Mambo 5 ambayo wanaume mnaweza kujifunza kutoka kwa wanawake.

G70

JF-Expert Member
Jul 13, 2022
1,109
2,252
Wanaume mnaweza kujifunza kutoka kwetu wanawake.

Tuna mengi ya kuwashirikisha mjifunze kutoka kwetu wanawake, kwa leo nitawapa mambo matano tu...

1. Wape kipaumbele watu wako
Wanaume wengi ni wabinafsi kwa asili na ni wachoyo wenye roho mbaya.
Bali wanawake wengi huweka maslahi ya familia kwanza.

Upendo wa kweli hauna ubinafsi. Watu wakuu wanaishi kwa ajili ya Mungu na wengine.

2. Ombeni msaada
Acheni kutenda kwa nguvu kupita uwezo wenu huku mkiwa na huzuni ndani ya mioyo.

Wanaume wengi wameshuka moyo na ndoa nyingi huvunjika kwa sababu wanaume hawapendi kupata ushauri nasaha.

Kuomba msaada ni ishara ya kuongeza nguvu.

3. Muwe tayari kujifunza.
Mkubali masahihisho. Kupingwa si kudhalilishwa. Kuwa na nia ya kujiboresha kwa kuhudhuria semina za maendeleo ya kibinafsi.

Kufanya hivyo sio udhaifu, bali ni ishara ya nguvu.

4. Fahamu mipaka yako
Acha kujenga matumaini ya uongo kwa wanawake wengine. Acha kuahidi kile ambacho huwezi kutoa. Acha kujituma kupita kiasi katika sehemu yako ya kazi.

Epuka pia uchovu kwa kuwa na muda wa kupumzika mpenzi wako baada ya kazi .

5. Nyenyekea mbele za Mungu
Wewe ni mwanadamu tu. Kiburi na upumbavu huwaweka watu wengi mbali na ibada. Mungu huwainua wanyenyekevu na kuwashusha wenye kiburi. Jinyenyekeze kwa Mungu na mambo yatakuendea vyema.
 
Wanaume mnaweza kujifunza kutoka kwetu wanawake.

Tuna mengi ya kuwashirikisha mjifunze kutoka kwetu wanawake, kwa leo nitawapa mambo matano tu...
Kuwapa kipaumbele watu wako si ndio uchoyo au
wanawake ndo wachoyo, wanaume tunatoa tu
Upendo wa kweli hauna ubinafsi. Watu wakuu wanaishi kwa ajili ya Mungu na wengine.

2. Ombeni msaada...
kuombaomba ni hulka ya kike, tunakufa kiume
3. Muwe tayari kujifunza.

Mkubali masahihisho. Kupingwa si kudhalilishwa. Kuwa na nia ya kujiboresha kwa kuhudhuria semina za maendeleo ya kibinafsi.

Kufanya hivyo sio udhaifu, bali ni ishara ya nguvu.
...
wivu huo
5. Nyenyekea mbele za Mungu.
naunga mkono
Wewe ni mwanadamu tu. Kiburi na upumbavu huwaweka watu wengi mbali na ibada. Mungu huwainua wanyenyekevu na kuwashusha wenye kiburi. Jinyenyekeze kwa Mungu na mambo yatakuendea vyema.
hujielewi
 
Wanaume mnaweza kujifunza kutoka kwetu wanawake.

Tuna mengi ya kuwashirikisha mjifunze kutoka kwetu wanawake, kwa leo nitawapa mambo matano tu....

"Wanaume wengi ni wabinafsi kwa asili na ni wachoyo wenye roho mbaya.
Bali wanawake wengi huweka maslahi ya familia kwanza.

Upendo wa kweli hauna ubinafsi. Watu wakuu wanaishi kwa ajili ya Mungu na wengine"
 
Asante rafiki yangu kwakuliona ilo
 
Ecoa5E1WkAAl0qF.jpg
vipi kuhusu mapozi kuna cha kujifunza?
 
Namba 1 umeiweka kibinafsi, mfumo wa utabaka wa kuwakubali aina fulani ya watu wenye interest na wewe.

