulirekebisha aliitwa msaliti.

Chacha Wangwe mwenyewe alisema kuwa yeye akifa kwenye msiba wake Zitto asiende, hujiulizi kwanini mkuu?

UKOMBOZI KWANZA DEMOKRASIA BADAE
 
Salary slip hili angalizo lako limekaa vyema sana. Na mimi nashauri hizi nafasi zote za kuchaguliwa na wananchi kama udiwani, ubunge nk ziwe na ukomo na mwisho iwe miaka kumi na tano. Uenyekiti wa chama mwisho iwe miaka 10. Ila vigezo vya uongozi viwe uwajibikaji na sio jinsia, kabila au umri.

Mawazo ya Katiba ya Chama ndio yamwisho. Asante

Chadema Kwanza
 
Mkuu salary slip,

Naungana nawe ktk hoja zako uko sahihi asilimia mia, ila napingana nawe namna ya uwasilishaji wa hoja zako!! CDM inao utaratibu wake MZURI wa namna ya kuwasilisha maoni na eneo husika, HAPA SIO MAHALI SAHIHI PA KUWASILISHA HOJA ZAKO!!

Salary Slip, nina uhakika uelewa wako ni mkubwa, utatafakari na kunielewa katikati ya mistari. Kwa ufupi hapa unatafta kejeri na vijembe visivyo na msingi!! Otherwise uniambie unayafanyia checkup mawazo yako ili ukayawasilishe!!

Mjadara mwema wakuu.
 
...... Mwenyekiti Anaandaliwa Mnyika, Katibu Mkuu Salum Mwalimu
 
Mkuu hizo sio propaganda huo ndio ukweli, Na hicho ndio kichomponza Zitto pale alipotia nia ya kugombea uenyekiti na akataka kuirekebisha hali hiyo.
Ukishaona Upo sambamba na ccm kimawazo basi jitafakari sana
 
Zitto kama muumini wa demokrasia muulize ACT ataenda kupambana na nani kwenye nafasi ya uenyekiti? Muulize pia ilikuwaje binamu yake akapewa ubunge wa viti maalum, ndiomana huwa nasema kupigania neno demokrasia lenye zaidi ya definition 750 ni kazi sana, muhimu ni KUDELETE CCM NA UKOO WOTE WA PANYA.

UKOMBOZI KWANZA DEMOKRASIA BADAE
Mkuu mimi nachangia kulingania na kile alichokieleza mtoa mada.

Chacha Wangwe mwenyewe alisema kuwa yeye akifa kwenye msiba wake Zitto asiende, hujiulizi kwanini mkuu?

UKOMBOZI KWANZA DEMOKRASIA BADAE

Ni vizuri ungejikita katika mada. Ni kukumbushe tu!

Alianza mzee Mtei,Bobmakni na Sasa Mbowe hii itafanya ionekane kweli ni chama cha Wachaga
 
Back
Top Bottom