Mambo 5 ambayo wanaume mnaweza kujifunza kutoka kwa wanawake.

Wanaume mnaweza kujifunza kutoka kwetu wanawake.

Tuna mengi ya kuwashirikisha mjifunze kutoka kwetu wanawake, kwa leo nitawapa mambo matano tu...

1. Wape kipaumbele watu wako
Wanaume wengi ni wabinafsi kwa asili na ni wachoyo wenye roho mbaya.
Bali wanawake wengi huweka maslahi ya familia kwanza.

Upendo wa kweli hauna ubinafsi. Watu wakuu wanaishi kwa ajili ya Mungu na wengine.

2. Ombeni msaada
Acheni kutenda kwa nguvu kupita uwezo wenu huku mkiwa na huzuni ndani ya mioyo.

Wanaume wengi wameshuka moyo na ndoa nyingi huvunjika kwa sababu wanaume hawapendi kupata ushauri nasaha.

Kuomba msaada ni ishara ya kuongeza nguvu.

3. Muwe tayari kujifunza.
Mkubali masahihisho. Kupingwa si kudhalilishwa. Kuwa na nia ya kujiboresha kwa kuhudhuria semina za maendeleo ya kibinafsi.

Kufanya hivyo sio udhaifu, bali ni ishara ya nguvu.

4. Fahamu mipaka yako
Acha kujenga matumaini ya uongo kwa wanawake wengine. Acha kuahidi kile ambacho huwezi kutoa. Acha kujituma kupita kiasi katika sehemu yako ya kazi.

Epuka pia uchovu kwa kuwa na muda wa kupumzika mpenzi wako baada ya kazi .

5. Nyenyekea mbele za Mungu
Wewe ni mwanadamu tu. Kiburi na upumbavu huwaweka watu wengi mbali na ibada. Mungu huwainua wanyenyekevu na kuwashusha wenye kiburi. Jinyenyekeze kwa Mungu na mambo yatakuendea vyema.
Hiyo namba moja inaonyesha huna unachokijua.
 
Back
Top Bottom