Mfumo huo haufai kwa mwenye falsafa ya kirasta ya kuishi kijamaa.

Namba 5 itafanywa na wajinga
 
  • Kicheko
Reactions: G70
Wanaume mnaweza kujifunza kutoka kwetu wanawake.

Tuna mengi ya kuwashirikisha mjifunze kutoka kwetu wanawake, kwa leo nitawapa mambo matano tu...

1. Wape kipaumbele watu wako.

Wanaume wengi ni wabinafsi kwa asili na ni wachoyo wenye roho mbaya.
Bali wanawake wengi huweka maslahi ya familia kwanza.

Upendo wa kweli hauna ubinafsi. Watu wakuu wanaishi kwa ajili ya Mungu na wengine.
Mwanaume angekuwa mbinafsi asingekuweka ndani na kukuhudumia kwa kila kitu. Ubinafsi tunajua nani anao by nature

2. Ombeni msaada.

Acheni kutenda kwa nguvu kupita uwezo wenu huku mkiwa na huzuni ndani ya mioyo.

Wanaume wengi wameshuka moyo na ndoa nyingi huvunjika kwa sababu wanaume hawapendi kupata ushauri nasaha.

Kuomba msaada ni ishara ya kuongeza nguvu.
Naweza kukubaliana na wewe kwa hili.
3. Muwe tayari kujifunza.

Mkubali masahihisho. Kupingwa si kudhalilishwa. Kuwa na nia ya kujiboresha kwa kuhudhuria semina za maendeleo ya kibinafsi.

Kufanya hivyo sio udhaifu, bali ni ishara ya nguvu.
Hatuwezi kukubali kwa kusema "ndio", tuna namna yetu ya kukubaliana na mawazo yenu.
4. Fahamu mipaka yako.

Acha kujenga matumaini ya uongo kwa wanawake wengine. Acha kuahidi kile ambacho huwezi kutoa. Acha kujituma kupita kiasi katika sehemu yako ya kazi.

Epuka pia uchovu kwa kuwa na muda wa kupumzika mpenzi wako baada ya kazi .
Mwanamke bila kudanganywa haelewi somo
5. Nyenyekea mbele za Mungu.

Wewe ni mwanadamu tu. Kiburi na upumbavu huwaweka watu wengi mbali na ibada. Mungu huwainua wanyenyekevu na kuwashusha wenye kiburi. Jinyenyekeze kwa Mungu na mambo yatakuendea vyema.
Nakubaliana na wewe
 
  • Nzuri
Reactions: G70
Mwanaume angekuwa mbinafsi asingekuweka ndani na kukuhudumia kwa kila kitu. Ubinafsi tunajua nani anao by nature

Naweza kukubaliana na wewe kwa hili.

Hatuwezi kukubali kwa kusema "ndio", tuna namna yetu ya kukubaliana na mawazo yenu.

Mwanamke bila kudanganywa haelewi somo

Nakubaliana na wewe
Ni wabinafsi kwa kiasi chake
 
Pole, mwanaume ameumbwa kujitoshereza. Kama ni mkristo angalia laana aliyopewa adamu, Kwa jasho utakula na ardhi ikaamuliwa kuota nyasi na cheki ya Eva, kwa uchungu utazaa. Hivyo toka awali mwanaume lazima ugangamale ili maisha yaende. Hatuna cha kujifunza toka kwenu
 
Preeeach Pastor Figo 🗣️
I say again, "Preeeach Pastor Figo"
 
  • Nzuri
Reactions: G70
Sasa nimeelewa kwanini Pamela alikupiga doba!

Kwel dada zetu mama zetu tunawaheshimu, tunawapenda na tunawaskiliza sana.

Tatizo linakuja unapompa nafasi kubwa ya kumsikiliza mnafanya mambo flan ya kawaida na mepesi sana ataanza kukwambia tushone nguo za kufanana, atataka uadapt falsafa zake atakugombanisha na ndugu zako na vitu kibao ambavyo havina tija ya mda mrefu.
 
Hapana wachache ndio wana roho iyo sio wote
 
Back
Top Bottom