Ipo hivi...hiki ni kigezo nilichokosa
Nilikuwa katika mahusiano na nilitegemea tungeoana, kipindi hicho nilikuwa ndiyo nimepata ajira huku nikiwa naishi nyumbani nilikuwa nafanya saving nzuri hasa ukizingatia sikuwa na majukumu makubwa..huku nikijipanga kuanza maisha hasa kujitegemea.
Hapa sasa nikawa na mpenzi tuliyependana sana sikutaka iwe tofauti na tulivyopanga. Mahusiano aliyagundua dada mtu akagoma kuwa mimi sikuwa hadhi ya mdogo wake.
Mwanzo tulipambana kuonesha maneno yao yasingekuwa kitu ila ushirikiano ukaanza kupungua, nikapata mashaka kuna muda simu nikipiga anapokea yeye huku akinipa maneno ya kunikatisha tamaa..wakaungana familia wakagoma nisikanyage kwao maana ni kipindi ambacho nilipanga kuwafahamisha wazazi kisha masuala ya ndoa yaendelee..nikasitisha maana kwao hawakutaka kuniona hapa waliungana wote sasa familia nzima.
Naye alianza kunichukia japo si sana, Nikapanga mbali na nyumbani..maisha yakaendelea huku nikiwa nae mwaka 2017 kazi nikaachisha kiasi cha pesa nikafanya uwekezaji ambao ulinipa hasara kutokana na uzembe wangu kumshirikisha yeye kuwa msimamizi pia.
Hapa nikabaki na kigezo kimoja tu, ukawa mtihani mkubwa kelele za ndugu zake zikiendelea.
Kipindi kilichokuwa kigumu zaidi ni pale tulipokosana muda wa kuombana msamaha na kuzungumza haukupatikana kwa urahisi maana kwao hakuwa na uhuru wa kutoka na kibaya alipoumia alikuwa akilia huku akiwashirikisha ndugu zake ambao hawanipendi hapo walipata nafasi nzuri ya kumlisha maneno.
Baadaye aliolewa na mwanaume aliyechaguliwa na ndugu zake.
Nijambo baya sana mtu anapoonesha kutokupendezwa nawewe huku akijaribu kuyafanya mawazo yake ndiyo yamuendeshe yule uliye na ndoto nae na anayekuone wewe ni sahihi kwake, mwanzo haina tabu ila ikitokea ukakosana nae huku wanampa maneno,
Mfano "umeona, tulikuambia ukawa hautuelewi na hataishia hapa atazidi kukuumiza mpaka ukome". Hapo ukipiga simu hapikei ukituma ujumbe anajibu asiyekupenda.
Nimejaribu kufupisha japo sikupenda kuyaandika haya.