Kabla ujaingia kwenye ndoa weka mambo haya kwanza ili ndoa iwe imara na kudumu

Kabla ujaingia kwenye ndoa weka mambo haya kwanza ili ndoa iwe imara na kudumu

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
561
Reaction score
990
Kabla ujaingia kwenye ndoa fanya mambo haya

Ndoa ni muunganiko kati ya mwanaume na mwanamke kuwa kitu kimoja.

Hii ni Wazo(idea) la Mungu mwenyewe alimpa Adam msaidizi wake hawa na kuwa kitu kimoja hivyo ndoa ni jambo la Mungu.

Mwanzo 2:22
na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.


1.uhusiano na Mungu, kabla ujaingia kwenye ndoa omba Mungu akupatie mtu sahihi ambaye amekuchagulia

ndoa ni ibada unapokuwa na mtu sahihi basi mnaweza kupiga hatua kwenye maisha yenu, ndoa kutoka kwa Mungu inaleta amani, upendo na utulivu katikati yenu.

Kwenye ndoa muwekeni Mungu katikati yenu,
Mungu ni chanzo cha hekima, hivyo mkiwa na Mungu atawasaidia kufanya maamuzi ya hekima pindi mnapo tofautiana kama binadamu,

ndoa azikosi changamoto au matatizo lakini akiwepo Mungu basi mtakuwa na hekima kutatua.

2.Upendo, kabla ujaingia kwenye ndoa tengeneza upendo,
upendo utakusaidia kutengeza bond(muunganiko) imara kati kati yenu, Mtu mwenye upendo ata mjari mwenzie ata kipindi cha changamoto kama tatizo la kukwama kipesa, magonjwa n.k

3.Nidhamu, ndoa ni majukumu ya wote wawili
hivyo ni muhimu wote wawili kuwa na nidhamu ya pesa, muda hivi ni vitu vitasaidia ndoa yenu kuwa na uchumi imara,

uchumi imara utawasaidia kutatua changamoto mbalimbali za kifamilia kama chakula, mavazi, malezi bora kwa familia n.k

4.Heshima, ndoa inajengwa kwa heshima, ukijenga tabia ya kuheshimu kila mtu basi ata kwenye ndoa itakusaidia,

kuheshimu utu wa mwengine, mawazo, n.k vinaweza kujenga ndoa imara, kuto heshimiana kunaweza kuleta migogoro mingi katika ndoa na mwisho kuvunjika.

5.Tabia(character), ndoa inajengwa kwa tabia ni muhimu kujenga tabia bora kabla ujaingia kwenye ndoa,

tabia kama uongozi, usafi, nidhamu, kujali, lugha nzuri, kujituma, ubunifu, maarifa, uwazi n.k
tabia hizi zinamchango mkubwa wa kufanya ndoa kuwa imara na yenye upendo

Mnapokuwa wote mna tabia bora mnafanya pia familia mnayojenga kuwa bora na yenye mafanikio.
 
rastamonkey_podcast_d16c8c0d_1.jpg
 
Kuna watu hivyo vyote walikuwa hawana ila vilijitengeneza vyenyewe.


Kwa sasa wana miaka 17 ndoani unawashauri nini?
 
Hiyo pointi ya uhusiano na Mungu hapo imekaa kimakosa sana.
 
Kuna watu hivyo vyote walikuwa hawana ila vilijitengeneza vyenyewe.


Kwa sasa wana miaka 17 ndoani unawashauri nini?
Waachane warudie process sisi wengine hatukuepo.
 
Ndoa wanaichukulia serious sana ndiyo maana inakuwaga mbilingembilinge

Take kawaida ukivaa nguguvuvi utabaki tabalala
 
Back
Top Bottom